Pages

Pages

Tuesday, October 21, 2014

LUNDENGA AZUNGUMZIA UTATA WA UMRI WA MISS TANZANIA 2014 SITTI MTEMVU

Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa mashindano  ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga (wapili kushoto) akifafanua kwa waandishi wa habari juu ya sakata la umri Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu (kushoto),katika mkutano huo Lundenga alitolea ufafanuzi swala la umri wa Mrembo huyo kulingana na vilelezo alivyopewa na mrembo huyo wakati akijiunga na mashindano hayo. Wengine pichani ni Miss Tanzania namba mbili, Lilian Kamazima na Katibu Mkuu wa Kamati ya Miss Tanzania, Bosco Majaliwa.
 
Aidha Lundenga alifafanua kuwa Washiriki wote hujaza fomu maalum zilizoandaliwa na Kamati ya Miss Tanzania, na katika fomu alizojaza mrembo wa Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu amejaza tarehe yake ya kuzaliwa ambayo ni Mei 31,1991 na hivyo kuwa ni sahihi kushiriki mashindano hayo. 
 
 Katika suala la kumvua taji hilo ama laa, Sitti Mtemvu, Lundenga amesema kamati yake haina mamlaka hayo bali ni Baraza la Sanaa la Taifa na Wizara husika ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. 

Lundenga aliendelea kusema kuwa Mashindano ya Miss Tanzania hayaruhusu mshiriki yeyote mwenye mtoto kushiri,hivyo katika swala la Sitti Mtemvu kuwa ana mtoto,hilo kalina ukweli wowote bali ni uvumi tu wa kwenye mitandao ya kijamii baada ya Mrembo huyo kuonekana akiwa katika picha na mtoto alieomba kupiga nae.

No comments:

Post a Comment