Pages

Pages

Thursday, October 24, 2013

Kat Dahlia kupiga colabo na Navio

 
Msanii mwenye uwezo mkubwa na wa kipekee wa kurap kutoka nchini Uganda, Navio ameendelea kuchana mawimbi katika gemu, na hii ni baada ya kufanya kolabo nyingine na msanii Kat Dalhia kutoka Marekani.
Kolabo hii kali ni katika kazi ya mwanadada Kat ambayo inakwenda kwa jina Clock Strikes 12 ambayo itakuwepo katika album yake ambayo itatoka hivi karibuni, Album ambayo itasimama kwa jina My Garden.

Kazi hii mpya inatarajia kupanua zaidi wigo wa mashabiki wa msanii Navio kutoka Uganda hasa kutokana na idadi kubwa ya watu ambao wanafuatilia kazi za mwanadada Kat kutoka sehemu mbalimbali duniani.

 Kama humkumbuki vema tizama moja ya nyimbo zake ambayo mimi Metty naikubali sana.
VIDEO:(ganstar)

No comments:

Post a Comment