Pages

Pages

Monday, June 2, 2014

KIFO CHA GEORGE TYSON CHAZUA MINONG"ONO KIBAOO..!!

Tatizo! Huku macho ya waigizaji na wadau wake hayajakauka machozi kufuatia vifo vya ghafla vya mwongoza sinema, Adam Philip Kuambiana (38) na mwigizaji Sheila Leo Haule ‘Recho’ (26), tasnia imempoteza mwingine, mwigizaji, prodyuza na mwongozaji filamu mahiri, George Otieno ‘Tyson’ (41).

Kufuatia kifo hicho ambacho pia ni cha ghafla, wadau mbalimbali wa filamu, wakiwemo wasanii wenyewe wamesimamia mawazo yao kwamba lazima kuna kitu!
Tyson alifariki dunia Ijumaa usiku akiwa njiani kukumbizwa Hospitali ya Mkoa ya Rufaa Mkoa wa Morogoro kufuatia ajali mbaya ya gari iliyotokea maeneo ya Gairo, Morogoro.
Katika ajali hiyo, mbali na marehemu walikuwemo watu wengine watatu ambao ni dereva, MC Gladness Chiduo ‘Zipompa’ na mwingine aliyejulikana kwa jina moja la Nick ambao walijeruhiwa vibaya na kupatiwa matibabu ya haraka.
Msanii AY akisimamia utaratibu mzima wa kuandaa jeneza kwa ajili ya msiba wa marehemuGeorge Otieno 'Tyson'.
WALIKUWA WAKITOKEA WAPI? Gari walilopata nalo ajali ni Toyota Noah ambalo liliharibika mno. Wote walikuwa wakitokea Dodoma ambako Ijumaa mchana walirekodi kipindi na pia kutoa misaada ya madawati 60 kwenye Shule ya Msingi ya Chalula iliyopo Chamwino kupitia Kipindi cha Mboni Show kinachoongozwa na Mboni Masimba kupitia Runinga ya EATV.
Mboni yeye kama bosi wa msafara huo alikuwa kwenye gari jingine na watu kadhaa.
KISA CHA AJALI Kwa mujibu wa chanzo, ajali hiyo ilitokea baada ya tairi la nyuma la kulia kupasuka ghafla kisha kufuatiwa na la mbele kushoto hali iliyosababisha gari hilo kupinduka na kubiringita mara tatu.
“Kwanza ilipobiringita mara moja, Tyson alichomoka kwenye gari, likabiringita tena mara mbili. Marehemu alipasuka sehemu ya kati ya paji la uso,” kilisema chanzo na kuanza kulia.
Marehemu Tyson akiwa na mwanaye Sonia enzi za uhai wake.
MANENO YA MWISHO YA MAREHEMU Chanzo kilizidi kusema kuwa wakati marehemu anazingirwa na roho wa mauti alikuwa akisema ‘najua nakufa lakini nasikitika kuwaacha wanangu.’
KUNA KITU Kwa upande wa wasanii kutoka tasnia ya filamu Bongo waliozungumza na paparazi juzi, walikazia dhana ya kuwepo kwa kitu kinachoondoa uhai wa wasanii kwa njia ya kufumba na kufumbua.
Marehemu Tyson akiwa katika picha ya pamoja na Mboni Masimba wa Kipindi cha Mboni Talk Show kupitia Runinga ya EATV, enzi za uhai wake.
“Haiwezekani kila kukicha sisi tu. Tena ghafla. Aisee lazima kuna kiti japokuwa hatujakijua ni kitu gani,” alisema msanii na kiongozi wa Kundi la Jakaya Theatre, David Mponji ‘Lazi’.
Akaongeza: “Lakini nataka kukwambia kwamba huu ni mpango wa Mungu kabisa ili tufanye ibada. Unajua asilimia themanini ya wasanii hawaendagi kanisani wala misikitini? Hapa sasa tunakumbushwa.”
JACOB STEVEN ‘JB’: “Hii ni too much! Kweli kifo sasa hata mimi nakiona kiko karibu. Nadhani kuna kitu.”
Gari aina ya Toyota Noah baada ya ajali iliyotoa uhai wa George Tyson.
WILLIAM MTITU: “Da! Sijui mimi niseme nini. Nadhani iko sababu ya kujiangalia, inakuwa kama kuna kitu vile.”
JACQUELINE WOLPER: “Siamini aisee! Yaani juzi tu Kuambiana, akaja Recho, leo Tyson! Mh! Pana kitu hapa. Afadhali tungekuwa tumelia mpaka tumekauka machozi.”
WACHUNGAJI, SHEHE WAMSHUKIA MTABIRI “Ukisema tabiri maana yake umba jambo. Ndiyo maana hata kwenye maandiko Mungu alimwambia nabii mmoja atabiri mafuvu kuwa binadamu, ikawa hivyo.
Marehemu Tyson enzi za uhai wake.
“Sasa huyu mtabiri (hakumtaja jina) ambaye amekuwa akisema wasanii watakufa kwa wingi ndiye ‘mchawi’ wao maana anaumba vifo kwa wasanii,” alisema Mchungaji Daniel Rashid wa Kanisa la EAGT Tegeta jijini Dar.

Mboni Masimba akilia kwa uchungu mara baada ya kupata taarifa za msiba.
Naye shehe aliyejitambulisha kwa jina la Hussein alipozungumza na paparazi juzi alisema yeye anaamini mtabiri ambaye amekuwa akisema wasanii watakufa ndiye mchawi wao. “Kwanza kwa nini uwatabirie wenzako tu? Kuna nini hapo? Mbona sijawahi kusikia amejitabiria mwenyewe?” alihoji Shehe Hussein ambaye hakupenda kuuanika msikiti anaofanyia utumishi wake.
WOSIA MZITO KWA MASTAA Katika hatua hiyo, viongozi hao wa dini walitoa wosia kwa mastaa wakisema kwamba katika hali kama hii hakuna njia mbadala zaidi ya kufanya ibada. Walisema huenda pia vifo hivyo ni mpango wa Mungu ili kuwakumbusha kufanya ibada kwani wasanii wanaonekana muda mwingi wapo kazini kuliko kwenye nyumba za Mungu au hata kumkumbuka kwa maombi tu.

No comments:

Post a Comment