Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Monday, April 23, 2012

CHEKA NA MAUGO KUFIA ULINGONI KWAAJILI YA GARI

 


Mwisho wa pambano la ubingwa wa IBF kati ya Francis Cheka na Mada Maugo leo wameonesha rasmi gari watakalogombania  Mabondia Mada Maugo Na Francis Cheka  Aprili 28 mwaka huu katika ukumbi wa PTA, Dar es Salaam.

Pambano hilo linatarajiwa kuwa katika uzito wa kg 75 la raundi 12 la Kimataifa ambapo linatarajiwa kuwa chini ya Kamisheni ya Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) huku majaji wa pambano hilo wakitegemewa kutoka nje ya nchi.
Akizungumza Dar es Salaam leo, Msemaji wa mpambano huo Yasini Abdallah alisema kuanikwa kwa mkanda huo na Gari kuwekwa Hadharani kutaashiria kupamba moto kwa pambano hilo ambalo linatarajia kuwa katika ngazi ya Kimataifa ili kuweza kupatikana kwa mshindi wa halali na pia itafuta hisia za kuwepo na ubabaishaji katika pambano hilo.

“Tunauanika Gari na mkanda ili kuwathibitishia wadau wa ngumi na mashabiki kwa ujumla kuwa tupo makini na pambano hili na sio la kibabaishaji na kama tulivyosema awali kuwa majaji watoka nje ya nchi na hiyo yote ni kutaka mchezo uchezeshwe kulingana na hadhi ya mkanda,” alisema Kaike.
Alisema, maandalizi kwa ujumla ya pambano hilo yanaendelea vizuri na zawadi ya gari kwa mshindi iko pale pale ambapo mshindi atakabidhiwa siku hio hio ya pambano baada a kutangazwa mshindi na kupewa mkanda itafuatiwa na zawadi hiyo ya gari.
Awali mabondia hao walishakutana mara mbili ulingoni ambapo katika pambano la kwanza lilofanika PTA Cheka alishinda kwa pointi ambapo Maugo hakukubali matokeo hao na kuandaliwa pambano la marudiano lilofanyika Uwanja wa Jamuhuri Morogoro ambapo Cheka aliibuka mshindi tena kwa kumtwanga kwa pointi.
Baada ya kumalizika kwa pambano hilo kila bondia aligoma kucheza na mwenzake tena lakini baada ya kuandaliwa pambano hilo la ubingwa kila mmoja alibadilisha nia na kuamua kurudi ulingoni kuwania mkanda huo.
Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano la Cheka na Maugo ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D
.

UJUMBE MAHUSUSI KATIKA VIKARAGOSI

Friday, April 20, 2012

MWANAMKE MWINGINE ALIEZAA NA KANUMBA AJITOKEZA

SALMA Hamidu, mkazi wa Igogo, jijini Mwanza ameibuka na kudai amezaa na marehemu Steven Kanumba mtoto wa kike aitwaye Treasure Steven Charles Kanumba (2), Ijumaa linashuka na maneno ya kinywa chake.
Akizungumza na mwandishi wetu, Salma anayefanya kazi kwenye Ofisi ya Uwakili ya Law Consultancy jijini Mwanza, alidai alianza kufahamiana na marehemu mwaka 2006 wakati yeye akiwa kwenye Kundi la Nyakato Arts chini ya Mwalimu Joseph.
Salma akasema kuwa, uhusiano wao uliunganishwa na Mwalimu Joseph ambaye alimpa marehemu namba zake za simu wakati alipopeleka filamu za Machozi Yangu na Siri Yangu kuifanyia uhariri (editing) jijini Dar es Salaam katika studio alizokuwa akifanyia kazi marehemu.
 

