Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Friday, November 12, 2010

MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA

AMBULANCE KIJIJINI PETU.

USAFIRI NA MIUNDO MBINU.

KWAO MBOGA SABA KUJISEVIA KWETU MULO MUMOJA WA MANATI.

TWAISHI KAMA NYOKA.

DARASA KAMILIFU NA UPEPO MWANANA HAIHITAJI FENI WALA AIR CONDITION.

NYUMBA ANAYOISHI MWALIMU MKUU.

DARASA LA MWANANGU KARNE YA 21.

KWAO GESI NA UMEME.

MAKAZI YETU.

MAJI SAFI KWA KILA M... MWENYE HELA.

MAJI SAFI KWA KILA MWENYE NIA.

MAJI YETU KWAO MAJI TAKA.

HALI YAKUKATISHA TAMAA.

Thursday, November 11, 2010

MCHUJO WA GIRAFFE UNIQUE MODEL 2010 NI NOVEMBA 20 PALE GIRAFFE HOTEL

Wadau na washiriki wanaowania nafasi ya kushiriki Giraffe unique model mnataarifiwa kuwa tarehe 20 novemba utafanyika pale katika hotel ya Giraffe katika ukumbi wa Jetty 1 mnakaribishwa watu wote kushuhudia mchujo huo ila washiriki ni wanawake pekee

ENZI ZA UJANA WANGU ...WADAU !!!

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhT3FrovdCXYIVNnCRz2bnca3bW4arNFmr2-r3qpwlSo4SlWlU82aXczaX7sSH4zN9Klcd8DQDgpaTw0wQSL6KiW97ZPd5jGWt_XYKWkqrc34-SmmtG2bii3TPnfaVlg2cjOe5s83z84xvP/s1600/magse1.jpg

Monday, November 8, 2010

TAMASHA LA WIKI YA SEYCHELLES KUFANYIKA DAR

Balozi wa Seychelles, Maryvonne Pool, akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu Tamasha la wiki ya Seychelles inayotarajia kufanyika Nov 15-19 mwaka huu Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Msaidizi wa Balozi, Sauda Simba Kulumanga. Picha na Benjamin Sawe- Maelezo
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgSGVb_yrDvJFw2ueSD3lLsZD2BlSUcyNO3lQjHtvRTslDnr9ytIXJS8BBUVTbUuBXQ_RC_D0_3wKZDDFGp6G_DDUVXyyEPF1yDuo-3qj14jSxr7v90GoVzOTy0f_LS2HcZqCQMG63hBA_f/s1600/POSTER+FC_.jpg

Na Alistide Kwizela


Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) liko kwenye mikakati ya kuandaa kongamano kubwa la muziki linalotazamiwa kufanyika katika siku za hivi karibuni ili kujadili mwenendo mzima wa fani hii ikiwa ni pamoja na kujenga utambulisho wa muziki wa Tanzania.

Katibu Mtendaji wa BASATA Ghonche Materego aliweka wazi hilo wakati akifafanua masuala mbalimbali yaliyojitokeza kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila Jumatatu kwenye Ukumbi wa BASATA ambapo alisema kwamba,kongamano hilo pamoja na mambo mengine litakuja na majibu kadhaa ya changamoto mbalimbali zinazoikabili fani ya muziki nchini sambamba na kujenga heshima ya wasanii wa Tanzania ndani na nje ya nchi.

“Tunakusudia kufanya kongamano kubwa ambalo litahusisha maproducer, wadau wa vyombo vya habari, mapromota, wasanii wote wa muziki na wadau mbalimbali wa sekta ya sanaa ili sasa kwa pamoja tujiulize ni muziki gani tunaoutaka, fani yenyewe iendeje na ni kwa vipi tutajenga utambulisho wa muziki wetu na hivyo kuuzika kimataifa” alisisitiza Materego.

