Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Monday, January 14, 2013

WEMA SEPETU NA JB FULL KUKUMBATIANA KILIMO KWANZA DODOMA


Wema Isaac Sepetu na Jacob Steven ‘JB’ wakiwa wamekumbatiana.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na mwanahabari wetu lilijiri katika Kijiji Cha Kwadelo wilayani Kondoa, Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo mastaa hao walikwenda kuzindua mpango wa Kilimo Kwanza, Ajira kwa Vijana ulioongozwa na Diwani wa Kata ya Kwadelo, Omary Kariati.
Waigizaji hao walionekana kupeana ‘kampani’ kwa kila walichokifanya, huku kila mmoja akigandisha mkono kiunoni kwa mwenzake na kushikanashikana hadharani huku Wema akideka na ‘kale kasauti kake kanakoweza kumtoa nyoka haraka pangoni’.
...Wakiwa pamoja kimahaba.
“Hawa wasanii wetu bwana, hebu waone wale (Wema na JB), muda wote wameshikana vile. Mh! Ndiyo nini sasa?” alisikika mmoja wa maustadhi aliyejitokeza katika uzinduzi huo.
Wakiwa mashambani, ulifika wakati wa mastaa hao kulima kwa kutumia trekta ambapo JB alionekana akimbeba Wema na kumsaidia kupanda kwenye trekta kisha akamsaidia tena kushuka baada ya kumaliza kazi.

MUONEKANO MPYA WA UNIQUE MODEL CATHERINE


Unique model of the the year 2012(catherine Masumbigana) ni celebrity hivyo muonekano wake hubadilika siku hadi siku,tizama umati unavyomshangaa,ooh mamaaah....she roc the country.   Big up my doughter Cathy

Today

Big up u have reached a top step. I pray that u reach to the very top dear
  written by Britney urasa (spontchick brit)

MKENYA ADUNDWA NA MTANZANIA MASUMBWI

Bondia Mtanzania Thomas Mashali kushoto akiwa amemgalagaza bondia Bernad Mackoliech na kwenda chini akimsubili ili amwendelezee kipondo wakati wa mchezo wao wa kugombania ubingwa wa Afrika Mashariki uliofanyika katika ukumbi wa Friends Conner, Manzese jijini Dar es Salaam na Mashali kuibuka na ushindi wa K,O katika raundi ya sita.

 Bondia Bernad Mackoliech wa kenya na Mtanzania Thomas Mashali wakioneshana ufundi wa kutupiana makonde wakati wa mchezo wao wa ubingwa wa Afrika Mashariki Mashali alishinda kwa K,O raundi ya sita.
Refarii Mark Hatia akimwesabia Bondia Bernad Mackoliech huku akimuamulu Thomas Mashalikwenda katika kona nyeupe baada ya kumtwanga konde zito lililomsababisha kulamba sakafu wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa Afrika Mashariki

Kamanda wa polisi mkoa wa Kipolisi wa kinondoni Charles Kenyela akimvisha ubingwa wa Afrika Mashariki bondia Thomas Mashali baada ya kumpiga Bernad Mackoliech wa Kenya kwa K,O Raundi ya 6 picha na wwww.superdboxingcoach.blogspot.com

MMOJA APASUKA KICHWA AJALI YA GARI TWTZ JIJINI DAR

 Baadhi ya askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ, wakimshusha mwenzao baada ya kujigonga kwenye mti na kujeruhiwa vibaya na kupasuka kichwa wakati akiwa kwenye Lori lenye namba za usajili 5514 JW 07 aina ya IVECO kandokando ya barabara ya Samora jirani na Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar es Salaam leo jio.
 Baadhi ya wasamalia wema wakimpeleka hospitali majeruhi huyo.
 Majeruhi akiingizwa katika Bajaji tayari kwa ajili ya kupelekwa hospitali.
 Lori aina ya IVECO ambalo majeruhi huyo alikuwa amepanda.
 Hii ndio Barabara ya Samora ilipotokea ajali hiyo. 
Hapa ndipo alipojigonga majeruhi na kupasuka kichwa. Picha na Habari Mseto

GARI YA MARIO BALOTELI GUMZO

http://cdn.bleacherreport.net/images_root/article/media_slots/photos/000/623/444/mario-balotelli-car_original.jpg?1353707407

Gari yenye thamani ya Tshs 337,505,000 inayomilikiwa na msakata kambumbu huko majuu Mario Baloteli,kibongobongo lazima wajeda wamdake.

Sunday, January 13, 2013

UNIQUE MODEL CATHERINE MASUMBIGANA NA UNIQUE PHOTOGENIC ELIZABETH PERTTTY

Umique model 2012 Catherine Masumbigana (alienyosha mikono juu) akiwa na Unique model photogenic Elizabeth Pertty (wa kwanza kutoka kulia) na rafikize kwa picha iliyopigwa kwa mapozi ya kiunamitindo huku wakishow love!  teh teh.....
Hapa ni siku ile alipovishwa taji la mwanamitindo bora wa mwaka kwa kugha ya kikristo unique model of the year 2012.

