Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Wednesday, April 27, 2011

KANUMBA NA RAMSEY NOAH....WAJA NA MOVIE!

ACTORS RAMSEY NOAH (NIGERIA) NA STEVEN KANUMBA (TZ)

Mwigizaji filamu toka TZ,Steven Kanumba amefanya kazi kwa pamoja na mwigizaji maarufu toka nchini Nigeria Ramsey Noah iitwayo Devil's Kingdom
Pia humo ndani kuna kipaji kipya kabisa,Kajala na mwanamuziki toka FM Academia Patcho Mwamba na Devil's Kingdom itakua kitaani soon mwezi ujao!

MBWANA MATUMLA ANOGESHA NGUMI ILALA

Bondia Mbwana Matumla (kulia) akioneshana umwamba wa kutupa makonde na Omari Bayi wakati wa tamasha la kuamasisha mchezo wa ngumi uliofanyika, Dar es Salaam jana mabondia wote wanajiandaa na mapambano yao yatakayofanyika mei mosi katika ukumbi wa PTA sabasaba Dar es salaam 

VITA VYA LIBYA VYAZADI KUUGAWA ULIMWENGU

Vita vya Libya vinachukuwa sura ya vita vya kidiplomasia kwenye jamii ya kimataifa, huku Urusi na Umoja wa Afrika zikisimama upande mmoja na Umoja wa Mataifa na nchi za magharibi zikisimama upande mwengine.

  Ushindi wa waasi wa Libya mjini Misrata dhidi ya vikosi vya kiongozi wa nchi hiyo, Muammar  Gaddafi, unaelezwa kuwa ni wa hatua moja mbele, moja nyuma, kutokana na vikosi vya Gaddafi kuendelea kuushambulia mji huo na kuongezeka kwa idadi ya wahanga.
  Taarifa za asubuhi ya Jumatano zimethibitisha kuwa maroketi kadhaa yamerushwa kutoka upande wa vikosi vya Gaddafi kuelekea bandari ya   Misrata na kuilazimisha meli ya Shirika la  Kimataifa la Wahamiaji ishindwe kutia nanga kuwaokoa wakimbizi.
  Meli hii ilikusudiwa kuchukua wakimbizi 550 wa Kiafrika, kati ya 2,000 waliokwama katikati ya vita. Kwa mujibu wa madaktari, wakimbizi watatu wa Kiafrika wameuawa na 20 kujeruhiwa kutokana na mashambulizi haya.
  Katika mji wa Kabao, ripoti zinasema kuwa mapigano makali ya Jumanne jioni yalimalizika kwa ushindi wa waasi, ambapo wanajeshi 45 wa serikali waliuawa na wengine 17 kukamatwa mateka. Waasi wamepoteza wapiganaji wawili na watatu kujeruhiwa.


MASHABIKI WA SEAN KINGSTON WAMTOA NISHAI

Artist toka Jamaica,Sean Kingston alikua nchini Zimbabwe kupiga showz kibao wakati wa sikukuu za Pasaka
Lakini baada ya kumaliza showz zake ilidaiwa kuwa alitupia kwenye mitandao ya Tweeter na Facebook account zake kuwa alitupa hela kwa fans wake wakati anapiga showz zake hizo 2 nchini Zimbabwe na kusababisha fans wake kusema sio kweli kuwa aliwatupia hela,na kwa sasa wanamuona Sean Kingston kama si mfano mzuri!


United yaichapa Schalke 2-0

Manchester United imepiga hatua kubwa kuelekea katika fainali ya Klabu Bingwa Ulaya, baada ya kuifunga Schalke katika nusu fainali ya kwanza nchini Ujerumani.
Giggs
  Giggs amekuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kufunga goli katika michuano hii
United wangeweza kufunga mabao mengi kabla ya mapumziko, kama sio uhodari wa kipa wa Schalke, Manuel Neuer.
  Hata hivyo United walipata bao la kwanza katika kipindi cha pili, baada ya Wayne Rooney kupenyeza pasi wa Ryan Giggs. Rooney baadaye alipachika bao la pili baada ya kupata pasi kutoka kwa Javier Hernandez.
  United itaikaribisha Schalke kwenye uwanja wa Old Trafford, Jumatano tarehe 4 mwezi Mei, kwa ajili ya mchezo wa pili wa nusu fainali.
  Iwapo watadhibiti ushindi wao, United itawakilisha soka ya England katika Fainali ya Klabu Bingwa Ulaya itakayochezwa kwenye uwanja wa Wembley.


   

Living Presidential? Diddy Gets Police Escort After NY Concert! Bloomberg Gets P’d Off As Result!


      As if the NYPD couldn’t f*** up any more they waste resources on providing a police escort to Diddy after an NYC concert last week.
      Apparently his original plan was to fly to the concert’s after party in a helicopter but that idea was shot down by authorities. In an attempt to keep up with his grand entrance in true “Diddy” style he arranged for the police escort. 
     The after party was in New   Jersey but the police only escorted him to the tunnel.
We’re not sure if was just for fanfare of if  Diddy actually feared for his safety. However, if you think about it, its a dope ass concept but is a huge waste of resources.  Major news outlets report that Mayor Bloomberg is pissed and the NYPD Commissioner’s head is probably going to be served to Bloomie on a stick.


Sunday, April 24, 2011

bREAKING NEEWS ...KONDA WA DALADALA NAE ATOA TIBA YA KIKOMBE..!!




MKAZI wa Mbagala jijini Dar es Salaam, ameibuka na kusema kuwa ameoteshwa na Mungu kutoa dawa kwa njia ya kikombe kutibia wagonjwa wenye maradhi sugu.
Dawa hiyo amedai Mungu amemuotesha kutoa dawa ambayo ni maji ya kisima, bomba na haichanganywi na chochote zaidi ya maji hayo.

Awali kijana huyo aliyekuwa akiabudu dini ya Ukristo na baadae kubadili dini na kuwa Muislam na ndipo ameoteshwa.

Awali imedaiwa kijana huyo alikuwa akifanya kazi ya ukonda katika daladala na hivi karibuni ameibuka na kudai kuwa ameoteshwa.

Kufuatia taarifa hiyo watu wameanza kujitokeza nyumbani kwa kijana huyo kupata kikombe cha dawa hiyo huku akiwa ameshika msaahafu mkononi.

Hata hivyo Kamanda wa Polisi Temeke, wanafanya jitihada za kufanya mahojiano maalum na kijana huyo na taarifa itatolewa kwenye vyombo vya habari.

Kijana huyu ni wa saba kujitokeza na kudai wameoteshwa na Mungu na wengine wamejitokeza katika mkoa wa Mbeya, Moshi, Mbeya, Iringa, Tabora na Morogoro, Pwani wote wakidai kuoteshwa na Mungu kutoa tiba kwa njia ya kikombe.