SAKATA LA WABUNGE KUMVUA MADARAKA WAZIRI MKUU(Mh.PINDA)

Deo Filikunjombe:- Ameliambia bunge kuwa Waziri wa Fedha Mkulo sio muaminifu anaitafuna nchi. Wabunge hawana imani na baadhi ya mawaziri wetu.
Awali alisema wengi wa mawaziri ni wezi na ushahidi anao atautoa ameongeza kuwa anashangazwa kwamba tangu jana hadi leo hakuna hata Waziri mmoja aliye jiuzuru na hii ni kutokana na malalamiko ya wabunge kuhusiana na kutokuwepo kwa usimamizi kutokuwepo kwa uwajibikaji mali za wananchi mali za umma zinapotea.
Vicent Nyerere:- Anashangazwa kwamba magari yananunuliwa na kufanyiwa ukaguzi kwa makampuni feki yanayotajwa kuwa ofisi zake ziko nje, kwa hali hii mawaziri wanaruka sarakasi na taulo watabaki uchi.

Baada ya hapo wakafuata Wenyeviti wa KamatiJohn Cheyo:- Alichoguswa zaidi ni kwa jinsi gani wabunge wameungana pamoja bila kujali itikadi zao katika kusimamia matumizi ya pesa za serikali nakuhakikisha kuwa fedha hazipotei kama ilivyo sasa.Agustino Mrema:- Kuna haja sasa kuhakikisha kwamba kesi hizi zinazo husiana na watu waliotumia vibaya madaraka yao kwa kutafuna fedha za wananchi zinaharakishwa badala ya kusikilizwa kwa muda mrefu kama ilivyo hivi sasa.

Msumari wa Mwisho:
Zitto Kabwe:- Yeye akasema huko huko TBS kumekuwa na matatizo mengi lakini bado viongozi wake wamekuwa kimya kunakosekana uwajibikaji akagusia kwamba kama kuna marekebisho mapya yanayopaswa kuwekwa katika katiba hii mpya ni uwajibikaji kwa wale ambao wamefanya vibaya, ambao wamelitia hasara taifa waweze kuwajibika kwa hili sasa akasema wao kama wabunge kuanzia kesho watakusanya saini 70 za wabunge watakaounga mkono hoja itakayoletwa Bungeni ya bunge kutokuwa na imani kwa Waziri mkuu ili jumatatu iwasilishwe. Lengo ni kukomesha ubadhirifu na wizi unaopewa baraka na mawaziri.

Thursday, April 19, 2012

NAVIO ASHINDA TUZO YA MWANAMUZIKI BORA AFRIKA MASHARIKI

Ugandan hip hop star Navio won the Best East African Artist award at the Asia – Africa Entertainment Awards 2012.
The awards ceremony was held in Eastlin hotel in Malaysia last weekend 14th April, 2012. Navio battled it up with other African high ranking artists such as D’Banji from Nigeria whom he also battled with in last year’s Channel O Music video Awards 2011 among other African stars. Navio emerged out the overall winner for Best East African Artist 2012.
At the channel O awards last year, Navio, Goodlyfe and Keko were nominated. Navio emerged most nominated Artists overall with nominations for Most Gifted Hip Hop Video Artist, Most Gifted Male Video Artist and Most Gifted Video of the Year Artist.
Since the start of this year, Navio has been doing well at the prestigious HiPipo Charts, making impressive appearances with at least one of his acts in the top 20 every week. The acts include Hot Temper Featuring Golola Moses and Dream featuring Jose Chameleone. He has appeared on HiPipo charts consecutively since the beginning of this year.
At the end of last year, Navio took home for the second time running the PAM awards Hip Hop artist of the year accolade.

