Pages

Pages

Sunday, November 17, 2013

AFANDE SELE ATANGAZA RASMI KUIUNGA NA CHAMA CHA CHADEMA LEO

Hatimaye msanii mkongwe wa bongofleva hapa nchini Afande Sele amefunguka leo na kusema kuwa hii leo anajiunga rasmi na CHADEMA, haya hapa chini ndiyo maneno yake kupitia facebook account yake
"Hakuna kusanda,hakuna kumbwanda,mbele kwa mbele makamanda,vua gamba vaa gwanda kisha kaza mkanda, wanashuka sisi tunapandaaa,,,,
Leo tunaanza kuandika historia mpya ktk mkoa wetu wa morogoro na tz kwa ujumla kwa sababu nikiwa kama msanii wa muda mrefu na mfalme pekee wa mzk wa kizazi kipya ninaetunga nyimbo zangu kwa kuzingatia ujumbe muhimu ktk jamii kwa mambo ya kisiasa,kiuchumi,elimu,amani na upendo nk,
Sasa leo nimeamua kwa ridhaa yangu iliyosukumwa na uzalendo na mapenz makubwa kwa taifa langu kuchukua kadi ya kujiunga rasmi uanachama wa CHADEMA,tukio hilo kubwa litafanyika leo jioni ktk mkutano wa hadhara utakaofanyika kata yetu ya mafiga/misufini na utahudhuriwa na viongoz mbalimbali wa chama kutoka makao makuu ya chama Dsm pamoja na mbunge wa nyamagana mh Ezekiel Wenje,kwa wakaz wa Moro wazalendo nyote mnakaribishwa saaana, ahsanteni wana'ndugu, siasa si uadui, tupingane/tusipigane, Pendo moja!,,,,”

No comments:

Post a Comment