NGUMI KUPIGWA PANANDIPANANDI ILALA BUNGONI 


     MABONDIA wa ngumi za ridhaa wa mkoa wa Ilala wanatarajia kupanda ulingoni kesho katika ukumbi wa Panandipanandi, Ilala Dar es Salaam. ambapo kutakuwa na ngumi kutoka kwa mabondia mbalimbali toka pande zote za mkoa wa DAr es Salaam

     Tamasha hilo litakalokuwa likitimua vumbi kila wiki inatarajia kuwakutanisha mabondia wa Ilala na wa sehemu nyingine za Dar es Salaam ili kuweza kujipima nguvu katika kuinua mchezo huo katika mkoa huo.

       Katika Tamasha hilo kesho bondia Mbwana Matumla anayejiaandaa kwa ajili ya kushiriki katika kuwania ubingwa wa UBO pambano linalotarajia kufanyika siku ya Mei mosi katika ukumbi wa PTA dhidi ya Mkenya Gabriel Ochieng atachuana na mabonmdia Yohana Robert na Issa Sewa.

      Akizungumza Dar es Salaam leo, Mratibu wa Tamasha hilo kup itia Taasisi ya Kinyogoli foundation, Habibu Kinyogoli alisema mapambano yote yatakuwa katika raundi nne huku pambano la Mbwana likiwa katika uzito wa Kg 55 likiwa ni sehemu ya maandalizi ya pambano lake hilo.

     Alisema, mkakati huo wa kuanzisha Tamasha akishirikiana na kocha msaidizi wa timu ya mkoa huo Rajabu Mhamila 'Super D' utasaidia kuinua vipaji vipya vya mchezo huo kwa kiasi kikubwa kwani kutawajenga wachezaji kujikita katika mchezo huo na kuufanya kama ndio ajira yao.

   Alisema, katika kulifanikisha hilo anawaomba wadau mbalimbali kuwasaidia kuwadhamini ili waweze kufikia malengo yao katika kuinua vipaji hivyo.pia alisema kutakuwa na wageni waalikwa ambao watatoa mada mbalimbali kuhusu kuinua mchezo wa ngumi Tanzania akiwemo mdau wa ngumi.Innocente Melleck na mwingine Benedictor Hulilo ambao watakuwa wageni waalikwa.


 MAKAZI YA GADDAFI YABOMOLEWA
Waasi Mjini Misrata
  Mapigano makali yanaendelea mjini Misrata licha ya serikali kutangaza kusitisha mashambulio dhidi ya waasi
  Ndege za kijeshi za shirika la Nato zimeangusha makombra kwenye mkaazi ya Kanali    Muammar Gaddafi mjini Tripoli.
  Walioshuhudia wanasema makombora hayo yamesababisha uharibifu mkubwa kwenye eneo Bab al Azizia.
Waasi wakikatisha katika mitaa ya mji wa Misrata

  Milipuko hiyo inasemekana kuwa mikubwa zaidi kusikika mjini Tripoli na ilisababisha vituo viwili vya kitaifa vya televesheni kukatiza matangazo yao kwa muda wa nusu saa.
  Matangazo ya vituo hivyo Jamahiriya na Shababiya yalikatizwa muda mfupi baada ya saa sita usiku baada ya shambulio hilo la Nato mjini Tripoli.
  Majeshi ya Nato yamekuwa yakishambulia majeshi na kambi za jeshi za Kanali Gaddafi baada ya kuidhinishwa na baraza la usalama la   Umoja wa Mataifa. Nia ikiwa kuwalinda raia wa   Libya waliokuwa wakilengwa na majeshi.
Awali, Kiongozi wa Upinzani, Mustafa Abdel  Jalil amesema Kuwait imekubali kuwapa dola milioni 180 kama msaada, huku wakiendelea na mikakati ya kupambana na majeshi ya serikali ya kanali Gaddafi.
  Bw Jalili ambaye pia ni Mkuu wa baraza la kitaifa la serikali ya mpito nchini Libya, amesema wanahitaji msaada huo wa kifedha kwa wakati huu.
  Kwengineko mapigano makali zaidi yameendelea mjini Misrata licha ya serikali kutangaza kuwa inasitisha mapigano.
Lakini msemaji wa serikali Moussa Ibrahim amesema jeshi linajibu mashambulizi kutoka kwa waasi.



             POMBE SI CHAI MNENGUAJI AKUDO IMPACT AZIMIKA
  Katika nderemo za Pasaka, ndani ya Ukumbi wa Mango Garden Kinondoni, Dar, mrembo mpya wa Bendi ya Akudo Impact ‘Vijana wa Masauti’ katika safu ya unenguaji, Mariam Sagwa alijikuta akidondoka stejini na kuzimika kwa dakika kadhaa baada ya kupandwa na ‘mzungu’ wakati akinengua.


Hata hivyo, wanenguaji wenzake walimpiga ‘tafu’ ya kusimama lakini alionekana akiyumbayumba hadi alipotolewa stejini.





  WATOTO WABAKWA UBUNGO
         Uchunguzi wa blogu hii umebaini kuwa idadi kubwa ya watoto ombaomba wenye umri kati ya miaka minne mpaka kumi hubakwa na vijana wenye umri mkubwa zaidi kutokana na mazingira hatarishi wanayoishi ya kulala nje huku wakisumbuliwa na mbu,mvua,baridi na kubakwa hasa kwa wato wa kiume hulawitiwa .
         Duru za habari zinamuomba rais Jakaya kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali kuwanusuru watoto hao kwani wanaathirika kisaikorojia na kupoteza imani na malengo ya maisha ya baadae,pia ni kinyume na haki za binadamu kwa mtoto kuingiliwa kinyume na maumbile.
                 Vitendo hivi hufanyika kwa watoto waliopo maeneo ya ubungo tanesco,inauma sana jamani...!!


Mabomu yalipuka Nigeria


Milipuko ya mabomu Nigeria
      Mabomu matatu yamelipuka mjini Maiduguri kaskazini-mashariki mwa Nigeria, na kuua takriban watu watatu.
      Mabomu mawili yalilipuka kwenye hoteli na jengine kwenye kituo cha usafirishaji siku ya Jumapili usiku.
Polisi wamesema walioathirika wamepelekwa kwenye hospitali mbili tofauti mjini humo.
      Kundi la kiislamu la Boko Haram linalopinga vitabu vya magharibi limelaumiwa kwa mashambulio kama hayo ambalo limekuwa likipambana na majeshi ya usalama mjini hapo.
      Milipuko ya hivi karibuni imetokea kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa magavana siku ya Jumanne katika majimbo 36 ya Nigeria.
     Ghasia ziliibuka kaskazini mwa Nigeria kufuatia uchaguzi wa rais Aprili 16, ambapo Bw Goodluck Jonathan aliyetoka upande wa kusini aliibuka mshindi.
Mamia wanaaminiwa kuuawa na maelfu wamekimbia makazi yao.
     Haikufahamika iwapo milipuko hiyo ya mabomu mjini Maiduguri, mji mkuu wa jimbo la Borno, lina uhusiano wowote na ghasia hizo.




