Pages

Pages

Monday, May 19, 2014

...Lupita Nyong'o kuigiza filamu moja na Eminem..

Muigizaji aliyepata umaarufu zaidi kupitia filamu ya 12 Years a Slave amepewa nafasi nyingine ya kuigiza katika filamu nyingine kubwa itakayowahusisha watu maarufu akiwemo rapper Eminem.
Kwa mujibu wa Fashion Times, Lupita anatarajiwa kuigiza kwenye filamu ya ‘Southpaw’ kama mfanyakazi wa mcheza masumbwi ambaye alikuwa juu na akashuka ghafla ambaye anafanya juu chini kurudi kwenye rekodi yake ya awali.
Katika filamu hiyo itawahusisha watu wengine maarufu akiwemo rapper Eminem, Jake Gyllenhaal, Forest Whitaker, Rachel McAdams na wengine.  
Lupita pia amepata shavu la kuigiza kwenye flamu nyingine mbili ambazo zimetajwa kuwa ni ‘A Most Wanted Man’ na ‘Taken’.

No comments:

Post a Comment