Pages

Pages

Tuesday, December 10, 2013

Ajali mbaya ya Gari LIliloangukiwa na Mti Mkubwa huko Jang'ombe


Wananchi wakiwa katika harakati za kumuokoa dereva wa gari hili ambalo limeagukiwa na mti katika eneo la Skuli ya Jangombe wakati akipita katika barabara hiyo. Wakati mvua ikinyesha na kusababisha ajali hiyo.
 Kutokana na juhudi za wananchi na Kikosi cha Askari wa Uokozi cha Faya walifanikiwa kumuokoa dereva huyu aliyejulikana kwa jina la Ali Abdulrahaman Juma (Chatne)alikuwa akiendesha gari yenye usajili wa namba  Z 249 AK.   
Askari wa Kikosi cha Uokozi Zanzibar Faya wakisaidiana na Wananchi kumuokoa Ali Abdulraham, baada ya kuangukiwa na mti katika maeneo ya barabara ya skuli Jungombe akiwa katika safari zake
Wananchi wakimtoa dereva katika gari hiyo kwa kumkimbiza hospitali ya mnazi mmoja kwa matibabu zaidi, amepata majeraha kwa kuangukiwa na mti huo. 
 Hii ni sehemu ya dereva ilivyoharibika katika ajali hiyo, katika gari hiyo alikuwa dereva peke yake na kupata majaraha na kukimbizwa hospitali ya Mnazi Mmoja kwa matibabu zaidi. 
                       Hivi ndivyo ilivyokuwa katika ajali hiyo katika barabara ya jangombe. skuli.

No comments:

Post a Comment