Pages

Pages

Friday, September 6, 2013

MISS UNIVERSE TANZANIA KUHITIMISHA USAILI WA WAREMBO JUMAMOSI DAR ES SALAAM

       Miss Universe Tanzania chini ya kampuni ya Compass Communications inakamilisha jumamosi hii usaili wa warembo jijini Dar es Salaam.
Timu ya Miss Universe Tanzania ilifanya mchakato wa usaili na picha (scouting) katika mikoa 8 ambayo ni pamoja na Mwanza, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Dodoma, Manyara, Mtwara na Dar es Salaam.
Miss Universe Tanzania msimu huu utafanya fainali zake mwezi Septemba taehe 27 katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa (NATIONAL MUSEUM), Shaban Robert street jijini Dar es Salaam.
Mashindano ya mwaka huu umepata wafadhili mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mohamed Enterprises na Fastjet. Wadhamini wengine watajulikana ndani ya siku chache. Wadhaimini wote watatambullishwa wiki ijayo.
Kuhusu Miss Universe Tanzania:
Miss Universe Tanzania ilianza mashindano yake mwaka 2007 na mshindi wake alikuwa Mwanamitindo Flaviana Matata na aliweza kuitoa kimasomaso nchi yetu ya Tanzania kwa kushika nafasi ya Sita kidunia.Mwaka uliofuata, 2008 mrembo Amanda Ole Sululu alimrithi Flaviana Matata na kuvaa taji la Miss Universe Tanzania 2008 akifuatiwa na mrembo Illuminata James mwaka 2009, kisha Hellen Dausen mwaka 2010. Baadae taji lilichukuliwa na Nelly Kamwelu 2011 na mwaka jana 2012 taji lilinyakuliwa na mrembo Winfrida Dominic.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na MWANAKOMBO SALIM 0655 441165, SEIF KABELELE-0713302075 USAHILI WA DAR ES SALAAM UTAFANYIKA KESHO TAREHE 7-9-2013 PALE NYUMBANI LOUNGE KUANZIA SA NNE ASUBUHI

No comments:

Post a Comment