MPENZI MPYA WA NORAH HUYU HAPA
SIKU
chache baada ya msanii wa filamu Bongo, Nuru Nassor ‘Nora’ kumwagana na
mpenzi wake Geofrey Kusila, sasa amezua gumzo baada ya kuibuka na
mwanaume mwingine mtandaoni. Risasi Mchanganyiko limenasa picha ya Nora
akiwa amepozi na mwanaume
huyo ambaye jina lake halijapatikana huku pembeni kukiwa na mbwa, katika
Mtandao wa Kijamii wa Instagram ikisindikizwa na maneno: “...na
mlivyosawigika kama huyu mbwa, mjipange nina hasira na nyinyi hadi Mungu
anajua.”
Paparazi wetu alivyomtafuta kwa njia ya simu, Nora
alisema: “Mimi ni mwanamke hivyo kuwa na mpenzi ni lazima na huyo
uliyemuona ni mwanaume, hivyo haina haja ya kujibu na kuhusu anaitwa
nani hiyo ni siri yangu, siwezi kuweka wazi jina lake kwa sasa.”
No comments:
Post a Comment