Pages

Pages

Saturday, October 18, 2014

FIESTA YAWATAMBULISHA T.I, DAVIDO, VICTORIA KIMANI NA WENGINEO LEO KABLA YA KUPANDA KWENYE JUKWAA LA FIESTAUSIKU WA LEO

Msanii TI akiingia katika Ukumbi wa Bongoyo uliopo katika Hoteli ya Sea Cliff Jijini Dar Es Salaam kwaajili ya kufanya mkutano na waandishi wa Habari kabla ya kupanda kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta muda mfupi ujao
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Bw Steve Ganon akiongea na wanahabari leo katika ukumbi wa mikutano wa Bongoyo uliopo katika Hoteli ya Sea Cliff Jijini Dar wakati timu nzima ya Serengeti na Prime Time Promotions ambao ndio waandaaji wa Tamasha la Fiesta walipokuwa wakimtambulisha msanii nguli kutoka Nchini Marekani TI kabla ya kupanda jukwaani Muda mfupi ujao katika Viwanja vya Leaders.
Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Bw Joseph Kusaga akitoa machache kabla ya kumtambulisha Msanii wa Muziki Kutoka Nchini Marekani TI ambae atapanda kwenye jukwaa la Fiesta muda mfupi ujao katika Viwanja vya Leaders.
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Ephraim Mafuru akitoa machache wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Hoteli ya Sea Cliff jijini Dar Es Salaam.
Baadhi ya wasanii kutoka mataifa mbalimbali ambao watapanda katika jukwaa la Fiesta leo
Msanii kutoka nchini Nigeria Davido akiongelea jinsi atakavyo wapagawisha watanzania leo katika jukwaa la Fiesta muda mchache ujao katika viwanja vya Leaders.
 Kijana wa Kitanzania ambae amemchora TI katika taswira ya Kimasai na kumkabidhi msanii TI kama Zawadi kutoka Tanzania
Wanahabari wakiwajibika wakati wa mkutano wa Kumtambulisha Msanii TI ambae atapanda katika jukwaa la Fiesta leo katika Viwanja vya Leaders.

No comments:

Post a Comment