Pages

Pages

Saturday, October 5, 2013

AJALI MBAYA YATOKEA MKOANI LINDI,BAADA YA MALORI YAGONGANA.

Mtu mmoja aliejulikana kwa jina la Burhan Islam(fundi wa gari) amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria aina ya Fuso kugonga lori lingine nae kubanwa na bodi na kuokolewa baada ya
jitihada zilizofanywa na baadhi ya Abiria waliokuwa wakisafiri katika barabara kuu ya Dar es salamu kwenda Mtwara na Lindi.
Gari hilo lenye namba za usajiri T 56ANQ lililokuwa likiendeshwa na Kunja Mshamu limepata ajali hiyo leo katika kijiji cha Mkwajuni wilayani Lindi baada ya kutaka kulipita gari lenye namba za usajili T 402 AJG Scania lililokuwa likiendeshwa na Amos Chadenyile na kushuhudiwa jitihada zilizokuwa zinafanywa kuokoa maisha ya kijana huo.Majeruhi huyo baada ya kuokolewa katika ajali hiyo alikimbizwa katika kituo cha afya kitomanga kwa huduma ya kwanza kabla ya kupelekwa katika hospital ya Mkoa wa Lindi kwa Uchunguzi zaidi
Katika ajali hiyo iliyousisha malori hayo hakuna majeruhi mwingine
aliepata jeraha huku gari hiyo ya Fuso likiwa limeharibika sana

No comments:

Post a Comment