Pages

Pages

Wednesday, August 21, 2013

SIFAZAMPONZA DIAMOND INSHU YA KUUZA UNGA

Baada ya msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya nchini Diamond Platnum kutajwa kujihusisha na mtandao wa dawa za kulevya waziri wa Uchukuzi Mwakyembe atoa agizo msanii huyo aanze kuchunguzwa.
Msanii huyo leo ameripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kujihusisha na dawa za kulevya.Uchunguzi huo utahusisha kuangalia vyanzo vyake vya mapato kama vinaendana na matumiz yake, wakati inasemekana  akaunti za diamond ambazo zinaonekana kubwa mno kulinganisha na kipato cha kawaida cha wasanii.
Hali hiyo imetokana na vugu vugu la kujaribu kuisafisha tanzania kutokana na kushamiri kwa madawa ya kulevya limefikia hatua nzuri na yakipee. Mh mwakyembe amejitoa haswa kupambana na hawa watu wauza unga, moja kati ya majina yanayosemekana ya wauza unga/punda ambayo yapo ktk kitengo internal intelligency lipo jina la msanii diamond.
Inasemekana diamond anaurafiki wa karibu na mabosi wa masogange, ambao wengine wapo nchini Afrika Kusini .kamera za cctv za uwanja wa wa ndege wa kitaifa JNA zimekuwa zikionesha ukaribu wa diamond na wale watu waliotajwa na waziri kuwa walimsaidia masogange kupitisha mzigo.
Pia safari za kimuziki sehemu mbalimbali duniani ambazo nyingi hupangwa/kutafutwa na vigogo wa madawa ya kulevya waliopo tanzania na wale waliopo Afrika Kusini .
Wakati pia sasa serikali inajaribu kuchunguza akaunti za diamond ambazo zinaonekana kubwa mno kulinganisha na kipato cha kawaida cha wasanii. Uchunguzi bado unaendelea, lakini diamond amekanusha kuhusika na sembe

No comments:

Post a Comment