AIRTEL YATOA COMPUTER NA VITABU YENYE THAMANI YA 25ML UDOM

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akikabidhi baadhi ya
vitabu  vya chuo kikuu vilizotolewa na Airtel kwa chuo kukuu cha Dodoma
(UDOM) kwa Makamu Mkuu wa chuo hicho Profesa Idrisa Kikula (kulia) jana
wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika chuoni hapo.  anaeshuhudia
ni Mkuu wa wilaya ya Bhahi Bi Betty Mkwasa (kati). Airtel imetoa vitabu 104
na computer 20 vyote vyenye  thamani ya milioni 25/- TZS ikiwa ni
muendelezo wa Airtel katika kuchangia sekta ya Elimu nchini.
Mkuu wa wilaya ya Bhahi Mheshimiwa Betty Mkwasa akiongea na waandishi wa
habari na baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho jana wakati wa hafla fupi ya
makabidhiano ya vitabu 104 na kompyuta 20 vyote vyenye  thamani ya milioni
25/- TZS  toka Airtel ikiwa ni muendelezo wa Airtel kuchangia sekta ya
Elimu nchini. Anaefuata ni Makamu mkuu wa chuo hicho profesa idrisa Kikula
na Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando.

IDDI AZAN AMUUMBUA NAIBU WAZIRI WA MICHEZO

MBUNGE wa Kinondoni, Iddi Azan, (CCM), amemuumbua Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, kutokana na kutoa taarifa za kupotosha bungeni kuhusu timu zilizoshinda katika Kombe la Chalenji na Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati.
Akitoa taarifa bungeni jana, mbunge huyo alisema, si kweli kwamba timu ya taifa, ilitwaa kombe hilo mara tano na timu za Simba na Yanga, zilishinda Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati mara moja kwa kila timu.
Azan alisema usahihi ni kwamba, Simba ilishinda kombe hilo mara sita na Yanga mara tano, huku timu ya taifa ilishinda mara tatu Kombe la Chalenji, mwaka 1974, 1994 na mwaka 2011.
“Nimesikitishwa na majibu yaliyotolewa na serikali kuhusu matokeo ya michuano hiyo. Naomba kutoa taarifa Naibu Spika,” alisema Azan.
Katika swali la msingi la Mbunge wa Ziwani, Ahmed Ngwali, aliyetaka kujua ni mafanikio gani ya msingi na ya kujivunia yaliyopatikana kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), mpaka sasa.
Akijibu swali hilo, naibu waziri huyo alisema kwa jumla shirikisho hilo limefanikiwa kukuza na kuendeleza mpira wa miguu kila kona ya nchi na kuweka muundo wa utawala katika kila ngazi, kuandaa wataalamu wa fani za ufundishaji, uamuzi, utawala na tiba kwa wanamichezo zaidi ya 10,000 na kuongeza kuwa, wataalamu hao wamepata mafunzo hayo tangu nchi ilipopata Uhuru.
“Shirikisho pia limefanikiwa kuandaa na kuendesha programu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mashindano ya timu za vijana, wanawake na watoto kama sehemu ya kuweka msingi bora wa maendeleo ya mchezo wa soka,” alisema.
Pia alisema timu ya taifa ilifanikiwa kucheza mara moja fainali za Kombe la Afrika na mara moja kwa timu za taifa za wachezaji wa ligi za ndani, (CHAN), pamoja na kujenga na kuimarisha uhusiano mwema kati ya shirikisho na serikali. 

ZITTO KABWE AZILIPUA TANESCO NA ATCL


Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), imependekeza kwa serikali iwakamate na kuwafikisha mahakamani maofisa wa serikali walioingia mkataba wa ukodishaji wa ndege ya ATCL, Air Bus 420-214, mwaka 2007.

Hali kadhalika, kamati hiyo imelishutumu Shirika la Umeme nchini (Tenesco), kwa kufanya manunuzi ya Sh. bilioni 600 bila kufuata sheria za manunuzi.

Hayo yalisemwa bungeni jana na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Zitto Kabwe, wakati akiwasilisha taarifa yake, kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2010.

Zitto alisema fedha hizo ni nyingi hivyo ni muhimu msisitizo na hatua za kisheria zitaendelea kuchukuliwa kwa taasisi zote ambazo zinakiuka sheria za manunuzi ya umma  kuisababishia serikali hasara kubwa.

