Pages

Pages

Wednesday, May 28, 2014

WANACHAMA WA SIMBA WAANDAMANA NA KUFUNGA NJIA ZA MSIMBAZI WAKITAKA WAMBURA ARUDISHWE KWENYE ORODHA YA WAGOMBEA

 Wanachama wa simba wakiwa wamelizunguka Jengo la klabu yao mchana huu kupinga kuondolewa kwa wambura kwenye uchaguzi wa klabu hiyo
 Wanachama wa Simba wakipiga kelele nje ya jengo la klabu yao hiyo wakitaka wapewe ufafanuzi wa kina kwanini wambura ametolewa kwenye uchaguzi unaokuja
 Mmoja wa wanachama wa Simba akiongea na mamia ya wanachama nje ya jengo la klabu hiyo kutaka wambura arejeshwe mara moja kwenye orodha ya wagombea

 Hapo mmoja ya wanachama waliojikusnya akiwatuliza wanachama wenzake ili waweze kupatamaelezo
 Polisi wakiwa wamefika eneo la klabu ya simba ili kuimarisha ulinzi na kuwataka wanachama wa simba kutulia ili wapate majibu kwa kamati ya uchaguzi
Mamia ya wapenzi na washabiki wa klabu kongwe ya mpira wa miguu hapa nchini Simba leo mchana wamejikusanya kwa wingi na kupinga Michael Wambura kuondolewa kwenye orodha ya wagombea kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Wanachama hao ambao walizunguka jengo hilo na kutaka wapewe sababu za msingi kwanini Wambura ameondolewa huku wakitaka kufanya vurugu lakini vyombo vya usalama waliwahi kufika eneo la tukio na kuweza kuwatuliza wanachama Hao.

No comments:

Post a Comment