Pages

Pages

Sunday, September 29, 2013

MISS UTALII TANZANIA KUMTANGAZA NYATI MWEUPE DUNIANI

Miss Utalii Tanzania 2013, Hadija Said Mswaga, amesema kuwa kupatikana kwa nyati mweupe wa ajabu na pekee duniani katika hifadhi ya Ngorongoro, imekuwa ni chachu na kichocheo cha pekee kwake katika mpango mkakati wake wa kuitangaza Hifadhi ya Ngorongoro kitaifa na kimataifa, ambapo kwa kuanzia ameamua kuanza kampeni hiyo kupitia mashindano ya dunia anayokwenda kushiriki ya Miss Tourism World 2013, ambayo mwaka huu yanafanyikia nchini Equatorial Guinea Octoba 12, 2013.
Kupatikana kwa Nyati huyo wa ajabu Mweupe, ambaye hapatikani sehemu nyingine yoyote Duniani, wakati huu ambao anakwenda katika mashindano hayo ya Dunia, imekuwa ni fulsa ya pekee kwa Tanzania, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na kwake , kuithibitishia dunia kuwa Ngorongoro Cater ni Ajabu la Asili la Dunia Barani Afrika. Ambapo sasa Ngorongoro Crater  pamoja na maajabu ya bonde lenyewe la kreta ya Ngorongoro, pia kuna maajabu ya Nyati Mweupe, Unyayo wa Binadamu wa kale zaidi Duniani, Mchanga wa ajabu unao hama kila mwaka kwa umbo la Nusu mwezi, Mlima wenye Volkano Hai wa Oldonyo Lengai, lakini pia ushirikiano wa kuishi bila kudhuriana wa binadamu na Wanyama katika hifadhi hiyo na upatikanaji wa jamii karibu zote za Wanyama wakubwa (BIG FIVE) na adimu duniani wakiwemo Faru Weusi,Duma,Mbwa Mwitu, Kaka kuona n.k.

No comments:

Post a Comment