Tuesday, April 17, 2012

MAMA YAKE SUMA LEE AFARIKI KWA KIHARUSI

Habari zilizotufikia hivi punde chumba cha habari ni kwamba mama mzazi wa msanii wa kizazi kipya Suma lee amefariki dunia kwa ugonjwa wa kiharusi katika hospitali ya muhimbili jijini Dar.
Suma Lee anaetamba na kibao cha "hakunaga" yuko katika hali ya majonzi mazito ya kuondokewa na mpendwa wake,tunampa pole sana mwenzetu katika burudani.

MISS UKONGA 2012 YAPAMBA MOTO



 

warembo wanaowania taji la Miss Ukonga 2012, wakiwa katika picha ya pamoja katika kambi yao ya mazoezi Iliyopo Banana jijini Dar es Salaam. Kitongoji cha Ukonga ndio kitafungua pazia la Mashindano ya Miss Tanzania mwaka huu.
Washiriki wa shindano la Miss Ukonga wakimsikiliza mkufunzi wao Jaquline Chuwa akiwapa nasaha za namna ya kufanya.
Warembo wakifanya mazoezi ya kucheza mziki wa ufunguzi wa show yao. hakika warembo hawa ni wajuzi.
Baadhi ya warembo wakimwangalia mwezao aliyekuwa akifanya mazoezi ya kutembea.

TBL YATOA SH. MIL. 100 UJENZI WA CHUO KIKUU TUMAINI

    

Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kushoto),akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu Huduma za Jamii wa
 Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Robert Charles (kulia) mfano wahundi yenye thamani ya sh. mil. 100 za kusaidia
ujenzi wa majengo mapya ya Chuo Kikuu cha Tumaini, Dar es Salaam. Anayeshuhudia
makabidhiano hayo yaliyofanyika, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, ni Mkuu wa chuo hicho kamapasi ya Dar es Salaam, Profesa Geofrey Mmari
.

POLISI WAFANYA MSAKO WA PIKIPIKI ZINAZOTUMIKA KWA UJAMBAZI

Maaskari wa jeshi la Usalama wa Raia wakiwa wamekamata pikipiki Mataa wa Agrey kwa ajili ya

kuwafikisha kituo cha polisi msimbazi. Dar es salaam leo Jeshi hilo linafanya Operesheni
ya kukamata pikipiki hizo kutokana na kuhusishwa na matukio ya hualifu ukiwemo ujambazi wa
kutumia pikipiki
Maaskari wa jeshi la Usalama wa Raia wakiwa wamekamata pikipiki Mataa wa Agrey kwa ajili ya
kuwafikisha kituo cha polisi msimbazi. Dar es salaam leo Jeshi hilo linafanya Operesheni
ya kukamata pikipiki hizo kutokana na kuhusishwa na matukio ya hualifu ukiwemo ujambazi wa
kutumia pikipiki

MAKAMU WA RAIS (TANZANIA) DK GHARIB BILAL ASAINI KITABU CHA KUMBUKUMBU CHA KIFO CHA ALIYEKUWA RAIS WA MALAWI, DKT. BINGU WA MUTHARIKA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha maomboleo ya aliyekuwa Rais wa Malawi, Dkt. Bingu wa Mutharika, katika Ofisi za Ubalozi wa Malawi nchini, zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam leo, Aprili 17, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha maomboleo ya aliyekuwa Rais wa Malawi, Dkt. Bingu wa Mutharika, katika Ofisi za Ubalozi wa Malawi nchini, zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam leo, Aprili 17, 2012. Kulia ni Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Flossie Asekanao Gomile-Chidyaonga. Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu Wa Rais.

