Pages

Pages

Monday, June 2, 2014

LAANA: MSICHANA WA MIAKA 15 ABAKWA NA WANAUME ZAIDI YA 38

Unyama: Msichana mwenye umri wa miaka 15 abakwa kwa zamu na wanaume zaidi ya 38
Kuna baadhi ya binadamu wana roho mbaya zaidi ya wanyama wakali wa mwituni na ukisimuliwa matukio waliyofanya unaweza kujiuliza kama kweli ni binadamu au ‘mashetani’!.
Siku mbili baada ya kuripotiwa habari ya kusikitisha ya wasichana wawili ndugu wa nchini India waliobakwa na baadae kunyongwa, mtandao wa MailOnline umeripoti tukio la ubakaji alilofanyiwa msichana mdogo mwenye umri wa miaka 15 na wanaume zaidi ya 38 nchini Malaysia.
Taarifa zinaeleza kuwa tukio hilo limefanyika Kaskazini mwa Kelantan, Malaysia, May 20 ambapo msichana huyo alienda sehemu fulani kukutana na rafiki yake mwenye umri wa miaka 17 lakini alijikuta akipelekwa kwenye jumba bovu wasiloishi watu.
Akiwa kwenye jumba hilo, msichana huyo alibakwa kwa zamu na wanaume hao ambao miongoni mwao ni kundi la watu wanaojihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya.
Msichana wa miaka 17 ambaye ni rafiki ya msichana huyo anasadikika kuwa ndiye aliyemtenezea mazingira ya kuingia mikononi mwa watu hao wanyama japo polisi wamesema wanaendelea na uchunguzi ili waweze kufahamu kama kweli msichana huyo alihusika kupanga njama ama na yeye alibakwa.
Polisi wa Malaysia wamewakamata watuhumiwa 13 hadi sasa na kwamba kati ya hao yupo baba na watoto wake wawili wa kiume.

No comments:

Post a Comment