Pages

Pages

Thursday, October 24, 2013

KISANGA KISANGANI BLAZA: FUMANIZI LA MKE,MME WA MTU GUEST HOUSE

Live: Mume wa mtu, Emmanuel Benedict na mke wa mtu aitwaye Rehema baada ya kunaswa gesti saa 7 usiku.
Wawili hao walinaswa hivi karibuni kwenye gesti ambayo pia ina baa iitwayo Blue Roze maeneo ya Buguruni-Sokoni jijini Dar wakijiachia kwa raha zao.
Habari zilizopenyezwa katika timu yetu ni kwamba, baa hiyo hutumia vibaya leseni yake ya biashara kwa kugeuza gesti hiyo danguro ambapo machangu hufanya biashara ya kuuza miili yao katika eneo hilo.


  Aibu: Emmanuel na Rehema wakiwa na aibu wakati wakijiandaa kutoka chumbani.
Ilielezwa kuwa baa hiyo huwahifadhi machangudoa ndani yake huku biashara ya ngono ikifanyika mchana kweupe na usiku kucha bila kushtukiwa.
Ikiwa imebeba kauli ya Kamishina wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Suleiman Kova kuhusiana na kukomesha biashara ya madanguro jijini, mapaparazi walitinga ndani ya baa hiyo kama wateja na kukamilisha uchunguzi wao ambao uliwapa jibu moja tu – biashara ya ngono inafanyika nje nje!

Wakati huohuo, kijana mwingine wa OFM aliingia upande wa gesti iliyopo ndani ya baa hiyo ili kupeleleza bei zake huku mhudumu akiahidi kupunguza bei kwa kuwa alikuwa na changudoa kutoka ndani ya baa hiyo tofauti na wengine waliokuwa wanatoka nje ya eneo hilo.

TAARIFA POLISI

Baada ya kujiridhisha kuwepo kwa hali hiyo, OFM ilitoa taarifa kwa Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Ilala, Lucy Kakulu ambaye haraka alimtaarifu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi ambaye muda mfupi baadaye aliwasili kituoni hapo na kutoa baraka kwa OFM na kushiriki kuwachagua askari shupavu wa kufanya oparesheni hiyo.


Ilipotimia usiku wa manane, ndipo zoezi zima lilianza kwa mmoja wa mapaparazi wetu kuingia ndani ya baa hiyo na kupitiliza moja kwa moja hadi ndani ya gesti.

Akiwa ndani, paparazi huyo alifanikiwa kupatana na mmoja na kuingia naye chumbani huku akitoa ishara kuwa kila kitu kilikuwa wazi ni kiasi cha zoezi kufanyika tu.


No comments:

Post a Comment