Pages

Pages

Thursday, August 1, 2013

MISS ILALA WAANZA KUJINOA KWA FAINALI


JUMLA ya warembo 15 kutoka katika vitongoji vinne vya wilaya ya Ilala, wameanza mazoezi ya kujiandaa na kumsaka mrembo wa wilaya ya Ilala ‘Redd’s Miss Ilala 2013’ yanayofanyika katika ukumbi wa klabu Billicanas uliopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Shindano hilo litafanyika katika ukumbi wa Golden Jubilee Tower tarehe 16 Agosti mwaka huu, kati ya hao warembo watatu ndio wanaowania nafasi ya kushiriki shindano la Redds Miss Tanzania, shindano linalotarajia kufanyika baadae mwezi Septemba.

Warembo hao ambao wanatoka katika vitongoji vya Mzizima, Tabata, Ukonga na Dar City Centre wamekuwa wakijifua na kufanya onesho hilo kuwa la kuvutia zaidi, tofauti na miaka iliyopita.

Maandalizi ya shindano hilo yanaendelea vizuri na wamepania kuonesha vipaji vyao kwa kufanya shindano la kuoesha vipaji ambalo linatarajiwa kufanyika wiki ijayo.

Sisi kama kamati tunaowaomba wadau wa urembo kujitokeza kwa wingi kuja kushuhudia muonekano mpya wa mashindano ya urembo, lakini pia kuangalia jinsi Ilala ilivyosheheni warembo watakaoleta ushindani mkubwa Redds Miss Tanzania 2013.

Warembo waliopo katika kambi ya Miss Ilala ni pamoja na Alice Isaac, Clara Poul,Anna Johnson,Iren Mwelolo, Munira Mabrouk,Rehema Mpanda, Shamim Mohamed, Martha Gewe, Diana Joackim, Natasha Mohamed, Dorice Mollel, Pendo Lema, Kazumbe Mussa na Kabula Kibogoti.

Hadi sasa kampuni zilizojitokeza kudhamini ni Redd’s, Dodoma wine,CXC Tours,Chilly Will,Tanzania Daima,Jambo Leo,Clouds FM,Tanzania Daima,City Lounge na Times FM. 

No comments:

Post a Comment