Pages

Pages

Wednesday, October 1, 2014

Mapya Yaibuka ! Gari Aina Ya BMW Alilozawadiwa Wema Sepetu Ni Kutoka Kwa Kigogo Mpenzi Wake Mpya !

Wema Sepetu ndani ya gari aina ya BMW alilopewa zawadi kwenye birthday yake
Mapya yaibuka gari la birthday alilozawadiwa Wema Sepetu !.......habari mpya toka kwa chanzo kilicho karibu na Wema Sepetu zinasema kuwa gari aina ya BMW alilozawadiwa Wema juzi likidaiwa kutoka kwa Martin Kadinda na wapambe wanaompenda Wema ni uzushi bali gari hilo linatoka kwa kigogo ambaye anadaiwa kuwa mpenzi mpya wa siri wa Wema Sepetu.
Chanzo hicho kikizungumza na mwandishi Jana kwa sharti la kutotajwa jina kilisema kuwa Kigogo huyo mpya wa Wema ni mfanyabiashara mkubwa ndani na nje ya nchi na wakati mwingine huwa nchini Congo kikazi na anajihusisha pia na biashara ya madini. Chanzo hicho kiliongeza kwa kusema kuwa kigogo huyo ndiye amenunua gari hilo BMW la rangi nyeupe na kumpa Martin Kadinda ampe Wema kwasababu kigogo huyo hataki kabisa kujulikana kwenye media na kuanza kuandamwa kama ilivyokuwa kwa CK aliyekuwa kigogo wa ikulu wakati anatoka na Wema Sepetu ambapo media hasa magazeti ya udaku na mitandao haikuwapa nafasi ya kufaidi kama wapenzi.

"Lile BMW alopewa Wema na Martin Kadinda nafikiri mliliona, sasa nakupa ukweli wa lile gari, aliyelinunua ni buzi jipya la Madam, ni kigogo mwenye pesa nyingi sana anafanya biashara nyingi pamoja na madini, huwa anaenda sana Congo, amenunua gari akampa Kadinda ampe Wema unajua walichokubaliana na Wema ni kuwa mapenzi yao yasishamiri kwenye media kama yale ya Wema na CK, huyo kigogo wa sasa hataki cheap publicity, Kadinda ni kiunganishi tu na anajua kila kitu"

"Kadinda atapata wapi pesa ya kununualia gari lile?, amedanganya watu,  baada ya Wema kuachana na CK zile mbwembwe zake mjini za kumwaga pesa si mliona wenyewe zilikauka but zimerudi mwezi sasa , hata zile pesa alizomwaga Madam kwenye show ya Skylite Band na alizomtunza Dogo Aslay pale Ya Moto Band hivi majuzi ni kutoka kwa huyu pedeshee mpya, anamhudumia madam fresh tu, si pia tumeanza kula bata kama kawaida yetu madam si yupo kapata buzi jipya ya nini kujipa mawazo ! Si mnakumbuka habari ya Wema kutawala media amenunua nyumba ya milion 400 then Kadinda kusema kama haya haya eti madam kanunua nyumba kuendana na hadhi yake ipo wapi sasa ile nyumba!" Kilisema chanzo hicho pasipo kuendelea kuzungumza kwa madai kinawahi sehemu flani.
Wema na gari alilozwafiwa BMW
Hata hivyo mara tu baada ya gari kuonekana baadhi ya watu walianza kuingiwa na wasiwasi kuwa ni kweli Diamond kamzawadia Wema gari aina ya Nissan Murrano jeusi lakini gari jingine la BMW  halitoki kwa Martin Kadinda kama ilivyoelezwa ambapo Kadinda inaonekana alisikia haraka minong'ono hiyo na kuandika maneno hayo hapo chini Instagram...........

No comments:

Post a Comment