Pages

Pages

Sunday, September 29, 2013

MAJAMBAZI YAPORA 150 ML BENKI YA I&M JIJINI DAR

Majambazi saba akiwemo mmoja ambaye amevalia sare za polisi wameiteka benki ya I&M  jijini Dar es Salaam na kuchukuwa fedha zinazohisiwa  kuwa  ni zaidi ya shilingi milioni 150 na kutokemea kusikojulikana.
Tukio hilo limetokea katika benki hiyo iliyoopo katika makutano ya mtaa wa Indira Gandi na Mosque ambapo baadhi ya mashuhuda wameelezea tukio hilo lilivyokuwa.   Akizungumza katika eneo la tukio kamanda wa polisi mkoa wa Ilala kamanda Marieta Minagi amesema bado wanaendelea kufanya uchunguzi wa tukio lenyewe ingawa  mpaka sasa ni kama milioni zaidi  150 zinahisiwa kuibiwa.   Naye mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meki Sadiki akiwa katika eneo hilo amesema  matukio ya Kuiba fedha katika benki yanazidi kushamiri na hivyo kuna haja ya taasisi husika kujipanga  upya.
  Hata hivyo ITV ilishuhudia baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo wakipandishwa katika gari la polisi lenye namba za usajili  T220 AMV na kuondoka  nao kwa ajili ya mahojiano  zaidi

No comments:

Post a Comment