Pages

Pages

Friday, May 16, 2014

kumekucha miss ubungo 2014

Baadhi ya washiriki wa Miss Ubungo 2014 wakiwa katika pozi. 
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Meneja Miradi wa Kampuni ya AKO Group Ltd, Honesty Minde, alisema wameamua kudhami ni shindano hilo ili kusaidia kulifanikisha.

Alisema wameamua kuwasaidia waandaaji wa shindano hilo ili kukuza sanaa ya urembo, wakiamini kuwa ndio dira ya maendeleo kwa Watanzania wote.
Baadhi ya washiriki wakiwa katika pozi kwenye clabu ya Ako Labamba.
“Tuliamua kuwapa maeneo ya kufanya mazoezi pamoja na huduma nyingine muhimu kwa waandaaji na warembo wao. “Naamini kwa pamoja tutafanikisha kwa vitendo mafanikio makubwa ya Miss Ubungo mwaka huu, ukizingatia kuwa ndio lengo letu,” alisema.

Wadhamini wengine katika shindano hilo ni Sigmark Tanzania, Prima Hair, Smart Bol, Handeni Kwetu Blog, MG Hostel, City Park Hotel, Milladayo.com, Dartalk na Nelson Fashion.

No comments:

Post a Comment