Aliongeza kwamba, muda umefika sasa kwa wasanii wa muziki na wadau wote kukaa chini na kukuna vichwa juu ya muenendo mzima wa fani hii kwani kwa muda mrefu kumekuwa na changamoto nyingi ambazo zimekuwa zikiibuka na kuzua wasiwasi wa fani hii kudidimia na kukosa muelekeo kama jitihada za makusudi hazitafanyika.

Alihoji tabia inayokua kwa kasi ya baadhi ya wasanii wa kitanzania kunakiri vionjo (beats) vya miziki kutoka nje hasa Marekani na kuonesha wasiwasi wa wasanii wetu kuja kuburuzwa mahakamani na hata kutozwa faini kubwa za fedha kutokana na kitendo hicho kukiuka sheria za kimataifa za hakimiliki na hakishirikishi.

“Mimi najiuliza sana hivi siku wasanii wa Marekani wakija Tanzania na kuwaburuza wasanii wetu mahakamani kwa kosa la kunakiri kazi zao bila ruhusa nani atapona kiama hiki?Nasema hivi kwani hili haliko mbali kutokana na ukweli kwamba, tunaingiliana nao sasa.Ni lazima haya tuyaangalie mapema ndiyo maana BASATA inaona ni muda muafaka sasa wa kuwa na kongamano hili la wanamuziki wote” alimalizia Materego.

Mada ya wiki hii kwenye Jukwaa la Sanaa iliwasilishwa na Mtangazaji wa ITV/Radio One,Maulid Kambau na ilihusu Mchango wa Maprodyuza wa Muziki Katika Kukuza Utambulisho na Soko la Muziki Tanzania ambapo alilenga kuwakumbusha wasanii na waandaaji wa muziki kujikita kwenye muziki wenye vionjo vya kitanzania na kuacha kabisa tabia inayoota mizizi ya kunakiri kazi za watu wengine.
 

Sunday, November 7, 2010

NAOMI CAMPBELL ACCUSED

    NAOMI CAMPBELL has "unequivocally" denied claims by her former agent, Carole White that she lied under oath in a fragrance lawsuit. Campbell was sued by Moodform in June this year after reportedly backing out of a contract to launch a perfume called Cat Deluxe with Kisses.
According to the New York Post, White wants Campbell to be investigated by the Manhattan DA for possible perjury, with the aim of having her criminally prosecuted. The supermodel is countersuing, claiming White misrepresented her role in the contract negotiations.
USIKU WA PAMBA FM ACADEMIA ULIVYOBAMBA WAKAZI WA SINZA



https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh7Qs9pMx8zi3qHkaURhyphenhyphenLwxMYadnD476uulcQ6N2GdOmLEHtpSqp-R8z3wC6xj4vbcBIN6dRhu-5ZbIlqXSWQFbms_CMzlJI5QsITBAZtI52OUZqGeS6ZrGBY47gUv9daybsk4AIraAOA/s1600/DSC_5501.JPG

TAMASHA LA MITISIKO-MBEYA


Kikundi cha black ninja kikionyesha umahili wao wa kareti kwenye tamasha la mtikisiko lilifanyika uwanja wa Sokoine Mbeya na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
TIMU YA TAIFA YA POOL YAENDA UFARANSA


Mkuu wa wilaya ya kinondoni JORDAN RUGIMBANA akikabidhi bendera ya taifa kwa nahodha wa timu ya pool ALLY AKBAR.
TIMU ya Taifa ya mchezo wa POOL imeagwa rasmi pamoja na kukabidhiwa bendera ya taifa tayari kushiriki kwenye mashindano ya DUNIA ya mchezo huo yaliyopangwa kufanyika nchini UFARANSA.
Wachezaji hao ambao wanaondoka usiku huu waliweza kupata nasaha kutoka kwa mkuu wa Wilaya ya KINONDONI , JORDAN RUGIMBANA ambaye amewataka wachezaji hao kucheza na kuonyesha nidhamu wakati wa mashindano hayo ikiwa ni pamoja na kurudi na ushindi
Naye kocha wa timu hiyo DENIS LUNGU na nahodha ALI AKBAR timu hiyo ipo tayari kushiriki katika mashindano hayo na kuliletea taifa heshma ingwa ni mara ya kwanza kwa TANZANIA kushiriki katika mashindano hayo
Kikosi cha timu hiyo kinajumuisha wachezaji SABA akiwemo mchezaji wa kike pekee VIOLET MREMA ambaye ndiye bingwa wa taifa katika mchezo wa POOL nchini.
Nchi THELATHINI kwa upande wa wanawake na wanaume zinatarajia kutoa wawakilishi wake kushindana katika mashindano hayo ya dunia.

