Pages

Pages

Tuesday, September 2, 2014

Wizkid aeleza chanzo cha Beef kati yake na Davido

Video: Wizkid aeleza chanzo cha Beef kati yake na Davido
uimbaji wa Nigeria, Wizkid amezungumzia beef kati yake na Davido akigusia kiini cha tofauti yao iliyokuzwa zaidi na comments za mashabiki wao kwenye mitandao ya kijamii.
Wizkid amefunguka katika mahojiano aliyofanya na Olisa Abibua katika kipindi cha ‘The Truth’.
Ameeleza kuwa chanzo cha beef kati yao ni pale alipokuwa anatweet akitoka kwenye show Marekani lakini tweet hiyo ilichukuliwa tofauti na Davido aliyefikiria kuwa lilikuwa dongo kwake.

“Ile situation ilikuwa ya kuchekesha kwangu kwa sababu tulikuwa wote kwenye ndege moja. Nilirudi, nilikuwa natweet kweli kuhusu show yangu, nilikuwa naongea kuhusu show yangu. Nilikuwa na show New York kabla ya hapo, hiyo ilikuwa kama mwaka mmoja, miaka miwili iliyopita na ilikuwa mbaya. Vyombo vya muziki vilikuwa vibaya, eneo lilikuwa la ajabu…!
“Nilishuka uwanja wa ndege, nilikuwa naenda hotelini nilipofikia, nikapitia kwenye eneo la show, nikaona jina langu kwenye taa zinazongaa. Na nilikuwa ‘Wow’! Huyuni ni mimi!? “Nilishuka chini, nikapita picha, nikapost nikisema nafanya show sahihi, kwenye maeneo sahihi (I do Proper shows, proper venues). Watu wakaanza kuwaka na hisia zao.”
Nilipoona hivyo, ilikuwa kichekesho. Wote ulikuwa mchezo, sipati muda wala sina nguvu za kuomba. ‘show sahihi, eneo sahihi’ ndicho ninachofanya. Sasa kama unakasirika, kwa nini unakasirika? Haufanyi show sahihi kwenye maeneo sahihi? Nilikuwa siongei na wewe. Ninajisikia hivyo kama nafanya kitu kwa ajili yangu, nafurahia mafanikio yangu na unayachukia mafanikio yangu. Sijui cha kukwambia. Nikuchukulie kama rafiki ama adui? Sijui.”
Wizkid ameeleza kuwa kama alikuwa amesema vile bila kuwataja watu basi wasanii wote wa Nigeria wangechukizwa na kauli yake, na amehoji kwa nini ilikuwa msanii mmoja tu aliyekasirishwa na tweet hiyo.

No comments:

Post a Comment