Mshindi
wa Miss Lake Zone Inter-College 2012 ni Migeshi john na wapili(kushoto)Josephin Winfred(kushoto)ambae ni
mshindi wa pili na mshindi wa tatu Enfilda Clemence (kulia).
Top 5 katika picha ya pamoja mara tu baada ya Josephin kutangazwa mshindi.
Josephine katika kivazi la ufukweni.
Pages
BRAND NEW MUSIC
metty magese
Listen & Download
http://mdundo.com/a/32626
Sunday, June 24, 2012
MISS TOURISM KUJA KIVINGINE MWAKA HUU
HILDA EDWARD AWA MISS DAR INTER COLLEGE 2012
![]() |
Hilda akipigana busu moto moto la pongezi na Miss Dar Inter College aliyevua taji Blessing Ngowi
|
![]() |
| TOP 5; Kutoka kulia Veronica Yole, Sada Suleiman, Rose Muchunguzi, Jamila Hassan na Hilda Edward |
![]() |
| DIAMOND PLATINUM; Nassib Abdul akitumbuiza kwa hisia, kibao Wema Wangu mbele ya jaji Wema Sepetu, ilikuwa tamuuu |
Wednesday, June 20, 2012
AZAM MARINE KUMALIZA TATIZO ZANZIBAR
a
Meli hiyo inavyoonekana kwa Nje

Meli hiyo inavyoonekana kwa ndani.

Meli hiyo inavyoonekana kwa Ujumla
Azam
yaamua kufanya kweli na hivi karibuni meli ya kisasa iko mbioni
kuzinduliwa ambayo ikawezesha watu kwenda na magari yao Zanzibar. Meli
hiyo inauwezo kubeba magari 200, abiria 1500 na Mizigo tani 500.KAMPUNI
ya Usafiri wa baharini ya Azam Marine inatarajia kuzindua meli kubwa
ya kisasa kwaajili ya abiria waendao Dar es Salaam, Pemba na Unguja.
Meneja Mkuu wa kampuni hiyo Hussein Mohamed Said, amesema Julai 15 mwaka
huu meli hiyo yenye urefu wa mita 100 itazinduliwa.
Waziri Mwenye dhamana ya Mawasiliano na Miundombinu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hamadi Masoud, alithibitisha kwamba anataaarifa za ujio wa meli hiyo ambayo alisema kwa kiasi kikubwa itakuwa ni ya kutoa huduma tu na siyakutengeneza faida. Meli hiyo inauwezo wa kwenda kasi ya notkomail 20.
Monday, June 18, 2012
DIAMOND PLATINUM KUPAMBA MISS DAR INTERCOLLEGE 2012
MSANII
wa muziki wa kizazi kipya nchini Nasib Abdul ‘Diamond’ anatarajiwa
kupamba shindano la kumsaka Miss dar Intercollege 2012 linalotarajiwa
kufanyika Juni 22 kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa , uliopo mkabala
na chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
Mratibu
wa shindano hilo Dina Ismail amesema kwamba mbali na Diamond, onyesho
hilo pia litapambwa na burudani kutoka bendi ya Skylight iliyopo chini
ya mshiriki wa Tusker Project Fame mwaka juzi, Anneth Kushaba.
Alisema
maandalizi ya shindano hilo yanakwenda vema ambapo warembo 14
watakaosghiriki wanaendelea na mazoezi katika hoteli ya The Grand
Villa iliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam
“Mwaka
huu tumejipanga vema kuhakikisha mmoja ya warembo kutoka Miss Dar
Intercollege anafanya vema katika fainali za Miss Tanzania ,”alisema
Dina.
Warembo
watakaoshiriki shindano hilo wanatoka vyuo vya Biashara (CBE),
Uandishi wa Habari (DSJ) na Time, Ustawi wa Jamii, Usimamizi wa Fedha
(IFM) na Chuo Kikuu huria (OUT ambapo taji linashikiliwa na Rose Msuya