MISS KILIMANJARO YAANZA KULINDIMA..!!     Baadhi ya Warembo watakaowania taji la miss Kilimanjaro wakiwa katika pozi, Dar es salaam jana kabla ya kwenda kuweka kambi rasmi itakayoanza mwanzoni mwa mwezi ujao mkoani Kilimanjaro. kutoka kushoto ni Catherine Edwin,Diana Lymo na Jackline John

Catherine Edwin
Jackline John
Diana Lymo
Miss kilimnaro iedhaminiwa na Vodacom,Redds,Bamm solution,kilimanjaro bus service,kilimanjaro safari lodge,Africa sana pub,Rafiki min super market,Snow view hotelRahisi petrol stationMoshi fm,Fortune MountainresortVia africa busness solutionBen Expetation,OrientalBureau de change,www.uniqueentertz.blogspot.com na Shear Ellusion.


Arsenal yabomotwa 2-1 na Bolton

Matumaini ya Arsenal kuwania ubingwa wa ligi kuu ya England yamefifia zaidi baada ya kufungwa 2-1 na Bolton.
Bolton
Bolton
   Arsenal wakicheza chini ya kiwango chao katika kipindi cha kwanza walifungwa na Daniel Sturridge kwa bao la kichwa kufuatia mpira wa kona.
   Mapema katika kipindi cha pili, Kipa Wojciech Szczesny aliokoa mkwaju wa penati uliopigwa na Kevin Davies, na dakika moja baadaye Robin Van Persie kufunga bao la kusawazisha kwa Arsenal.
  Arsenal walikuwa na nafasi za kutosha kushinda mchezo huo, lakini walijikuta wakipoteza katika dakika ya mwisho.
Tamir Cohen aliunganisha kwa kichwa mpira wa kona na kuwapa ushindi Bolton.
  Arsenal walitakiwa kupata ushindi katika mchezo huu ili kuwa na matumaini ya kuwania ubingwa.



Watu 57 wameuwawa mapigano Sudan Kusini

     Katika vita baina ya jeshi la serikali na wapiganaji wakati Sudan Kusini inapojitahidi kupambana na uasi katika eneo hilo.
Raia wa Sudan Kusini
Raia wa Sudan Kusini
               Serikali ya Sudan Kusini inajitahidi kupambana na uasi wakati nchi hiyo inajitayarisha kujitenga na Sudan Kaskazini, ambapo uhuru unatarajiwa mwezi wa Julai.
Mapigano yalizuka baina ya jeshi la Sudan Kusini na wapiganaji wake wa zamani waliokuwa wakisubiri kujumuishwa kwenye jeshi la jimbo lenye mzozo la Jonglei.
               Zaidi ya wapiganaji 55 waliuwawa na wanajeshi na raia 70 walijeruhiwa.
Idadi hiyo huenda ikaongezeka, maelezo yakitolewa.
               Sudan kusini inajaribu kuzima uasi wa vikundi kama saba vya waasi, huku inakaribia uhuru kamili katika miezi mitatu ijayo.
               Umoja wa Mataifa unasema watu zaidi ya mia nane wameuwawa na 94,000 wamelazimika kuhama makaazi yao tangu Januari.
               Mzozo huo unatia wasiwasi kuhusu mustakbali wa taifa hilo jipya.
Katika siku za karibuni, watu wamehamishwa kutoka jimbo muhimu la mafuta la Unity, baada ya mapigano ya siku nne.
               Sudan Kusini imeishutumu serikali ya Sudan Kaskazini, kwa kuwasaidia wapiganaji wa kusini, madai ambayo yamekanushwa na kaskazini.


Dirty Money’s Dawn & Kaleena Sing The National Anthem For Knicks vs Celtics Game 3


       Dirty Money’s Dawn Richard & Kaleena hit up Madison Square Garden before their NY tour stop last night, to sing the National Anthem for the Knicks vs Celtics Game. The Celtics went on to beat the Knicks 113-96, placing them at a game away from shutting the Knicks out of the Eastern Conference playoffs.



  UJASILIAMALI WA WIKI

Mjasilia mali akiwajibika kutafuta ridhiki ya siku



Naomi Campbell to tie the Knot

 CampbellVlad
      After being embroiled in a blood diamond scandal, and cases of assault on her employees, Naomi Campbell is making headlines for a happier reason.Wedding bells are set to toll in what's going to possibly be the wedding of the year on December 7 & 8, 2010.
Naomi and her long time boyfriend Vladimir Doronin have set the date for the ceremony, which will take place in Egypt's grand Luxor Temple.The bride and groom reportedly will spend their honeymoon in Luxor at the Winter Palace Hotel. 
    Their bridesmaid will be their long time friend Dasha Zhukova, an entreprenuer and designer.
    Meanwhile, Vladimir Doronin is said to be still married to his wife Ekaterina, who he has been with for 21 years, and has a daughter with him. Vladimir is said to be Russia's version of Donald Trump.


TAIFA STARS YATUNDIKWA 2-0 NA MSUMBIJI







MABAO mawili ya mshambuliaji Jeremias Sitoe katika kila kipindi yameipatia   Msumbiji (Mambas) ushindi wa 2-0 dhidi ya Tanzania (Taifa Stars) kwenye mchezo wa kirafiki uliofanyika usiku (Aprili 23 mwaka huu) 


     Mechi hiyo maalumu kwa ajili ya ufunguzi wa uwanja huo wa kisasa uliojengwa na Wachina na wenye uwezo wa kuchukua watazamaji ilikuwa ya ushindani wa hali ya juu.


     Rais Armando Guebuza wa Msumbiji ndiye aliyezindua uwanja huo.Sitoe alifunga mabao hayo dakika ya 19 na 51 karibu kwa staili ileile baada ya mabeki wa kati Aggrey Morris na Nadir Haroub 'Cannavaro' kujichanganya katika kucheza mipira mirefu aliyopigiwa mshambuliaji huyo mwenye kasi na pia kudhani ameotea.

Friday, April 22, 2011

KWA STAILI WABONGO WATALILIA SANA KWENDA BIG BROTHER AFRICA..!!

Mtu mzima akizila zile bata za ndani ya jumba enzi zake mjengoni humo.
 
Hawa nao wakipata natural juice jikoni,vijana wa kibongo wakiona hivi watarogana kwenda huko.


BREAKING NEEWZ..!!.MTOTO WA SHIRIKO AFARIKI DUNIA

Shirko Loses Daughter

        
      Its a sad morning for the Mombasa music fraternity after one of their own lost his daughter today.
     Shirko of the famous sav clan music group who has a couple of hit singles under his belt like ni wewe which he did with 2berry from tanzania. He lost his daughter Salame earlier this morning after a short illness.
Hipipo.com sends a messege of condolences to the family during this trying time and may Allah rest her soul in peace.



