Pages

Pages

Monday, September 30, 2013

BUKU TATU YAMUUMBUA MUIGIZAJI NORAH

STAA wa filamu za Kibongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ anadaiwa kumzaba makofi mhudumu wa Hoteli ya Lunch Time, Mabibo, Dar aliyetajwa kwa jina la Joyce Mashika.
Joyce Mashika.
Katika tukio hilo lililojiri wiki iliyopita hotelini hapo, ilidaiwa kuwa kisa cha yote hayo ni kufuatia Nora kudaiwa shilingi elfu tatu za Kitanzania, deni aliloliacha kwenye gharama ya hoteli ambapo alitakiwa kulipa shiling elfu 30.
Joyce aliwaambia wanahabari wetu kuwa Nora alifika hotelini hapo, akaomba chumba na alipoambiwa atoe fedha kwanza aliomba udhamini aingie hotelini kisha atalipa mpenzi wake akifika.
Joyce alidai kuwa walichukua muda wa nusu saa kukubaliana naye lakini baadaye walimpigia meneja wa hoteli ambaye alikubali Nora apewe chumba.
Alidai kuwa alipofika mpenzi wake ambaye ni mtu mzima, Nora alilipa shilingi elfu 20 na kuacha deni la shilingi elfu 10 aliahidi kulipa wakati anatoka.

Joyce alidai kuwa usiku Nora aliagiza chakula na wakati anakilipia akampa mhudumu shilingi elfu saba badala ya shilingi elfu 10 ambapo Joyce alizikataa. Baadaye meneja wa hoteli aliagiza zipokelewe.
Mhudumu huyo alidai kuwa asubuhi wakati Nora anaondoka, alimzuia na kumdai ile buku tatu na ndipo staa huyo akamzaba makofi huku akimkaba shingoni.
Joyce alisema aliamua kwenda kumfungulia jalada la kesi katika Kituo cha Polisi cha External, Dar kwa jalada namba RB/10153/2013-SHAMBULIO.
Joyce alisema kuwa alishangaa alipofika polisi alikuta Nora ameshafungua kesi akidai kufanyiwa fujo na kuibiwa fedha shilingi laki sita kwenye gari lake ambapo kesi hiyo ilihamishiwa kituo kikubwa cha Mbezi Kwayusuf, Dar lakini Nora hakutokea akiomba wayamalize mambo hayo.
Nora alipopigiwa simu na gazeti hili alidai kuwa waandishi waandike walichokisikia kutoka kwa Joyce kwani yeye hahitaji kuzungumza chochote.

No comments:

Post a Comment