Monday, April 16, 2012

RAMBIRAMBI ZA MSIBA WA KANUMBA ZACHACHULIWA WENGI WANEEMEKA NA KIFO CHAKE

UONGOZI wa Bongo Movie uliohusika na uratibu wa shughuli za mazishi ikiwemo michango katika msiba wa msanii Steven Kanumba, umeingia kwenye kashfa nzito.
Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika kutoka ndani ya familia ya Kanumba, kamati hiyo imedaiwa kufanya uchakachuaji wa michango hiyo inayokadiriwa kuwa mamilioni ya fedha, achilia mbali
vitu kadhaa, yakiwemo magunia 32 ya mchele.
Chanzo hicho kimeidokeza blog hii kuwa, dalili za hali hiyo zilianza kujitokeza mapema kabisa pale mwanandugu mmoja alipoenguliwa kwenye kamati hiyo, kwa kile kinachoelezwa, kamati hiyo kufanya jukumu hilo kwa uhuru zaidi.
Dalili nyingine, ni kitendo cha wajumbe wa Kamati hiyo kutoweka baada ya mazishi hadi walipofika nyumbani kwa marehemu Alhamisi usiku.
Kwamba, pamoja na mambo mengine, kwenye kikao kilichofanyika siku hiyo kati
ya wanandugu na kamati hiyo, Mama Kanumba amezuia kuzungumzia suala la michango.
 “Mama Kanumba ametakiwa asiseme lolote kwa Waandishi wa Habari kuhusu michango… kaelezwa kama atafanya hivyo, huenda asipate kitu kabisa,” alisema ndugu huyo. 
Kwa mujibu wa chanzo hicho, Kamati hiyo imetoa onyo hilo kwa vile tangu kwisha kwa maziko ya Kanumba, wamekuwa wakipata usumbufu wa simu watu kuulizia kilichokusanywa na kilichobaki.
Chanzo hicho kimedokeza kuwa, baada ya kamati hiyo kukutana na wanafamilia kwa mara ya kwanza baada ya ukimya mrefu, ilisema michango yote ni sh mil 51.
Kati ya fedha hizo, gharama za mazishi ni shilingi mil 48 huku kukiwa na deni la sh
mil 2 za ukarabati wa barabara Leaders kutokana na uharibifu uliofanywa na waombolezaji.
Chanzo hicho kimedokeza kuwa, walipohoji fedha zilizochangwa kupitia M-pesa kupitia namba ambayo ilitangazwa, walielezwa ilipatikana sh 20,000 tu.
Kilisema, kiasi hicho ni kiduchu mno kwa sababu mashabiki wa Kanumba wa Mwanza pekee, walichanga sh 300,000.
Kilidokeza kuwa, pia kulikuwa na gunia 32 za mchele zilitotolewa na msamaria, hazijulikani zilipokwenda.
“Licha ya kutolewa gunia 32 za mchele, hazijulikani zipo wapi…. fikiria hata mfiwa, anakosa hata gunia moja la kwenda kuanzia maisha mapya bila mwanaye,” kilidokeza chanzo hicho.  
Kilipoulizwa kwanini hawakuweka ndugu kwenye kamati hiyo tangu mapema, kilisema alikuwemo, lakini akaenguliwakwa kwa zengwe.
Uratibu wa msiba huo ulikuwa chini ya Kamati iliyokuwa chini ya Gabriel Mtitu na wajumbe kama Ray, Cloud, Steve Nyerere, Hapines Magese, Mtitu William, Jacob Steven na wengineo.
Sayari ilipomtafuta Mtitu kwa njia ya simu jana, alisema kutokana na usumbufu ambao wanaupata kwa wengi kutaka kujua juu ya michango hiyo ya msiba, Kamati yake imeamua kukutana na waandishi wa Habari kesho Jumanne kuweka kila kitu bayana.
“Kuna mengi yanasema hadharani na chini ya zuria kuhusu rambirambi, kwa lengo la kuweka bayana kila kitu, tumepanga kukutana na waandishi wa Habari Jumanne (kesho) kuanzia majira ya saa nne,” alisema