KOMBE LA MFALME LAPASUKA
Copadelrey           Spain's most treasured football trophy, the King's Cup, slipped from the hands of a Real Madrid player Thursday, fell under the team bus and was reportedly crushed into pieces.
Defender Sergio Ramos held the 15 kg trophy above his head in an open-top bus as the triumphant team were about to enter Madrid's central Cibeles Square, packed with fans partying throughout the night.
But he lost his grip and the Cup, which Real Madrid got their hands on just hours earlier for the first time since 1993 after a 1-0 victory over Barcelona, fell in front of the bus.
         The team bus then ran over the silver trophy before stopping.
Police rushed to retrieve the Cup and gave it to the bus driver but it was not displayed to the public again. Emergency services workers picked up at least 10 pieces of the trophy, news radio Cadena Ser reported. "It fell, it fell, it's fine, it's fine," Ramos told reporters when asked about the slip.


MAJAMBAZI YAENDELEZA UNDAVA YATEKA MAGARI 20 POLINI
     WATU wanaodhaniwa kuwa na majambazi juzi walifunga barabara eneo la msitu wa Sao Hill wilayani Mufindi na kuteka magari zaidi ya 20 huku wakijeruhi abiria na madereva wa magari hayo.
     Katika tukio hilo, majambazi hao wakiwa na silaha mbali mbali za moto na zile za jadi kama mapanga na virugu waliteka magari mbali mbali katika barabara kuu ya Iringa –Mbeya na kufanikiwa kupora mali za abiria hao.
      Mmoja kati ya watu waliotekwa alimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa saba usiku na kuwa baadhi ya magari yaliyotekwa ni yale ya yenye namba za IT ambayo yalikuwa yakisafirishwa kwenda nchi za kusini mwa Tanzania yakitokea bandarini.
     Juma Sanga ambaye alikuwa katika gari la IT akisafiri kama abiria baada ya kukosa usafiri wa basi alisema walipofika katika eneo hilo ghafla walikuta magogo yametegwa barabarani na wakati wakijaribu kuyakwepa ndipo          walipojitokeza majambazi hao zaidi ya 20 ambao walianza kurusha risasi hewani na kutumia mapanga na virungu kuwaadhibu huku wakiwapora mali mbali mbali.
    “Majambazi hayo yalikuwa yamevalia mavazi ya kininja na kuwa yalikuwa zaidi ya 20 na wakati wengine wakipekua gari moja baada ya nyingine na kukusanya mali za wasafiri wengine walikuwa wakiendelea kuwaadhibu abiria kwa kipigo….wapo baadhi waliojeruhiwa sana walikimbizwa hospitali ya wilaya ya Mufindi baada ya polisi kufika kwa wakati kuwaokoa.”
    Alisema kuwa tukio hilo lilidumu kwa zaidi ya dakika 20 na baadhi ya abiria walifanikiwa kupiga simu polisi Mafinga ambao walifika kwa wakati eneo la tukio na majambazi hao kukimbilia porini.
    Habari zinaeleza kuwa katika tukio hilo hakuna mtu aliyepoteza maisha zaidi ya kujeruhiwa na kuporwa mali mbali mbali zikiwemo fedha, Laptop na mizigo mingine ambayo majambazi hao walipakia katika gari na kukimbia nayo.



  WATU 88 WAUAWA SYRIA

Idadi ya watu waliouawa katika maandamano ya kudai mageuzi ya demokrasia nchini Syria imeongezeka hadi kufikia 88.

Shirika la Haki za Binadamu la Amnesty International limetoa takwimu hizo kuuambatana na ripoti za wanaharakati wa nchi hiyo. 
Hiyo jana, vikosi vya usalama vya Syria vilifyatulia risasi na mabomu ya kutoa machozi katika mikutano ya upinzani iliyokuwa ikifanyika nchi nzima.
Waandamanaji nchini Syria  Waandamanaji nchini Syria
Kuendelea huko kwa maandamano ni dalili kwamba jaribio la Rais wa nchi hiyo Bashar al Assad kuzima upinzani huo uliodumu kwa mwezi mmoja na kusababisha machafuko pamoja na ahadi alizotoa za kufanya marekebisho, limeshindwa.
Rais al Assad na vyombo vya habari vya taifa, vimeendelea kulaumu njama zinazofanywa kusababisha machafuko katika maandamano hayo ya upinzani.
Waandamanaji Yemen  Waandamanaji Yemen
   Wakati huohuo, nchini Yemen nako, maelfu ya watu walikusanyika katika mitaa ya mji mkuu Sanaa na mji wa Taiz hapo jana katika maandamano ya kumpinga rais wa nchi hiyo Ali Abdullah Saleh.


NAULI ZAPANDA STENDI YA UBUNGO
    NAULI za mabasi yanayokwenda mikoani kuanzia Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo (UBT), imepanda mara dufu na kusababisha abiria kutapeliwa kwa kuuziwa tiketi hewa na wengine kushindwa kusafiri jana.

Vurugu zilianza kujitokeza saa 12:00  asubuhi, baada ya abiria wanaodhaniwa kusafiri kwa ajili ya Siku Kuu ya Pasaka kufika kituoni hapo na kubaini kupanda kwa nauli ghafla na kuwapo kwa mabasi machache kuliko kawaida.

   Kutokana na hali hiyo daladala zinazofanya safari katikati ya Jiji la Dar es Salaam, vikiwamo `vipanya’ vilijitosa kituoni hapo na kusafirisha abiria kwenda katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro kwa bei ya kuruka.

   Uchunguzi ulibaini kuwa nauli kutoka Dar es Salaam kwenda Arusha jana ilipanda kutoka Sh22,000 hadi Sh35,000 wakati kutoka Dar es Salaam kwenda Kilimanjaro ilipanda kutoka 18,000 mpaka Sh30,000.

   Hali hiyo ilisababisha abiria wengi waliotaka kusafari kuelekea mikoa ya Kanda ya Kaskazini kuahirisha safari.

   Daladala zinazofanya safari kati ya Gongo la Mboto-Mwenge, Mwenge-Posta na Makumbusho-Bagamoyo zilionekana zikipakia abiria waliokuwa wakienda  mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.

   Abiria waliozungumza kituoni hapo, walieleza kwamba kutwa nzima ya jana, kulikuwa na tatizo la upungufu wa magari na kupanda ghafla kwa nauli ya mabasi yanayokwenda katika mikoa hiyo.

 


MISS TABATA  MATAMBO YANAENDELEA..!!
Warermbo wakiwa katika pozi wakisubiri siku ya mchuano
       Warembo wanaoshiriki shindano la Miss Tabata 2011 wakiwa katika picha za pamoja katika pozi tofauti wakati wa mazoezi yao katika Ukumbi wa Dar West Park Tabata jijini Dar es Salaam. Warembo hawa wanachuana kuwania taji linaloshikiliwa na Miss Tabata 2010 Consolatha Lukosi.


