Pages

Pages

Monday, September 23, 2013

MOTO MKUBWA WAJITOKEZA JENGO LA WESTGATE HUKO KENYA



Huku hali ya mshikemshike ikiendelea kushuhudiwa katika jengo la Westgate lenye maduka, ufyatulianaji risasi umesikika ndani ya jengo hilo lenye maduka na mikahawa zaidi ya themanini. Milio hiyo ilidumu kwa dakika tatu na kufuatiwa na moshi mkubwa juu ya jengo hilo. Hakuna taarifa kamili kuhusu kilichosababisha moshi huo.

Wapiganaji wa Al shabaab wamewateka nyara raia ambao idadi yao haijulikani. Walikuwemo ndani ya jengo wakiendelea na shughuli zao kuanzia Jumamosi mchana wakati wapiganaji wa Al shabaab walipowavamia na kuanza kufyatua risasi kiholela.
Inaarifiwa kuna maiti kumi katika ghorofa ya kwanza ya jengo hilo.

Aidha wapiganaji hao wanaoaminika kuwa wanachama wa Al Shabaab ni kati ya kumi na kumi na watano na bado wangali ndani ya jengo hilo.

Ripoti zinasema kuwa ufyatulianaji mkubwa wa risasi pamoja na milipuko imesikika katika jengo hilo kwa takriban dakika 15.

Harakati za kuendelea kumaliza operesheni hiyo zinaendelea lakini hali ya mateka walio ndani ya jengo hilo inaendelea kudorora.




Wakenya waliofanikiwa kuondoka katika jengo la Westgate kwa usaidizi wa polisi
Rais Kenyatta amesema kuwa jeshi linajitahidi kuhakikisha kuwa linakabiliana vilivyo na wanamgambo hao.
Helikopta za polisi zinazunguka juu ya jengo hilo pamoja na ndege za kijeshi kushika doria. Vikosi vya usalama vinaendelea na operesheni kujaribu kuwanusuru waathiriwa wakati hali ikiwa ni ya ati ati katika eneo la shambulizi.

Awali jeshi la Kenya lilisema limeweza kudhibiti jengo hilo lote ingawa bado limetaja hali kuwa tete mno hasa katika kujaribu kuwaokoa mateka waliosalia ndani ya jengo hilo.

Ripoti zinasema kuwa watu 69 wamefariki katika shambulizi hilo la Al Shabaab kufikia sasa huku 175 wakijeruhiwa. Baadhi wametibiwa na kuondoka hospitalini. Baadhi ya majeraha waliyopata ni majereha ya risasi na kutokana na guruneti ambalo Al shabaab waliwarushia wale waliokuwa ndani ya mikahawa siku ya Jumamosi.

Kundi hilo limekiri kutekeleza shambulio hilo kutokana na hatua ya Kenya kupeleka majeshi yake nchini Somalia ili kukabiliana na wapiganaji hao.

TIZAMA VIDEO YAKE HAPA CHINI
 VIDEO YA MOTO UKITEKETEZA JENGO

UPDATES:
Kenya imesema mateka wachache wamebaki ndani ya maduka ya kifahari ya Westage Mall yaliyovamiwa na wanamgambo wa kiislamu wa Al- shabab Jumamosi ambapo dazani za watu wameuwawa.
Kundi la kigaidi la wanamgambo la Al- shabab limedai kuhusika na shambulizi likisema kuwa linajibu kuhusu majeshi ya Kenya yaliyoko katika operesheni nchini Somalia.
Majeshi ya Kenya yalianza kufanya mashambulizi Jumapili  jioni katika maduka hayo ya kifahari ya Westage Mall kuokoa watu waliokuwa wamejificha au kushikiliwa mateka na watu wenye silaha.

No comments:

Post a Comment