Pages

Pages

Friday, June 20, 2014

Watoto wa Will Smith hulala na nyoka 10 chumbani, wengine hawajafungwa.

Watoto wa Will Smith hulala na nyoka 10 chumbani, wengine hawajafungwa
Watoto wa Will na Jada Smith, Willow na Jaden wana mengi ya ndani ambayo wengi walikuwa hawayafahamu.
Kwa mujibu wa US Weekly, Willow Smith mwenye umri wa miaka 13 hulala na nyoka kumi chumbani kwake na baadhi yao hawajafungwa kabisa!
Lakini sio pekee ambaye ana mapenzi na nyoka hao, kaka yake Jaden pia huwachukulia nyoka wa dada yake kama wapenzi wake kwa kuwa huwa wanaingia chumbani kwake na kulala nae kitandani huku wakijizungusha mwilini kwake!
Willow ameshawazoea nyoka hao kwa kuwa alianza kuishi na nyoka wa kwanza mwaka 2008 wakati akiwa na umri wa miaka 7 tu.
Jada Pinkett aliwahi kulimbia jarida la Rebok mwaka jana kuwa yeye anawapenda sana nyoka na mwanae Willow pia amekuwa anawapenda daima.
“Anaweza kwenda kwenye store ya nyoka akachukua nyoka mmoja na akajizungushia. Sikuwahi kumgusa nyoka hapo kabla, na nilikuwa siwezi kuwashika…..nimekuwa nampenda Willow daima tangu mwanzo. Nilimwambia Willow, ‘umemfanyia mama msaada mkubwa. Umenisaidia kushinda uoga’..”

No comments:

Post a Comment