Toni Braxton Is Separated But In No Rush To Divorce


Well this makes for an interesting discussion…
      In her recent interview with Sister2Sister magazine, Braxton Family Values star Toni Braxton reveals details about her separation from husband Keri Lewis. Toni and Keri, who was once a member of R&B group Mint Condition, split in 2009, and this year marks the 10-year anniversary since they wed. She tells the magazine that the main reason she can’t see herself divorcing Keri is because she believes she’ll upset her children.
“We co-parent together. Sometimes he stays over with the kids; he’s very involved with his kids… April would have been 10 years (since we wed). We’re, like, the best of friends.
“We told the kids, ‘Sometimes mummy and daddy need a little break.’ That’s probably why I haven’t done a straight divorce yet.”


Lil B is Receiving Death Threats After Naming His Album “I’m Gay”


         It looks like Lil B the Based God is getting a lot of attention over the title of his new album, which he decided to title I’m Gay.  However, he may have gained some attention that he was quite expecting.
     After revealing the title of his upcoming project the California rapper has been receiving a series of death threats.  The threats mostly came via Twitter.  Peep what he had to say about the recent threats:
     People been hitting me up like, ‘I’m gonna bash your head in,’ ‘you f—-t,’ ‘I’m gonna kill you. I’m not gonna stop and I’m not scared of anybody on earth. That’s why I [titled the album I'm Gay] and nobody gonna stop me.



Picha ya mwanamke akigalagala baada ya kupata kichapo cha maana toka kwa mwanaume
      ANAKUFUMANIA: Analia, ananyamaza, anasononeka, unambembeleza anakuelewa
anakusamehe halafu anasahau!!!
      UNAZAA NJE YA NDOA: Anasononeka na kulia sana. Anakuchukia lakini baadaye
anakusamehe. Halafu analea mtoto uliyemzaa nje kwa upendo. Kama ni
kuchukiwa atachukiwa mtoto, si wewe uliyefanya umalaya!
     UNARUDI USIKU WA MANANE UKIWA MTUNGI: Anakukaribisha, anakuandalia
chakula, unagoma kula. Anahifadhi chakula alichokuandalia bila
manung'uniko.
    UNAAMKA ASUBUHI NA MAHANGOVER: Anakuandalia staftahi (saa nyingine unagoma
kutumia staftahi yake unakimbilia baa kwenda kunywa Supu na kuzimua. Wala
halalamiki!
     CHAKULA CHA USIKU: Ushapiga mtungi wako, unataka huduma. Unamrukia, hamna
maandalizi unamuumiza. Anavumilia ili akuridhishe. Na kesho yake tena
inaweza tokea hii; hana kinyongo!
     UNAJIANDAA KWENDA KIBARUANI: Unakuta kashakuandalia viwalo, suruwale
imenyooshwa kama ya askari trafiki, shati limepigwa pasi ya maana! Nguo
ulizovua jana zimeshalowekwa tayari kwa kufanyiwa usafi! Ulichomuudhi jana
kashasahau na kukusamehe!
    UNAMPA UJAUZITO: Anauthamini, anautunza anajifungua kwa uchungu, mtoto
anakuachia wewe umpe jina, la kwake halimo kabisa kwenye majina
atakayotumia mtoto! Na pamoja na uchungu wa kuzaa, bado yuko radhi
kukuzalia mtoto mwingine na mwingine tena!  





MISS DAR CITY CENTER WAJIMWAGA

Mratibu wa shindano hilo Fatma Abdalah ‘Fetty’(mbele), akiwa kwenye pozi la pamoja na washiriki hao.
   SHINDANO la kumasaka mrembo wa kitongoji cha Miss Dar City Centre 2011, linazidi kupamba moto kutokana na purukushani za mazoezi yanayoendelea katika kambi yao iliyopo Lamada Hotel Ilala jijini Dar es Salaam.

   Akizungumza na mtandao huu jana, mratibu wa shindano hilo, Fatma Abdalah ‘Fetty’, alisema kwamba kila kukicha anazidi kuridhizishwa na uwezo wa mazoezi ya warembo wake, na kwamba matumaini ya kutoa Miss Tanzania kwa kitongoji chake ni makubwa.




KUMBE AVRIL MSAGAJI..!!
      Pictures of Kenya's singer Avril surfaced on the internet last night.
The pictures show her in compromising positions with a female partner. 
    Avril, real name Judith Nyambura Mwangi, is signed to the Ogopa DJ stable
.
Avril2
avril











Avril3





 

 

 

 

 

 

 

Marekani kufanya mashambulizi Libya


Robert Gates
     Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Robert Gates amesema ndege za kivita zisizokuwa na rubani zinatekeleza mashambulizi ya anga nchini Libya.
     Gates amesema utumizi wa ndege hizo uliidhinishwa na rais Obama na kwamba zitaongeza uwezo wa wanajeshi wa muungano wa NATO katika harakati zao za kijeshi nchini humo.
Waasi nchini Libya, wamekuwa wakipambana na wanajeshi wa Kanali Gadaffi tangu mwezi Februri mwaka huu, lakini wameanza kupiga hatua ndogo.
     Katika kikao na waandishi wa habari mjini Washington, Gates amesema kwamba rais Obama aliidhinisha utumizi wa ndege hizo maalum zisizo na rubani kama mchango wao na pia kudhihirisha uwezo wao wa kijeshi.
Ndege za kivita za Marekani
Ndege za kivita za Marekani
     Amesema ndege mbili zitakua chini ya usimamizi wa NATO kwa saa 24 kila siku.
     Bwana Gates, amekanusha madai kuwa kutumwa kwa ndege hizo ni ishara ya Marekani ya kujiunga na Muungano wa NATO katika harakati zake za kijeshi nchini Libya, kwa njia ya siri.
     Ndege hizo maalum za kurusha makombora zinatumika kuwalenga wapiganaji wa waasi katika mipaka ya Pakistan na Afghanistan.
     Idara ya ulinzi ya Marekani imesema ndege hizo zitakuwa na uwezo wa kuwatambua wanajeshi wa Gadaffi ikiwa watajificha ndani ya magari ya kibinafsi au wakiingia kwenye maeneo ya makaazi ya watu.
     Ndege hizo zina uwezo wa kupaa muinuko wa chini kuliko ndege zingine za kivita na hivyo kuifanya bora katika juhudi za kijasusi na kufanya mashambulio, kwa kuwa ni vigumu kwa ndege hizo kuonekana kwenye mtambo wa rada.
     Wataalamu wanasema hii ni ishara tosha kuwa Marekani inajihusisha zaidi katika mzozo huo nchini Libya.