Friday, November 5, 2010

MAMBO YA SWAHILI FASHION WEEK 2010

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhDqHsfghNG9sFikAjfwb8B64Bg-0_d-TEW3ff1CforDjjbaDXbj_HK48QLfdZFImQ7jQQ-FnFT6bkMLaPP9IuLhDo3YwLBsob4x9EJi5pe4FgS5kaXcgjRM3IxYKK0-vZTsSQrrcteGp0O/s1600/Models_wearing_Zamda_George_Collection_during_the_first_day_of_Swahili_Fashion_Week_2010__Picture_by_Japheths_Njagi.JPG

Miss Earth aondoka na matumaini ya kushinda Philippines.

MWAKILISHI wa Tanzania katika mashindano ya Miss Earth 2010, Rose Shayo aliondoka nchini jana kwenda Vietnam huku akiwa na matumaini makubwa ya kufanya vyema katika mashindano hayo.
Akizungumza kabla ya kuondoka, Rose alisema kuwa amejiandaa viliyvyo chini ya muandaaji ake, Maria Sarungi wa Compass Communications and bila shaka atafanya vyema katika mashindano hayo.
Rose amesema kuwa haendi kuwa msindikizaji katika mashindano hayo na atafanya kila aliwezalo ili kufanya vyema kama ilivyokuwa kwa Miriam Odemba mwaka 2008 nchini Philippines.
“Najua kuna kushinda na kushindwa, mimi sitarajii kushindwa kutokana na maandalizi yangu, nawaomba Watanzania wanipe sapoti kubwa wakati wote nikiwa kambini na siku ya mashindano,” alisema Rose.
Maria alisema kuwa, alisema mrembo huyo amejiandaa vizuri kwakuwa mashindano ya kumsaka mrembo huyo yalifanyika mapema mwaka huu.
“Mashindano ya kumsaka mrembo huyu yalifanyika tangu mwezi wan nne mwaka huu kutokana na hali hiyo alipata muda mwingi wakujiaandaa hali inayomuweka ka

WABUNIFU KADHAA WASHUKA DAR KWAAJILI YA SWAHILI FASHION WEEK

Baadhi ya Wabunifu wa Mavazi watakaoshiriki katika Swahili Fashion Week wakiwa katika picha ya pamoja.

