Pages

Pages

Tuesday, August 20, 2013

MUUMINI MWINJUMA NA WAZIRI SONYO WAZICHAPA KAVUKAVU

WANAMUZIKI wawili wenye majina ya kutisha, Waziri Sinyo na Rais wa zamani wa bendi ya Victoria Sound, wamepigana katika mazoezi ya bendi yao yaliyofanyika Mbagala, jijini Dar es Salaam. 

Katika kichapo hicho, inadaiwa kuwa Sonyo nusura amchome Muumini kisu, hivyo kuzua hofu katika patashika ya aina yake inayoendelea kuonyesha mgogoro mkubwa kati ya wanamuziki hao ndani ya Victoria Sound.

Akizungumza muda mchache baada ya kadhia hiyo, Muumini alisema alishangaa kujikuta yupo chini na Sonyo akiwa ameshatoa kisu kutaka kumjeruhi.
Muda mchache baadaye Muumini aliandika kwenye mtandao wa kijamii akielezea tukio hilo alilodai ni la aina yake huku akitumia lugha kali za kuudhi dhidi ya Sonyo.

“Leo ndio nimedhihirisha huyu ( hapa kuna tusi ila limefichwa kwa sababu za kiungwana) ni kweli yy amenikuta nimekaa tena pembeni na tahadhali zote ila alivyokuja kwangu kunivamia sikumkawiza nikampa ngumi 3 takatifu zilizolenga uso wake ndio akaona kumbe huyu mzima akatoa kisu mfuko wa kulia watu ndio wakamshika lakini wakati nakwepa kisu nilianguka kama sio George Gama ameshanijeruhi au kuniua kabisa ngoja nimfunze adabu nampeleka mahakamani ili iwe fundisho na kwa ili sina msalie mtume hivi jimwili lote la Sonyo Bado anamshikia mwanaume mwenzie Kisu na amshukuru Janurry aliyenipakata ningempukutisha meno kwa ngumi maana alikuwa kama kuku mgonjwa hakurusha hata ngumi," mwisho wa kuipitia meseji ya Muumini.

Kupigana kwa wanamuziki hao ni mwendelezo wa mgogoro mzito uliokuwapo kwa bendi hiyo baada ya uongozi pia kumuondoa katika nafasi ya urais Muumini na kumpa Kassim Muhumba, huku pia Sonyo akienguliwa katika nafasi yake ya kiongozi wa shoo.

No comments:

Post a Comment