Pages

Pages

Thursday, September 26, 2013

MOJA YA AJALI MBAYA ZILIZOTOKEA WIKI HII














MNAMO TAREHE 26.09.2013 MAJIRA YA SAA 06:45HRS HUKO KATIKA MTEREMKO WA PIPE LINE INYALA BARABARA YA MBEYA/IRINGA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA. GARI T.605 AXX /T.480 CAX AINA YA SCANIA LORI LIKITOKEA NCHINI ZAMBIA KUELEKEA DAR – ES SALAAM LIKIENDESHWA NA DEREVA WILSON MACHA, AKIWA NA TINGO WAKE JUMA S/O SALEHE WOTE WAKAZI WA DSM [AMBAO KATIKA AJALI HIYO WOTE WAMEFARIKI DUNIA] LILIGONGA KWA NYUMA GARI T.548 BLY/ T.974 BVN AINA YA SCANIA LORI LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA SAMWEL ARON, MIAKA 30, MBENA, MKAZI WA SINZA, KISHA GARI HILO LILILIGONGA GARI T.876 BKV/T.465 BQU AINA YA IVECO LORI AMBALO LILIKUWA LIMEEGESHWA PEMBENI YA BARABARA LIKIWA LIMEHARIBIKA, LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA SAMWEL KASUSU, MIAKA 37, MJITA, MKAZI WA GONGO LA MBOTO DSM.
AIDHA GARI HILO T.605 AXX /T.480 CAX LIKIWA LIMEPOTEZA MWELEKEO LILIGONGANA USO KWA USO NA GARI T.255 AKV/T.272 CDZ AINA YA SCANIA LORI LILILOKUWA LIKITOKEA DSM KUELEKEA MBEYA MJINI AMBALO LILIKUWA LINAENDESHWA NA DEREVA SIXTUS S/O KAPINGA, MIAKA 35,MNGONI, MKAZI WA DSM AMBAYE ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO NA MWILI WAKE KUTEKETEA KWA KUUNGUA MOTO.
 KATIKA AJALI HIYO MAGARI MAWILI T.605 AXX /T.480 CAX NA T.255 AKV/T.272 CDZ YOTE YAMEUNGUA VICHWA NA KUTEKETEA NA GARI T.548 BLY/ T.974 BVN LILIUNGUA KIDOGO SEHEMU YA KICHWA UPANDE WA KULIA.
  CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA GARI T.605 AXX /T.480 CAX.
 MOTO ULIZIMWA KWA USHIRIKIANO KATI YA KIKOSI CHA ZIMA MOTO NA UOKOAJI KWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI NA WANANCHI.

No comments:

Post a Comment