DIWANI WA CCM AKAMATWA KWA WIZI

          JESHI la Polisi mkoani Rukwa limemkamata na kumfikisha mahakamani aliyekuwa diwani wa viti maalumu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Sumbawanga, Bora
Mohamed (40) kwa tuhuma za kupatikana na  Kompyuta ya wizi.

          Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Isunto Mantage diwani huyo mkazi wa Kitongoji cha Majengo Manispaa ya Sumbawanga alikamatwa juzi saa 9:30 mchana akiwa katika kituo cha daladala ya Chanji akiwa na seti moja ya
kompyuta yenye thamani ya sh. 400,000 akiwa katika harakati za kuiuza.

          Akifafanua zaidi juu ya tukio hilo, Kamanda Mantage alisema kuwa mtuhumiwa alikuwa akienda kuiuza katika Kitongoji cha Kizwite kilichopo ndani ya manispaa hiyo.

          Baada ya kukamatwa na kuhojiwa, diwani huyo alisema kuwa
mali hiyo ni ya kwake lakini baada ya kufikishwa katika Kituo cha Polisi, kompyuta hiyo ilitambuliwa kuwa iliibwa kwa Mwalimu Mjwadu Babala wa Shule ya sekondari Mafulala baada ya nyumba yake iliyopo eneo la Bangwe kuvunjwa na watu wasiofahamika na kuiba vitu mbalimbali January 26, mwaka huu.

         Hata hivyo, Kamanda Mantage alisema kuwa katika tukio hilo mwalimu huyo alilipoti kuibiwa kwa vitu mbalimbali ikiwemo pikipiki pamoja na kompyuta baada ya kuipekua walibaini kuwepo kwa nyaraka mbalimbali zilizomhusu mwalimu huyo.




RAIA KICHAPO LIVE
        binadamu mwisho wetu ni pale tunapokumbwa na mauti na kuelekea kusiko julikana.. je unamuomba mungu kifo chako kiwe salama? ufe bila mateso?tazama binadamu tulivyo wanyama, mwizi kakuibia simu au elfu tano katika pochi yako unamtoa uhai wake kama vile wewe ndiye uliyemuumba..hivi kweli na wewe unatamani kufa kifo hiki? vyombo vya dola vimewekwa kwa ajili gani? unajua sababu iliyompelekea kuiba? tusikurupuke na kushiriki mauwaji ya wenzetu kwa Mungu tunatoa maelezo gani ya kujitosheleza kwa haya tunayoyatenda?


IMPRESS YOUR GIRL: Without Breaking the BANK!


     Are you sick of punishing your wallet just to have a good time with your girl?  Tired of trying to impress her with all the *air quotes* finer things in life.  Well STOP!  There are ways to wine and dine on a budget while and have a great time with your boo.  Read an after the jump!

Mother of Gay Bride Collapses


Mother collapsed after members of public showed her news article
The mother of a woman who had a same-sex marriage in Iowa, USA, has collapsed and is now hospitalized after members of the public showed her the article on one of Kenya's dailies.
The Daily Nation reported that Terry Wakonyo, 24, married Courtney Nicole, 25, in a civil union in Iowa, where it is legal.
TerryNicole
           Ms. Ng'endo, Terry's mother works at the Kenyatta University as a casual employee, working for the Vice Chancellor Olive Mugendi. Terry on the other hand, won herself a scholarship to a Kansas University a few years ago.
         Reports tell us that members of the public who work with Ng'endo callously showed her the article, with disregard to her feelings or state of mind, or to whether she knew that her daughter was openly gay. She then collapsed in the office and was rushed to the campus health unit. Her son, who also works at the university as an administrator, is with her now at the health unit.
         Members of the public have been seen taunting Terry's mother and neighbors, with jibes being thrown about them accompanying her to the USA to 'pay bride price' to Courtney's family.
This incident brings back memories of how journalists rushed to bombard the feeble and elderly parents of Kenyans Daniel Chege Gichia and Charles Ngengi, who wed a few years ago in the UK.
Daniel_and_Charles

Thursday, April 21, 2011

MUUAJI WA SOUTH BEACH AKAMATWA UWANJA WA NDEGE AKITOROKA

     Marehemu Lilah Hussen Alieungua vibaya mwili mzima akiwa ndani ya Gari la Kubebea Wagonjwa(Ambulance)ya hospitalki ya Kigamboni jijini Dar es Salaam Tayari KukimbizwaHospitali ya taifa ya muhimbili mara baada ya kuchomwa moto Lakini baada ya siku chache alipoteza maisha.

Mmiliki wa hoteli ya south beach ambae ni mtuhumiwa wa mauaji ya kijana mmoja mkazi wa mjimwema kigamboni jana amekatwa na jeshi la polisi uwanja wa dege akijaribu kutoroka.

  Habari za kiuchunguzi zinasema kuwa raia huyo mwenye asili ya kiasia alitoroka polisi kinyemela angali akiwa mtuhumiwa wa mauaji ya kinyama,aidha wakazi wa kigamboni wameingiwa na hasira zaidi baada ya kuona mtuhumiwa huyo anatumia uwezo wake wa kifedha kuwa huru.

   Hata hivyo ni hali ya hatari kwa eneo la hoteli ya south beach kwani wakazi wa maeneo hayo wanataka kuichoma hoteli hiyo ama ifungwe na kwa kudhihirisha hayo jamii ya watu wa kihindi wanaofika maeneo hayo husimamishwa katika magari na kupewa kichapo ikiwa ni hasira za raia baada ya mwenzao kuawa bila hatia.

   Habari zisizo rasmi zinasema hoteli hiyo inamilikiwa na mama mmoja ambae ni mke wa kigogo kinyume na jinsi inavyojulikana kwa sasa likuwa ya muhindi huyo.

 