Jukwaa la tatu la Swahili fashion Week linaanza leo katika viwanja vya karimjee jijini Dar es salaam na kudumu kwa muda wa siku tatu hadi tarehe 6 ya mwezi wa November 2010.
Katika jukwaa la mwaka huu jumla ya wabunifu 24 kutoka nchi za Afrika hasa zile zinazozungumza lugha ya Kiswahili wamejiandaa vya kutosha katika kuonesha kazi zenye viwango vya kimataifa.
“Tunashukuru kwani mipango yote inakwend kama tulivyopanga na tayari wabunifu wote wamefika kwa ajili ya shoo kabambe ambapo itakuwa na tofauti kubwa kulinganisha na zile zilizopita. Tayari wabunifu wote 24 kutoka Tanzania na nchi za Pan Afrika wapo tayari kwa shoo ya mwaka, inayoandaliwa nyumbani mwa Swahili Fashion Week.” Alisema Mustafa Hassanali muandaaji wa Swahili Fashion Week
“Kwa mara nyingine tena tupo na Swahili Fashion Week 2010, na kusaidia kukuza Sanaa ya ubunifu wa mavazi hapa nchini, pamoja na kuwakaribisha wageni wetu ambao ni wabunifu wa kimataifa. Southern Sun inajivunia kutokana na mchango wake inayotoa kwa Sanaa ya ubunifu wa mavazi Afrika na hii intupa fursa ya kuendelea kwa njia mbalimbali.” Alisema meneja mkuu wa southern sun Hotel Ndugu Adam fuller
Southern Sun hotel imekuwa nyumba ya Swahili Fashion Week toka mwaka 2009.
Swahili Fashion Week inafanyika kwa mwaka watatu sasa na itawashirikisha wabunifu 24 ambapo kwa mujibu wa ratiba, siku ya kwanza shoo itapambwa na Manju Msita (Tanzania),Sonu Sharma (Kenya),Shelina Ebrahim (Tanzania/Canada),United Against Malaria (Tanzania Various),Farha Sultan (Tanzania),Tanzania Mitindo House (Tanzania - Various), KemiKalikawe (Tanzania) na Asia Idarous (Tanzania)
Kwa upande wa tarehe tano, siku ya ijumaa mwanamitindo kutoka Tanzania Jamila Vera Swai tfungua pazia akifuatiwa na Marinella Rodriguez (Mozambique),Stella Atal (Uganda),Kooroo (Kenya),Zamda George (Tanzania),Mafi Designs (Ethiopia),Moo Cow (Kenya),Robi Morro (Tanzania),Made by Africa (Tanzania) na Asos Africa (UK)
Tarehe sita November siku ya mwisho ya jukwaa la Swahili Fashion Week, wabunifu wtakoonesha kazi zao ni pamoj na wabunifu wanane wanaochipukia waliofanikiwa kuingia fainali kupitia shindano la wabunifu wanaochipukia, Emerging Designers Competition (Tanzania - Various),Gabriel Mollel (Tanzania),Khadija Mwanamboka (Tanzania),KikoRomeo (Kenya), John Kaveke (Kenya), Chichia London (Tanzania/UK), Ailinda Sawe (Tanzania)
“ Pamoja na kuwakaribisha wageni wetu ambao ni wabinifu wa mavazi , pia Southern itatoa zawadi kwa gauni bora katika Swahili Fashion Week kwa huu , lengo ni kusaidia kukuza Sanaa ya ubunifu wa mavazi” Aliongeza Saphia Ngalapi, Swahili Fashion Week PR manager

Miss Tanzania Genevieve Emanuel mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwlimu J.K.Nyerere jana akitokea nchini China.
Warembo kadhaa wakiwapokea wenzao wakati walipowasili jana kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere wakitokea nchini China
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Itifaki Kamati ya Miss Tanzania Bw. Albert Makoye, pamoja na Mrembo wa Chuo Kikuu Kikuu Huria Christina Justine, na Miss Shinyanga 2010 Buduri Ibrahim kwa pamoja wakiwapokea Miss Tanzania 2010 Genevieve Emmanuel na mshindi wa pili Glory Mwanga kushoto kwa Genevieve, na Miss Temeke mshindi wa pili Anna Daudi ambao waliwasili jana kwenye uwanja wa ndege wa Mwlimu J.K.Nyerere wakitokea Sanya China katika mashindano ya urembo ya dunia.
Mrembo Anna Daudi na Glory Mwanga walikwenda Sanya China kumpa sapoti Miss Tanzania 2010. pamoja na Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania Bw. Hashimu Lundenga, Katibu Mkuu Bosco Majaliwa, na mama wa Miss Tanzania 2010 Mrs. Mary Emmanuel Mpangala.

