Pages

Pages

Friday, October 3, 2014

Belle 9: Sioni Chemistry kati yangu na Diamond

Belle 9: Sioni Chemistry kati yangu na Diamond
Mwimbaji wa Bongo Flava kutoka Morogoro, Belle 9 hafikirii kufanya collabo na Diamond Platinumz hivi karibuni kwa kuwa bado haoni chemistry (muendano sawa) kati yao.
Akiongea katika Exclusive Friday ya kipindi cha Sunrise cha 100.5 Times Fm, Belle 9 amesema haoni kama kuna chemistry kati yake na mwimbaji huyo ingawa haweki mipaka ya collabo kati yao, ikitokea wamepata kitu wanaweza kufanya.
“Kama ikitokea nina wimbo ambao yeye anaweza kuplay part yake vizuri tunaweza tukafanya. Ikitokea mimi nimeandika wimbo ambao nahisi kabisa yeye akikaa atafit tunaweza tukafanya. Lakini sio chemistry hapo kwanza.” Belle 9 ameiambia Sunrise ya 100.5 Times Fm.
Mwimbaji huyo amesema hivi sasa anafikiria kufanya kazi na mzee Zahir Zorro au Banza Stone kwa ajili ya kupata kitu cha kipekee.
“Hawa vijana wanaimba vizuri. Kiwango kipo, sijasema sioni… lakini the same. Mimi ninahitaji kitu unique kwa sababu nahisi kwa kumshirikisha Zahir au Banza Stone hivi…yaani watu ambao mimi naweza kuchukua kitu pale. Kuna watu wengi ambao naweza kujifunza vitu vingi.” Belle 9 amefafanua.
Hata hivyo, amesema wasanii wapya wa kizazi kipya wanafanya vizuri sana pia na akawataja wengi aliowashirikisha kwenye nyimbo zao kuonesha jinsi anavyowakubali.

No comments:

Post a Comment