Pages

Pages

Tuesday, September 30, 2014

Weusi kuachia video tatu ndani ya wiki hizi mbili, Wampeleka director Mkenya mitaa waliozaliwa

Weusi kuachia video tatu ndani ya wiki hizi mbili, Wampeleka director Mkenya mitaa waliozaliwa
Kundi la Weusi linaloundwa na Joh Makini, G Nako, Nikki wa Pili, Bonta na Lord Eyez liko mbioni kuzitoa video tatu za nyimbo zao ndani ya wiki hizi mbili kuanzia leo.
Akiongea na tovuti ya Times Fm, msemaji wa kundi hilo Nikki wa Pili amesema kuwa wataanza kuachia video za ‘Sitaki Kazi’, I See Me ya Joh Makini na mwisho ‘Mavijanaa’ ambayo ni ngoma mpya ya G Nako aliomshirikisha Nikki.
“Tunakuja na video tatu ndani ya wiki mbili (kuanzia wiki hii). Kuanzia wiki hii zitaanza kutoka na itatoka mojamoja. Nafikiri zitapishana kwa wiki wiki lakini tunatoa video tatu.” G Nako ameiambia tovuti ya Times Fm.
Ameeleza kuwa video zote tatu zimefanywa na muongozaji wa Kenya, Enos Olik aliyeongoza video ya hit yao ‘Gere’ na zimefanywa katika maeneo tofauti, Arusha na Nairobi.
“Sitaki Kazi imefanyika maeneo ya karibu na mtaani kwetu. Na nimefanya Arusha kwa kuwa ni rahisi kumove kwa kuwa kule ndiko tumezaliwa kwahiyo ni rahisi kupata vitu vingi watu wengi wakatusaidia tofauti na tukifanya sehemu nyingine. Ndio maana Sitaki Kazi na Mavijanaa tumefanyia mitaa tuliuyozaliwa mimi na G-Nako. Tumefanyia Kaloleni, Mjini, River Camp…” Ameeleza G Nako.
Video ya I See Me imefanyika jijini Nairobi, Kenya.

No comments:

Post a Comment