Wednesday, November 3, 2010

RAIS SHEIN KUAPISHWA LEO ,ZANZIBAR AMANI NA UPENDO KULEJEA PANDE ZOTE

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjZ-mBWq5JIB7r0AAXV-T1snx1Uz71Ce7Wsh0BclgS9tpjA801IRVCNhdd24WcDKJSxZCH5_0zh2NXaPDVbT7G_O2N8h-ssf8Y60_wUaGXSah0cvS0ZuKuoodI0tFy8GqXKRfL6rgTplMRo/s1600/2.JPG

VICTORIA MARTIN APENYA MCHUJO WA SWAHILI FASHION WEEK 2010


Male Models waiting to audition at the model casting at the Southern Sun Hotel,victoria martin mwanamitindo maarufu nchini Tanzania amepita katika mchujo huo ni kazi na umuhimu wake atauwakilisha katika Giraffe unique model 2010 kama jaji mwanamitindo. 
                                            Selected Female Models for SFW 2010
Wajasirimali zaidi ya 50 watajumiika pamoja katika kuuza na kuonesha bidhaa za aina mbalimbali wanzozizalisha katika maonesho yanyojulikana kwa jina la Swahili Fashion Week Shopping Festival, maonesho yanayokwenda sambamba na onesho kubwa la mavazi linalowakutanisha wabunifu wa mavazi kutoka nchi za Afrika zinazozungumza lugha ya Kiswahili.
 
Swahili Fashion Week Shopping Festival itafanyika kuazia tarehe 4th hadi 6th ya mwezi wa November 2010 katika bustani ya Karimjee, na kuwashirikisha wajasiriamali kutoka Zanzibar na Tanga, Kirimanjaro, Mtwara na Dar es salaam.
“Hii ni mara ya kwanza kwa Swahili Fashion Week Shopping Festival kufanyika, lengo ni kutoa fursa kwa watu wa aina mbalimbali ambao watafika katika fashion show waweze kupata ladha ya tofauti na maonesho ya mavazi kwa kuona na kununua bidhaa mbalimbali ambazo ni adimu”. pia kuchangia kukuza dhana ya kupenda bidhaa zinazozalishwa Tanzania. Alisema Hamis Omar, Afisa masoko na mauzo wa Swahili Fashion Week.
Katika maonesho kutakuwepo na bidhaa kama vile nguo, mapambo ya aina mbalimba, vifaa vya mapishi, henna na vingine vingi. Maonesho yatakuwa wazi kuanzia asubuhi hadi jioni kwa muda wa siku  tatu, yaani tarehe 4, 5 na 6 ya mwezi huu kwa Novemba 2010.
“Wazo la kufanya maonesho haya limekuja kufuatia tathimini tulioipata mwaka jana, ambopo tuliona kwamba pamoja na kuwepo maonesho yalifanywa na wabunifu wa mavazi ya kuonesha nguo zao,  ambapo watu mbalimbali  waliofika katika maonesho walitaka kununua, ndio maana tukaja na tukio hili ili watu wa aina mbalimbali wawaeze kufurahi na kupata vitu adimu.” Aliongezea Hamis Omar.

Tuesday, November 2, 2010

MGOMBEA WA CHADEMA AZIRAI BAADA YA KUTANGAZWA USHINDI

  Haya ni baadhi ya maumivu na kutoamini baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi ambako kulimpelekea mgombea kuzimia ...ni hatari jamani inauma sana