KEKO KUMSHITAKI GENEXT

 Keko under her new management supanova music group is suing Genext for unauthorized use of her image in their recent social media campaigns. This came after the artist was contacted by one of the representatives at Blu Flamingo, the company charged to manage Genext’s twitter and facebook campaigns last December to make a jingle for Genext’s campaigns which was never used. 
  Besides making the jingle, the “Make you dance” artist was also asked to attend a photo shoot after which her image was run in various media houses without her consent. This has however forced her new record label take matters to another level after Blu flamingo under Genext totally refused to pay the artist even after claiming to the press that they had given her 60 million shillings for the campaign.
 “The matter is ongoing” was the only comment we could get from Just Jose who’s apparently one of the CEO’s at Supanova music group. Meanwhile, Keko’s management has changed the date of her “Kekonian” album launch from May 4th to the 27th of this respective month and kyadondo rugby grounds will be the main venue with Nigerian RnB singer Tiwa Savage of “Kele kele love” alongside Kenya’s Madtraxx supporting the Hip Hop maestro.

MELI YA TAWALIQ ILIVYOZAMA KATIKA MAJI

 
ILE meli maarufu kama Meli ya Magufuli ambayo Serikali ya Tanzania iiliansa katika Eneo lake la bnahari ya hindio ikivua samaki bila ya Kibali imenza kuzama baharini na imeharibika vibaya.

Inaelezwa kuwa Meli hiyo ya Twaliq 1 Machi 8, 2009 wakiwa samaki tani 293 aina ya Jodari ikivua samaki kwenye Ukanda wa Kiuchumi wa Tanzania (EEZ), bila kuwa na kibali

Meli ya Tawaliq 1 ilikamatwa ikiwa na wavuvi 34 na hadi kufikia tamati ya Kesi hiyo jumla ya wavuvi 20 walitiwa hatiani.

Lakini licha ya Mahakama kuamuru meli hiyo itaifishwe kwa sababu ilikuwa haijulikani na Tume inayojihusisha na shughuli za uvuvi katika Bahari ya India (IOCT) lakini meli hiyo imeanza kuzama kama inavuyoonekana pichani.

Kuzama kwa meli hiyo ni kutokana na kutoboka baadhi ya maeneo hivyo kuingiza maji ndani na kuzama.

Sunday, April 15, 2012

MISS UTALII KINONDONI 2012 KUFANYIKA SUNCIRO

Shindano la kumpata Binti wa Utalii Kinondoni 2011/2012(Miss Utalii Kinondoni 2011/2012 ngazi ya wilaya limepangwa kufanyika katika ukumbi wa kisasa na Club ya kimataifa ya Sinsiro,iliyoko Shekilango Sinza.Shindano hilo limepangwa kufanyika siku ya Ijumaa tarehe 25 Mei 2012 na kushirikisha mabinti 25 kutoka katika majimbo yote ya wilaya ya Kinondoni.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na mkurugenzi wa Miss Tourism Tanzania Organisation wilaya ya Kinondoni Pius Yalula,ambao ndio waratibu na waandaaji wa shindano hilo, washiriki wote wanatarajia kuanza kambi ya mazoezi katika ukumbi huo siku ya Jumatatu Mei 1,2012. Miss Utalii Kinondoni 2010/2011 Sophia Dioa ambaye pia ni Miss Utalii Dar es Salaam 2010/2011 na Miss Utalii Tanzania 2010/2011.

Piusi Yalula alibainisha kuwa ni mpango mkakati wa Miss Tourism Tanzania organisation mwaka huu, wa kuwafuata watanzania hususani vijana katika maeneo yao ya burudani,ili kuwahamasisha juu ya utalii wa ndani. 
Ndio maana fainali za mwaka za Miss Utalii Kinondoni ,tumeamua kuzifanyia katika Club ya Sunciro, ambako tunaamini kuwa vijana na watu wa rika mbalimbali wanapenda kwenda katika kumbi na club za aina hiyo kwa ajili ya burudani na mapumziko ya wikendi.

