Pages

Pages

Saturday, November 16, 2013

WAETHIOPIA 22 WAKAMATWA KUZAMIA TANZANIA

wahabeshi-300x169 77722
RAIA 22 wa Ethiopia wanashikiliwa na Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam kwa tuhuma za kuingia nchini bila kibali.
Akizungumza na Tanzania Daima ofisini kwake jana, Ofisa Uhamiaji Mkoa, Grace Hokororo, alisema Wahabeshi hao walikamatwa juzi usiku katika maeneo ya Kinondoni wakiwa katika pagale ambamo walikuwa wamejificha.(HD)

Alisema baada ya wananchi kuwaona waliwatilia mashaka na ndipo walipotoa taarifa polisi ambao walifika na kuwakamata.
"Hii hali ilikuwa imepoa lakini hivi sasa naona tena wameibuka kwa kweli kazi ipo na hawa tunategemea kuwasafirisha na kuwarudisha kwao wakiwemo Wanyarwanda tisa,'' alisema Hokororo.
Alisema wiki tatu zilizopota jumla ya wahamiaji 42 wakiwemo Wahabeshi, Wasomali na Wanyarwanda walisafirishwa na kurudishwa makwao.
Alisema pamoja na jitihada za idara hiyo kuwakamata raia hao, inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa watumishi na magari, jambo alilosema limekuwa likikwamisha jitihada za idara hiyo katika kutekeleza majukumu yake.
"Watumishi wengi wamechukuliwa na NIDA na hapa nimebakiwa na wachache na magari pia ni tatizo tunaiomba serikali iliangalie na ione umuhimu wa kutuongezea watumishi ili tuweze kufanya kazi vizuri," alisema.

No comments:

Post a Comment