 DR.SLAA AMULIKA ROSTAM AZIZ

          KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuchunguza mapato ya Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM), kwa kile alichodai yana uhusiano mkubwa na ufisadi.
         Dk. Slaa aliyasema hayo juzi jioni katika mkutano wake mjini Igunga, mkoani Tabora katika mwendelezo wa ziara zake.
        Alisema mapato ya Rostam kwa mwaka yanafikia sh bilioni 280, hivyo TAKUKURU haina budi kumkamata na kumchunguza kwani aliwahi kutangaza kuwa hana shida ya kuwa kiongozi au kung’ang’ania madaraka yoyote, kwani pesa alizonazo zinamtosha.
Kwa mujibu wa Dk. Slaa, ikiwa TAKUKURU haitamchukulia hatua Rostam, atawashawishi wananchi kutotoa ushirikiano wowote kwa taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na kuwazomea maofisa wake kila wanapowaona.
       Akifafanua tuhuma hizo za ufisadi, alisema kuwa kati ya makampuni 17 yanayosemekana kuwa ni ya Rostam hakuna jina lake hata moja.
       Alisema kama Rais Jakaya Kikwete angekuwa na nia ya kweli angemshirikisha kuwakamata mafisadi badala ya kuwapa siku 90 kuondoka ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
       Kwa mujibu wa Dk. Slaa, ikiwa Kikwete amewapa mafisadi hao siku hizo kuondoka ndani ya chama pamoja na kuachia ubunge, naye hana budi kujipa siku hizo, kwani naye ni fisadi.
       Alisema kujitokeza kwa mmiliki wa Dowans Brigedia Jenerali (mstaafu), Sulaiman Mohammed Yahya Al Adawi, ulikuwa ni usanii wa picha ya Rostam kwani baadaye ndiye atakayelipwa fedha hizo za Dowans.
Alisema CHADEMA haitakubali fedha hizo zilipwe na kwamba itaitisha maandamano nchi nzima kupinga.
       Dk. Slaa alisema ufisadi mwingine wa serikali katika sakata hilo la Dowans ni serikali kuweka mawakili watatu kinyemela na kupanga kuwalipa sh bilioni tano.
“Nilimtaja Rostam kuwa ni mmoja wa mafisadi kule Mwembeyanga, naye alinitumia vitisho kwa ujumbe mfupi kuwa nina sekunde chache za kuishi hivyo nipige magoti, nisali. Nilimjibu na nasema …nilizaliwa siku moja na nitakufa siku moja, sitaogopa kusema ukweli,” alisema Dk. Slaa.
      Katika hatua nyingine, Dk. Slaa alisema moto uliowashwa na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA) umeifanya serikali ya CCM akiwamo Rais Jakaya Kikwete kushindwa kulala.
      Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ikungi katika Jimbo la Singida Mashariki jana aliposimama kuwasalimia wakati akitokea Singida kuelekea Dar es Salaam, Dk. Slaa alisema Lissu ni mbunge jasiri katika Bunge ambaye amediriki kumnyooshea kidole hata Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema.
    

Real Madrid yashinda Copa Del Rey

    Real Madrid imeichapa Barcelona bao 1-0 na kunyakua kombe la kwanza katika msimu wa soka nchini Uhispania.
Ronaldo
Cristiano Ronaldo
     Bao pekee la Cristiano Ronaldo katika dakika za nyongeza ndio limeipa Real ushindi huo.
Real Madrid na Barcelona zitakutana tena mara mbili katika mchuano wa kuwania kucheza nusu fainali ya Klabu Bingwa Ulaya.




Earlier today we told you Rosa’s favorite positions and favorite time and place to get intimate, so if you meet these 3 requirements after the jump…maybe you should keep those other things in mind!! Hit the jump to find out if you qualify.
prv:
 she shared her favorite and least favorite sex positions. Wouldn’t you love to know what they are?! Hit the jump to find out, and see a couple pics of course.
prv :
she said My favorite time to get intimate is at night because it’s very romantic and I’m very passionate so I like the comfort of a bed.”




NYETI KULIKO NYETI TULIZONAZO
    Inasemakana ni bonge la soo ikiwa mke wako akiwa mjamzito kisha mkawa mnashea vyombo vyakuogea na baba mwenye nyumba,wachunguzi wa mabo wanadai mara nyingi wanawake wanaoshea vyombo vya kuogea na baba mwenye nyumba watoto wakizaliwa hufanana na baba mwenye nyumba hiyo,pengine ikwa sura,miguu,kifua ama kiungo chochote lazma kitawiana tu...hii ni sayansi jamii..



Snoop Dogg -- Is Today 4/20???

  In case you missed it -- today, 4/20, is an unofficial stoner holiday. 
  In fact,just spoke with Tommy Chong -- who told us he plans to celebrate by taking 420 hits from one of his favorite pipes at 4:20 PM. (Side note -- that can't be good for you.)
So, in summary, 4/20 seems like every other day for these guys.


Daladala yauwa wawili asubuhi hii


Thursday, April 21, 2011 11:32 AM
WATU wawili wamefariki dunia na wengine zaidi ya 21 kujeruhiwa katika ajali iliyotokea eneo la Kigogo jijini Dar es Salaam.
Basi aina ya Toyota DCM linalofanya safari zake kati ya Kigogo Mburahati na Kivukoni limepinduka lilipofika eneo la Kigogo Festini na kusababisha ajali hiyo.

Kufuatia ajali hiyo watu wawili wameweza kupoteza maisha papohapo na kupatikana majeruhi hao

 

Michael Owen ahuzunishwa baada kuzomewa na mashabiki

   Mshambuliaji wa Manchester United, Michael Owen amesema amehuzunishwa sana kutokana na kuzomewa na mashabiki wa Newcastle siku ya Jumanne, walipotoka sare ya 0-0 katika uwanja wa St James' Park.
    Owen mchezaji wa zamani wa Newcastle, alizomewa alipoingia katika dakika ya 81.
Owen amesema katika mtandao wa Twitter: "Kupata mapokezi mabaya ukiwa nje ya uwanja wa nyumbani inakera sana. Inakufanya ujitahidi ufunge bao!"
    Aliongeza: "Nilifahamu nitazomewa kama wanavyofanya mashabiki wengi, lakini iwapo wangefahamu ukweli basi wangekuwa na mawazo tofauti."
Owen alijiunga na Newcastle akitokea Real Madrid kwa kitita cha paundi milioni 16 mwaka 2005 na alifanikiwa kufunga mabao 30 katika mechi 79 alizoshiriki.
    Mshambuliji huyo wa England jitahada zake hazikuweza kufua dafu mwaka 2009 kuiokoa Newcastle isiteremke daraja na akaihama klabu hiyo na kujiunga na Manchester United akiwa mchezaji huru.
Baada ya mchezo wa siku ya Jumanne, Owen, mwenye umri wa miaka 31, alijibu mapigo ya kuzomewa na mashabiki wa Newcastle,    akisema: "Kwa kile ambacho nyinyi mashabiki wa Newcastle mnachokisema, mfurahi kwamba niliondoka katika klabu! Iwapo ningefahamu mapema, basi ningeondoka mapema zaidi!
   "Mkiangalia rekodi yangu, nilijitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu kuitumikia Newcastle. Chini ya KK (Akimaanisha Kevin Keegan) nilicheza vizuri sana na sitasahau mechi tuliyoshinda 2-1 dhidi ya Sunderland tarehe 20 mwezi wa Aprili 2008.
"Ninapokutana na mashabiki wa Newcastle au wa Liverpool wote wanaheshimu niliyofanya katika klabu zao. Uwanjani wanabadilika, mmoja anaanza kuzomea wengine wanafuata.
   "Hata hivyo siombi huruma. Mradi familia yangu hawanizomei ninapopita mlangoni, sijali kitu!!!"
    Owen alitazamia mapokezi ya kukera katika uwanja wa St James' Park, akasema kabla ya mchezo: "Ni siku nzuri, jua linawaka hapa Newcastle! Najiandaa kukutana na marafiki wangu wa zamani lakini mashabiki watanipokea kwa mtazamo mwengine!"
   Matokeo ya mechi hiyo yameifanya Manchester United kupoteza nafasi ya kuongeza wigo wa pointi katika msimamo wa ligi kileleni.