ANGELA MARTINI MWANAMKE MWENYE MVUTO ZAIDI JIJI LA NEW YORK

 Angela Martini

According to Blottr News, Angela Martini is the hottest woman in New York City!
The gorgeous Albanian model arrived at the Christie’s Bid to Save The Earth Event last night just to show off why she received such a prestigious honor.
Angela stepped out in an effortlessly stylish black and beige belted dress ensemble for the event. She paired the lock with uber glamorous flowing curls and simple jewelry. All eyes were on the model as she walked the red carpet in ACL and Stella McCartney.
On being named the hottest woman Angela said,
It's a pleasant surprise. It's always flattering to be seen that way, it's very sweet but I take it with a grain of salt.
Angela finished sixth in the 2010 Miss Universe pageant and currently holds the title as the highest-placed Miss Universe Albania contestant in history. We have a strange feeling we will be seeing a lot more of Ms. Martini - after all, she's NYC's most coveted asset. 

J-LO AMRUSHA ROHO CASPER KIDEONI

Jennifer Lopez heats up the screen with her boy toy Casper Smart in the video for her latest single “Dance Again,” featuring Pitbull.

WANAMUZIKI WALIVYONG’AA TUZO ZA MUZIKI KILI MUSIC AWARDS 2012.




















HAWA NDO WASHINDI WA KILI MUSIC AWARDS 2012.

1. WIMBO BORA WA RAGGAE.
-ARUSHA GOLD BY WARRIORS FROM EAST.

2. WIMBO BORA WA DANCE HALL.
- MANENO MANENO BY QUEEN DARLIN.

3. WIMBO BORA WA ZOUK RHUMBA.
- DUSHELELE BY ALI KIBA.

4.BORA WENYE VIONJO VYA KIASILI.
- VIFUU UTUNDU BY A.T-

5. WIMBO BORA WA TAARABU.
- NANI KAMA MAMA BY MASHAUZI CLASSIC ( AISHA MASHAUZI).

6. WIMBO BORA WA KISWAHILI.
- DUNIA DARAJA BY TWANGA PEPETA-

7. WIMBO BORA WA AFRO POP.
- HAKUNAGA BY SUMA LEE-

8. WIMBO BORA WA R&B.
- NUMBER ONE FAN BY BEN PAUL-

9. WIMBO BORA WA HIP HOP.
- MATHEMATICS BY ROMA-

10. MSANII BORA ANAECHIPUKIA.
- OMMY DIMPOZ (NAI NAI SINGER).

11. RAPA BORA WA BAND.
- KALIJO KITOKOLOLO-

12. MSANII BORA WA HIP HOP.
- ROMA MKATOLIKI-

13. WIMBO BORA WA KUSHIRIKISHWA.
 - NAI NAI BY OMMY DIMPOZ FT. ALI KIBA-

14. WIMBO BORA WA AFRIKA MASHARIKI.
-KIGEUGEU BY JAGUAR-

15. MTUMBWIZAJI BORA WA KIKE.
- KHADIJA KOPA-

17. MTUNZI BORA WA MWAKA.
    - DIAMOND-

16. MTUMBWIZAJI BORA WA KIUME
- DIAMOND-

18. MTAYARISHAJI BORA WA MAPIGO YA MUZIKI.
- MANEKE-

19. VIDEO BORA YA MWAKA.
- MAWAZO BY DIAMOND-

20. WIMBO BORA WA MWAKA.
- HAKUNAGA BY SUMA LEE-

21. HALL OF FAME.
     -  TAASISI JKT-

22. HALL OF FAME KWA MTU BINAFSI.
      - KING KIKII-

23. HALL OF FAME KWA MTU BINAFSI.
     - DR. REMMY ONGALA-

24. MWIMBAJI BORA WA KIKE.
     - LADY JAY DEE-

25. MWIMBAJI BORA WA KIUME.
      - BARNABA-