Pages

Pages

Saturday, June 21, 2014

Sarkodie, Tiwa Savage na Mafikizolo kutumbuiza tuzo za BET 2014

Tuzo za BET mwaka huu zitatolewa wikend ijayo, July 28/29 mwaka huu huko Los Angeles Marekani na kushuhudia wasanii wengi wakubwa duniani wakiperform kwenye jukwaa hilo kubwa..

Majina ya wasanii wakubwa wa Afrika yaliyotajwa ni pamoja na rapper kutoka Nigeria, Sarkodie, Tiwa Savage wa Nigeria na kundi la Mafikizolo la Afrika Kusini ambao watajumuika na wenzao kuperform Live katika jukwa hilo, Jumamosi, June 28 huko Los Angeles.
Hii ni mara ya kwanza kwa wasanii walio kwenye kipengele cha International acts kuperform katika tuzo hizo kubwa na zenye heshima zinazoandaliwa na kituo cha Black Entertainment Television (BET).
 
Diamond Platinumz kutoka Tanzania ni miongoni mwa wasanii wanaowania tuzo hizo kwa mwaka huu, na yuko katika kipengele cha Best International Act akiwa na Mafikizolo, Tiwa Savage, Davido, Sarkodie na Toofan.

No comments:

Post a Comment