HATIMAYE Chama cha Mapinduzi (CCM) kimefanikiwa kutwaa jimbo la Tarime ambalo lilikuwa likishikiliwa na chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa miaka mitano,huku mgombea wa CHADEMA, Mwita Mwikwabe akiangua kilio hadi kuzirai. Mgombea huyo alizirai baada ya matokeo kuhesabiwa tena na kubaini kuwa ameshindwa ,ambapo mgombea wa CCM, ambaye ni mtunzi wa vitabu, Nyabari Nyangwine,amefanikiwa kushinda kwa tafauti ya kura 730.
Akitangaza mataokeo hayo msimamizi mkuu wa uchaguzi jimbo la Tarime, Fedelis Lumato,alisema kuwa Mgombea wa CCM,Nyambari Nyangwine ameshinda kwa kura 28,064 huku mgombea wa Chadema Mwita Mwikwabe akipata kura 27334 ambapo aliyekuwa anatetea kiti hicho Charles Mwera wa CUF akiambulia kura 7368.
Lumato alisema kuwa mgombea wa NCCR-Mageuzi ,Peter Wangwe amepata kura 7811,mgombea wa UDP, Mchungaji Jacob Mwita ameambulia kura 185 akifuatiwa na mgombea wa TLP ambaye ni mwandishi wa habari na Mwanasheria Kichere Nyaronyo aliyepata kura 45 tu.
Aidha CCM imefanikiwa kutwaa halmashauri hiyo baada ya kupata madiwani 17 dhidi ya Chadema waliopata madiwani 12 na CUF wakiambulia kiti kimoja kutoka kwa aliyekuwa mbunge wa Jimbo hilo Mwera aliyepewa aliyepata kujifariji.
Kwa upande wa matokeo ya Rais Mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete, amepata kura 34930 sawa na asilimia 49 dhidi ya Mgombea wa Chadema 32470 sawa na asilimia 46 huku akifuatiwa na mgombea wa CUF aliyepata kura 1804 na mgombea wa APPT-Maendeleo Piter Kuga Maziray akiambulia kura 889sawa na asilimia 1.3.

Asilimia 42.5 ya wapiga kura katika jimbo la Tarime ambao walijitokeza kupiga kura katika jimbo lenye wapiga kura 160867 ambapo waliojitokeza ni 70907 jambo ambalo msimamizi wa jimbo hilo alisema inahitaji utafiti kwasababu katika miaka ya hivi karibuni wapigakura wamezidi kukosa muamko.
Hata hivyo licha ya kwamba CCM wameshinda shamrashamra zao ni za mashakamashaka kwani watu waliojitokeza kusherekea ni wachache walionekana hawajiamini kama wameshinda jimbo hili ambalo wamefanya kazi ya ziada na ngumu na hatimiye kufanikisha ushindi huo. Pamoja na zoezi hilo kumalizika hali ilikuwa tete tangu usiku wa kuamkia jana baada ya milio ya mabomu na risasi kusikika sehemu mbali mbali hadi jana mchama ambapo polisi walikuwa wanafanya kazi ya kutawanya makundi ya vijana wanadaiwa kuwa ni wafuasi wa CHADEMA waliokuwa wakiandama kupinga matokeo.

Christina Ricci, Kanye West Among Honorees at 2010 ACE Awards

 

New York – The Accessories Council celebrated the winners of the 2010 Accessories Council Excellence (ACE) Awards at their annual gala Monday night, Nov. 1, in New York, honoring the year's top contributors to the accessories industry, from brands to individual style makers.
Celebrities like Christina Ricci, wearing a glam leopard print strapless dress, her hair sleek and glossy, and the ever-dapper Kanye West, accepted awards for their iconic style. Ricci took home the "Style Evolution" award, while West won the "Verage Stylemaker of the Year" award.
Lauren Bush was given the "Humanitarian" award for her FEED Project tote bag, which to date has provided close to 55 million meals for children through the United Nations World Food Programme through sales of over 530,000 bags.
The big brand winners of the evening included Maria Sharapova and Cole Haan, for "Brand Collaboration," RACHEL Rachel Roy for "Brand Launch of the Year" and Tiffany & Co., winner of the "Hall of Fame" award.
Lanvin creative director Alber Elbaz, whose highly anticipated collaboration with H&M goes on sale Nov. 23, was voted "Designer of the Year."
On the retail side, Ed Bucciarelli accepted the award for Henri Bendel, "Retailer of the Year," and Mike George of QVC stepped in to receive the "E-tailer of the Year" award.
Other individuals honored by the Accessories Council included editor-in-chief of Paper magazine, Kim Hastreiter, who received the "Marylou Luther Award for Fashion Journalism" and Al Berg of Marchon Eyewear, winner of the "Business Visionary Award."
The ACE awards were founded in 1995 as a way of recognizing those who have made significant contributions in spotlighting the accessories industry, and winners are nominated and voted on by members of the accessory industry, retailers, the fashion press and the Accessories Council Board of Directors.