kutoka IFM, huku mshindi wa pili wa mwaka jana, Blessing Ngowi alitinga
fainali za Miss Tanzania.
Dina
aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na Veronica Ngota, Rose Muchunguzi,
Nancy Maganga, Hilda Edward, Diana Nyakisinda, Neema Michael, Veronica
Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, Saada Suleiman,
Rose Masanja na Jamila Hassan.
Shindano
hilo limedhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya
Redd’s,Dodoma Wine, Ndege Insurance, Skylight Band,Lamada Hotel, Screen
Masters,Makumbusho ya Taifa, Mustafa Hassanali, Shear Illusions, Lamada
Hotel,Grand Villa Hotel, Sporti Kizaa zaa, Clouds Fm na blog za Michuzi,
Mamapipiro, Bin Zubeiry,Mtaa kwa Mtaa na Fullshangwe.
MATRIDA MARTIN AWA MISS DAR CITY CENTER 2012
LISSA JENSEN NDIYE MISS WORLD TANZANIA 2012
Redds
Miss Tanzania, Lisa Jensen ambaye atawaiwakilisha Tanzania katika
shindano la Miss World 2012 akiwa amepozi kwa picha mara baada ya
kuvishwa taji hilo katika shindano lilofanyika katika ukumbi wa 327
Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Redds Miss World akitoa mada wakati wa shindano hilo.
Washiriki walioingia katika hatua za tano bora
Sunday, June 17, 2012
EDDA MISS KIGAMBONI CITY 2012
| Warembo waliokuwa wakiwania taji la Miss Kigamboni City 2012 wakicheza show ya ufunguzi jukwaani. |
MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Mlimani jijini Dar es Salaam, Edda
Silyvester, 21, usiku wa kuamkia juzi alifanikiwa kutangazwa kuwa
mshindi wa taji la kitongoji cha Kigamboni 'Redd's Miss Kigamboni 2012'
katika shindano lililofanyika kwenye ukumbi wa Navy Beach.
Kutokana na ushindi huo Edda alizawadiwa kitita cha Sh. 500,000 taslimu
na mgeni rasmi katika shindano hilo, diwani wa Kata ya Kigamboni, Dotto
Msawa.
Nafasi ya pili katika shindano hilo lililopambwa na burudani safi kutoka
katika bendi ya FM Academia maarufu Wazee wa Ngwasuma ilichukuliwa na
Agnes Goodluck ambaye naye alipata zawadi ya Sh. 350,000.
Elizabeth Boniface alichaguliwa kuwa mshindi wa tatu na kupata zawadi ya
Sh. 300,000 huku nafasi ya nne ikienda kwa Esther Albert na mshindi
watano akiwa ni Khadija Kombo. Elizabeth na Khadija kila mmoja alipata
zawadi ya Sh. 200,000.
Jaji Mkuu wa shindano hilo, Benny Kisaka, alitangaza kuwa badala ya
warembo watatu atachukua warembo wote watano kwenda kushiriki katika
shindano la Kanda ya Temeke baadaye mwaka huu.
Warembo wengine walioshiriki shindano hilo walikuwa ni Sophia Martin,
Rosemary Peter, Doreen Kweka na Linnah David waliambulia kitita cha Sh.
150,000 kila mmoja.
Waratibu wa shindano hilo, kampuni ya K& L Media Solutions wanawashukuru wadau wote waliosaidia kufanikisha shindano hilo
Kwa kufanikisha onyesho hilo ambalo lilikuwa ni la mwisho kwenye kanda ya Temeke
Friday, June 15, 2012
NYUMBA YA WEMA SEPETU YENYE THAMANI YA 400ML
Nyumba Ina sebule mbili, Moja ni TV Room na ya pili ni Sitting Room. Hii juu (pichani)ni TV Room na chini (pichani) ni Sitting Room