Rihanna Confesses That She Thought Russell Brand Was An Idiot The First Time They Met

      Though singer Rihanna seems to now have a pleasant relationship with her BFF Katy Perry’s British actor/comedian husband, Russell Brand, when she first met him she thought he was an “idiot” and didn’t think he was “funny.” She tells Australian’s Cleo Magazine:
“I first met him when he was interviewing me on TV. I was sick and it was the worst interview I’ve ever done. I was throwing up in a bucket and a doctor gave me a shot in my butt. Nothing was funny to me. I thought it was the most stupid f***ing interview I ever did in my f***ing life.[...]Why am I talking to this idiot? He made me want to throw up again.”
We did another interview on MTV and I realised he was funny. I was probably a complete bitch, but only months afterwards did I get it.”
Last year, Rihanna confessed that she felt bad about missing Katy Perry’s and Russell’s wedding in india. She revealed in an interview.
“I will never ever forgive myself for that, it was a crazy time, it was a crazy week, I’m switching management. There was no phone service in India and very little-to-no internet service, so it would have been a little irresponsible of me. I’m sad that I missed it.”



KANUMBA Vs SYLVIA SHALLY TAMU YAGEUKA CHUNGU 

   Kwa mujibu wa chanzo hicho, kabla ya tukio hilo, wawili hao     walitibuana kufuatia kutoelewana kwa suala la kimapenzi ambalo halijawekwa wazi.
“Unajua   kabla Kanumba hajamtumia demu wake meseji hiyo, walianza kupishana lugha kwenye uhusiano wao, ndiyo jamaa akaja juu,” kilisema chanzo.

    Kikaendelea kudai kuwa, baada ya Sylvia kulifikisha suala hilo polisi, Kanumba aliitwa na ‘kusomewa’ shitaka lake lakini hakuonesha kukiri wala kukataa.

     Inadaiwa kuwa, afande anayepeleleza kesi hiyo (jina tunalo) aliwataka wawili hao wakakae chini na kuondoa tofauti zao kisha warudishe majibu Jumatatu ya Aprili 18, mwaka huu.

     Hata hivyo, chanzo kinasema, mpaka siku inakatika Jumatatu, wawili hao hawakurudi kituoni hapo kuelezea walikofikia baada ya ushauri wa afande. 
Baada ya madai hayo, Jumanne ya Aprili 19, mwaka huu, mwandishi wetu aliamua kuwasaka wapenzi hao kwa njia ya simu zao za mikononi ili kuupata ukweli.

    Saa nne asubuhi, Kanumba ndiye aliyekuwa wa kwanza kupigiwa simu ambapo iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.

    Alipogeukiwa Sylvia, naye simu yake ya kiganjani iliita kwa kitambo bila majibu.
Hata hivyo, paparazi wetu aliendelea kufanya jitihada za kuwapigia simu mara kwa mara lakini hakuna aliyepokea.

    Ilipofika saa nane mchana, kila mmoja kwa wakati wake, walipigiwa tena simu na hakuna aliyeipeleka sikioni kutaka kujua kulikoni.

    Saa tisa alasiri, mwandishi wetu aliamua kumtumia ujumbe mfupi (sms) Kanumba akimtaka apokee simu huku akijtambulisha kwa majina yote na anakofanyia kazi.

    Baada ya hapo, simu hiyo ilipigwa tena, ikapokelewa na mtu aliyejitambulisha kwa jina la Kiuno ambaye alidai mwenye simu (Kanumba) alikuwa ‘shuting’.
Aliombwa amwambie kuna ishu muhimu inamtaka mwenyewe, Kiuno akasema atafanya hivyo muda si mrefu huku akimtaka mwandishi apige baada ya dakika tano.

    Kama vile haitoshi, mwandishi kabla ya kupiga tena, alimtumia Kanumba ujumbe mfupi akimwelezea ‘shitaka’ lililo mezani kwake.

    Baada ya meseji hiyo kuonesha imefika, mwandishi alitwanga simu, ikapokelewa na Kiuno yule yule ambapo alisema:
“Jamaa sijamwambia bwana. Lakini pia nimeona meseji, nikampelekea simu, alipoisoma akasema ‘si kweli.’

    Baada ya kugonga mwamba kwa Kanumba, mwandishi alimtumia meseji Sylvia, akajaribu kumwelezea kisa kamili kutoka kwa chanzo chetu makini, lakini mrembo huyo hakujibu meseji wala kupiga simu achilia mbali ‘kubipu’.
 Hivi karibuni, mmoja wa marafiki wa Sylvia alikaririwa akisema kuwa, mapenzi kati ya wawili hao yameingia nyongo.

    Rafiki huyo (jina tunalo) alisema kuwa, Kanumba ni kama amemtosa Sylvia kwani hana ukaribu naye tena kama zamani,  jambo ambalo linamkosesha raha mrembo huyo.
“Yaani naweza kusema kuwa, Sylvia anajua penzi la Kanumba kwake halipo, anasema ule ukaribu kama zamani hakuna tena, anakosa raha kabisa,” alisema rafiki huyo.   

Beyonce And Jay-Z Spotted Dining With Julez & Solange Ex-Husband in Paris

    Earlier today, Beyonce and Jay-Z were spotted leaving Le Meurice Hotel where they have been staying over the last few days. They then headed over to L’Avenue restaurant where they were spotted toasting to the good life while dining with Julez and Solange ex-husband Daniel Smith Sr.
            vinywaji vya kufa mtu

More photos and braabraaaa...




Beyonce would make such a cute mommy!



GAME AZUIWA KUINGIA CANADA

JAYCEON TERRELL TAYLOR AKA GAME

Jayceon Terrell Taylor aka Rapper The Game amepata matatizo nchini Canada,coz kwa nza alikataliwa kuingia nchini humo,lakini baadaye alizuiliwa kwa wiki 2
Game aliwaomba radhi fans wake wa Canada na kufunguka kuwa aliiingizwa mkenge na promoters waliomuambia kuwa angeingia bila matatizo,kusababisha issue yake isikilizwe na judge,ambaye ataamua kama afukuzwe au ashitakiwe kwa kuvunja sheria za uhamiaji za nchini Canada
Mwisho wa siku Game aliachiwa na kurudi Los Angeles na kutupia kwenye Tweeter “najisikia vibaya kupanda ndege toka Los Angeles mpaka Canada kwa ajili ya kuzuiliwa kwa wiki 2,ila anashukuru pia kukusanya kila kilicho chake na kurudi salama”