SUGU FLY HIGH..,HARAKATI KUENDELEZWA BUNGENI

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiuE7hNdNgYikrA6HoC8rlpwcf83qZs1lTSmpGEt6EaJI_B-E1C4RVSUQ9S_VEGYeIZXHrTEISXvhHpsE8Gx6wG7DGKMVXzidrZkQYc6aH3VNT31kg9xAT3PUouyQu-ndiJT8ENu7redUCw/s1600/Sugu.jpg

TAMASHA LA MTIKISIKO KUFANYIKA MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI!!

TAMASHA la Mtikisiko linalotarajiwa kufanyika katika mikoa ya Iringa na Mbeya, litafanyika Novemba 6 kwa Mbeya, Uwanja wa Sokoine, wakati Iringa litafanyika Novemba 13, huku kampuni ya Simu za Mikononi ya Vodacom Tanzanzania, ikidhamini kwa Sh Milioni 22.
Tamasha hilo limeandaliwa kwa mara ya nne mwaka huu na Ibony Entertainment ya mkoani Iringa na kupewa jina la 'Bata Mrefu', kwa nia ya kuwakutanisha viijana na wapenzi wa mambo ya burudani, huku pia likiwakutanisha vijana na kujadiliana vitu vinavyowakabili. Akizungumza na Gazeti hili, Mwakilishi wa tamasha hilo, kutoka Ibony, Leah Mbeyale, alisema kwamba tamasha hilo litashirikisha wasanii mbalimbali, wakiongozwa na bendi inayotamba kwa sasa, The African Stars Twanga Pepeta.
Pia kutakuwapo na michezo mingine, ikiwamo Pool table na masumbwi, huku wakiamini kwamba onyesho la mikoa miwili, litatumika kama sehemu ya kufurahia burudani za tamasha hilo lenye mguso mkubwa kwa mashabiki wa burudani. Kwa mujibu wa Leah, tamasha hilo la Mtikisiko, limepiga hatua kubwa baada ya kufanikiwa kuongeza mikoa ya kufanya tukio hilo na kuchangia kwa kiasi kikubwa kuongeza hamasa kwa wote watakaohudhuria.
"Tangu lianzishwe tamasha hili, limekuwa na mguso mkubwa mkoani Iringa, kitu kilichotuongezea hamasa na hamu ya kuona mikoa mingine wanapata fursa ya kusherehekea tukio hilo lenye dira na mguso kwa wadau wote wa Mbeya na Iringa. "Wadau waje kwa wingi, kwani kiingilio ni cha chini kabisa, Sh 5,000 huku ulinzi ukiwa wa kutosha wakati wote wa tamasha hilo, Novemba 6 huko Mbeya na hata Iringa pia kila kitu kitawekwa sawa ili kuwapatia kitu kizuri wadau wa mambo ya burudani kutoka kwetu," alisema Leah.
Naye Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Jackson Kiswaga, alifurahia kudhamini tamasha hilo, huku akisema kwamba litakuwa maalumu kwa wadau wao, kuifahamu vyema Vodacom na kusherehekea pia miaka 10, tangu kuanzishwa kwake. "Siku zote Vodacom inapenda kushirikiana na wadau wake katika mambo yote, huku wakiamini kwamba ndio fursa pekee ya kuwatumikia na kujitangaza kwao katika kuhakikisha kwamba kila kitu kinakwenda sawa," alisema Kiswaga.
Ukiacha Twanga Pepeta, pia wasanii wengine wa Bongo Fleva, akiwamo Juma Nature, Mh Temba, Chege, Niki wa 2, Barnabas, Loma, Izo B na wengineo, ambao wote kwa pamoja watahakikisha kwamba mambo yanakwenda vyema, huku waandaaji wakitafuta uwezekano wa Mh Joseph Mbilinyi, Mr Two, aliyeshinda ubunge, anakuwapo kwenye tamasha hilo la Mbeya.