Pages

Pages

Monday, July 20, 2015

THE STARS BAND YAZINDULIWA RASMI SIKU YA EID MOSI

Bendi mpya ya muziki wa dansi ijulikanayo kama The Stars Band iliyo chini ya Aneth Kushaba imezinduliwa rasmi siku Jumamosi ya Julai 18, siku ya Idd-Mosi ndani ya kiota cha Mzalendo Pub, Kijitonyama jijini Dar es Salaam huku ikisindikizwa na mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Barnabas pamoja na bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’.  
Mkurugenzi wa The Stars Band, Aneth Kushaba akijitambulisha kwa mashabiki wakenm  pamoja na azungumza na wapenzi wa bendi mpya ya The Stars Band wakati wa uzinduzi yeye binafsi alisema hawezi kusema yaliyopita bali wapenzi wa bendi hiyo wategemee makubwa kutoka kwenye bendi hiyo iliyozinduliwa siku ya Idd Mosi ndani ya kiota cha Mzalendo Pub
Mwimbaji wa Bongo Flava, Barnaba Elias aka Barnaba akiimba moja ya nyimbo zake huku akisindikizwa na waimbaji wa Bendi ya The Stars kutshoto ni Seghito na kulia ni Prince
Mwimbaji wa Bongo Flava, Barnaba Elias aka Barnaba akiendelea kutoa burudani ndani ya kiota cha Mzalendo Pub wakati wa Uzinduzi wa Bendi mpya ya The Stars iliyozinduliwa siku ya Idd - Mosi
RAIS wa bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma', Nyoshi El Sadat akiimba kwa hisia kali wakati wa uzinduzi wa bendi ya The Stars iliyofanyika kwenye kiota cha Mzalendo Pub siku ya Idd-Mosi
Wanenguaji wa bendi ya  Bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma wakiendelea kutoa burudani wakati wa uzinduzi wa bendi mya ya The Stars
Waimbaji wa Bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma wakiongozwa Rais wa bendi hiyo, Nyoshi El Sadat wakiendelea kutoa burudani wa wapenzi wa bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma pamoja naThe Stars Bandi
Ndani ya bendi ya The Stars ni full raha hapa waimbaji wa bendi hiyo wakionesha moja ya style yao kwa mashabiki waliofika kwenye uzinduzi huo

No comments:

Post a Comment