Hiki ni chumba cha Wema Sepetu, kina Dressing Table mbili, Massage Chair pamoja na Mini Saloon.
Anachumba pembeni ambacho ni kwa ajili ya viatu na nguo.
Hapa ni sehemu maalum ya kufanyia interviews mbalimbali.

Sehemu ya Dining
Wema akiwa amepozi kwenye TV Room
`


Hiki ni chumba cha Wema Sepetu, kina Dressing Table mbili, Massage Chair pamoja na Mini Saloon.

Anachumba pembeni ambacho ni kwa ajili ya viatu na nguo.

Hapa ni sehemu maalum ya kufanyia interviews mbalimbali.

Sehemu ya Dining

Wema akiwa amepozi kwenye TV Room
`

MISS DAR INTER COLLEGE KUTEMBELEA MAKUMBUSHO YA TAIFA J'MOSI
WAREMBO wanaotarajiwa kushiriki shindano la Miss Dar Intercollege 2012 jumamosi hii wanatarajiwa kutembelea makumbusho ya Taifa kwa ajili ya kujifunza.
Shindano hilo linatarajiwa kufanyika katika ukumbi huo wa Makumbusho ya Taifa uliopo mkatabala na chuo cha usimamizi wa Fedha (IFM) Juni, 22 mwaka huu.
Mratibu wa shindano hilo Dina Ismail, alisema ziara hiyo itawasaidia sana warembo hao katika harakati zao za kielimu.
Alisema Makumbusho ya Taifa ni sehemu muhimu kwa kila Mtanzania kufahamu kutokana na kuwepo vitu vingi vya kihistoria vilivyopata kutokea katika karne zilizopita.
“Kama mjuavyo kule kuna kuna fuvu la mtu wa kwanza duniani (zinjathropas), vyombo, magari na vitu vingine vya kwanza kuanza kutumika,”alisema.
Dina aliongeza kuwa maandalizi kwa ajili ya shindano hilo yanakwenda vema ambapo washiriki 13 kutoka vyuo vya IFM, Ustawi wa Jamii, Chuo Cha Biashara (CBE), uandishi wa Habari (DSJ) na Huria (OUT) wanaendelea na mazoezi kwenye hoteli ya The Grand Villa iliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Warembo hao ambao wapo chini ya ukufunzi Marlydia Boniface na Bob Rich ni pamoja na Veronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda Edward, Diana Nyakisinda, Neema Michael, Veronica Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.
Shindano hilo limedhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji cha Redd’s Original, Dodoma Wine, Ndege Insurance, Shear Illusions, Skylight Band, Lamada Hotel, Screen Masters, Makumbusho ya Taifa, Mustafa Hassanali, Grand Villa Hotel, Clouds Fm na blog za Michuzi, Mamapipiro, Bin Zubeiry, Mtaa kwa Mtaa na Full Shangwe.
Monday, June 11, 2012
BOB MAKANI AANGWA LEO JIJI DAR ES SALAAM
Waombolezaji
mabo wengi wao ni makada wa CHADEMA wakiwa wamebeba sanduku
lililohifadhi mwili wa Marehemu Bob Makani wakati mwili huo
ulipofikishwa katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam kwaajili
ya kutolewaheshima za Mwisho.
Vioongozi
wa juu wa Serikali akiwepo Rais Jakaya Kikwete (watatu kuli) Makamu wa
Rais, Dk. Gharib Bilali(wapili kulia) Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman
Mbowe (wa nne kulia) walihudhuria.
rais Kikwete akishiriki kubeba sanduku hilo.
CSTHERINE NDIYE REDDS MISS CHANG'OMBE 2012
Redds
Miss Chang’ombe 2012, Catherine Masumbigana 21, akipunga mkono mara
baada ya kusimikwa rasmi kuwa mshindi wa taji hilo ambapo aliwashinda
warembo wengine 13 waliokuwa wakiwania taji la Chang’ombe na tiketi ya
kushiriki Miss Temeke 2012.

Redds
Miss Chang’ombe 2012, Catherine Masumbigana 21, (katikati) akipunga
mkono mara baada ya kusimikwa rasmi kuwa mshindi wa taji hilo. Kulia ni
mmshindi wa pili, Jesca Haule (18) na Mshindi wa tatu Zulfa Bundala.
Masumbigana aliwashinda warembo wengine 13 katika shindano hilo
lililofanyika katika Ukumbi wa Quality Center jijini Dar es Salaam Juni
10, 2012.

Tano
bora ya Miss Chang’ombe 2012 ambao wote wamepata tiketi ya kushiriki
shindano la Miss Temeke 2012 wakiwa katika picha ya pamoja. Kutoka
Kushoto ni Zulfa Bundala (21), Jesca Haule (18), Catherine Masumbigana
(21), Miriam Nkisigwa (20) na Flora Kazungu.

Warembo wakicheza show maalum ya ufunguzi

Warembo wakipita na mavazi ya ubunifu. Kutoka kulia ni Debora Nyakisinda, Like Abraham na Jesca Haule.

Ilifika
zamu ya waarembo wakupita na vazi la ufukweni mbele ya majaji na
wapenzi wa sanaa ya urembo nchini waliokuwapo ukumbini hapo. Kutoka
kulia ni Debora Nyakisinda, Like Abraham na Jesca Haule.

Vazi la ufukwenu, Kutoka kulia ni Restituta Faustiney, Wensley Mabula na Clara Diu.

Miss Chang'ombe 2012, Catherine Masumbigana alivyojinadi na vazi la ufukweni

Warembo Flora Mayasa (kulia) Catherine Masumbigana (katikati) na Elizabeth Mushi wakiwinda point na vazi la ufukweni.

Kila mmoja alirusha kete yake, Latifa Mabewa (kulia) akijinadi na Zulfa Bundala

Mkali wa Bongo Fleva Nassib Abdul 'Diamond' na vijana wake walisindikiza show hiyo kwa kutoa burudani kali jukwaani.
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Vijana (Mb) Amos Makala akizungumza jukwaani.
Waratibu wa shindano hilo kutoka King Promotors wakifuatilia onesho. Kushoto ni Tom Chilala.
Mgeni
Rasmi Amos Makala (kushoto) akimpongeza Mshindi Miss Chang'ombe,
Catherine Masumbigana kwa kutwaa taji hilo. Kulia ni Mbunge wa Ludewa,
Deo Filikunjombe.
Amos Makala (kushoto) akizungumza na Viongozi Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga (kulia) na Prashant Patel.
Wapenzi wa urembo kutoka Chuo Kikuu cha Kampala tawi la Dar es Salaam nao walikuwepo.
Washiriki wa Miss Ilala 2012 kutoka Kitongoji cha Tabata jijini Dar es Salaam nao hawakukosekana
Familia ya Miss Tanzania 2011, nayo ilikuwepo ni mama yake na mdogo wake.
Vimwana
wa Kurasini ambao pia wamepata tiketi ya kushiriki Miss Temeke 2012
wakiwa ukumbini kushuhudia wapinzani wao wapya walioingia kushiriki nao.
Wadau kutoka Kampumi ya NeXus walidhamini shindano hilo na kulifuatilia kwa ukaribu zaidi.
Vijana wa Mapacha watatu walikuwepo jukwaani na kutoa burudani kali.
Subscribe to:
Posts (Atom)
