Saturday, January 12, 2013

ASKARI JWTZ ALIEPIGA PICHA NA MBUNGE WA CHADEMA ATUPWA JELA MIAKA MINNE


Abubakari Kikulu (29), alipiga picha na mbunge huyo Desemba 23 mwaka jana, baada ya Lema kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara eneo la Mererani, ikiwa ni sehemu ya mikutano aliyoifanya kutokana na Mahakama ya Rufani Tanzania kumrejeshea ubunge wake.


Mbali na kupiga picha hiyo na Lema pamoja na Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari, kijana huyo alionekana katika picha hiyo akionyesha vidole viwili, ambayo ni alama ya Chadema.

Hata hivyo, baada ya picha hiyo, JWTZ lilimtilia shaka kijana huyo na kutangaza rasmi kumsaka, ili lijiridhishe kama ni mmoja wa wanajeshi wake.
Baada ya kumsaka kwa takriban siku 12, kijana huyo alikamatwa Januari 3, katika Mji wa Bomang’ombe wilayani Hai na baada ya kupekuliwa alikutwa na sare hizo.


Jana, Kikulu alifikishwa mahakamani mjini Moshi, akiwa chini ya ulinzi wa polisi na kusomewa mashtaka mawili, ambayo yote alikiri kuyafanya kama ilivyodaiwa mahakamani.
Baada ya kukiri kosa hilo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Kilimanjaro, alimhukumu kifungo cha miaka minne jela, ili iwe fundisho wa wakosaji wengine wa aina hiyo.


Kabla ya hukumu hiyo, Wakili wa Serikali, Ignas Mwinuka alimsomea mshtakiwa huyo mashitaka yake mawili, likiwamo la kujifanya Ofisa wa Jeshi, wakati akijua ni uongo.
Wakili huyo alidai mahakamani kuwa Januari 3, mwaka huu katika eneo la Bomang’ombe wilayani Hai, mtuhumiwa huyo alijitambulisha kama mtumishi wa umma.


Katika shtaka la pili, wakili huyo alidai siku hiyo hiyo katika Mtaa wa Msikitini, eneo hilo la Bomang’ombe, mtuhumiwa alipatikana na sare za JWTZ kinyume cha sheria.

Sare hizo ni pamoja na suruali moja, mashati mawili na kofia mbili, vyote vikiwa na alama za Jeshi la Wananchi wa Tanzania la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Baada ya Hakimu Kobelo kumuuliza mshtakiwa kama ni kweli alitenda makosa anayoshitakiwa, mshtakiwa huyo alikiri makosa yake katika hali ambayo haikutarajiwa.

Kutokana na kukiri kwake makosa hayo, Hakimu Kobelo alimhukumu kifungo cha miaka miwili kwa kosa la kwanza la kujifanya Ofisa wa JWTZ na miaka mingine miwili kwa kosa la pili.
Hata hivyo, Hakimu Kobelo alisema kuwa kwa kuwa adhabu hizo zinakwenda kwa pamoja (concurrent), mshtakiwa huyo atatumikia kifungo cha miaka miwili jela.


Kwa mujibu wa hakimu huyo, kosa alilolifanya mtuhumiwa huyo ni baya na linastahili adhabu kali, ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaotumia vibaya sare za majeshi nchini.

DEREVA BODABODA AGONGA DALADALA NA KUFA PAPOHAPO JIJINI MWANZA

Ajali iliyotokea jana jioni eneo la Igoma jijini Mwanza na kusababisha kifo cha mtu mmoja ambaye anatajwa kuwa ni abiria ambaye alikuwa amembeba dereva wa pikipiki hiyo iliyopata ajali yenye namba za usajili T988 BDW.
 Ambapo dereva wake ndiye mmiliki aliyekuwa amepakizwa alikimbia mara baada ya ajali hiyo kutokea,inasemekana
 Pikipiki hiyo iliyokuwa kwenye mwendo kasi iligonga kwa nyuma basi la abiria aina ya daladala lenye namba za usajili T768ASA lililosimama ghafla mbele ya pikipiki hiyo kwa ajili ya kupakia abiria.
Gsengo

MENEJA; PAH ONE HAIJAVUNJIKA

WAKATI kukiwa na tetesi kuwa lile kundi la muziki wa bongo fleva Pah One, limevunjika meneja wa kundi hilo amekana ishu hiyo na kudai kuwa kundi bado lipo lakini kikubwa ambacho kilitokea ni kutokuelewana ndipo baadhi ya wasanii walipoamua kusafiri na kubaki wawili na watakaporejea wataendelea kama kawaida.
Kundi hilo linaundwa na vijana wanne ambao ni Nahreel , Ola, Aika na Igwee ambao wamekuwa wakifanya muziki wa tofauti ambao unaweza kuwatambulisha zaidi hata kimataifa.

Hata hivyo meneja huyo alipotakiwa kujitambulisha jina lake alidai huwa hapendi jina lake litokee kwenye vyombo vya habari na kitu anachokifanya yenye ni kuwasaidia vijana.

Friday, January 11, 2013

UNIQUE MODEL OF THE YEAR 2012/2013 CATHERINE MASUMBIGANA KUWASHA MOTO LADY IN RED

 Mwanamitindo aliebuka na taji la Unique model of the year 2012/2013 kutoka katika shindano la Unique model 2012 Catherine masumbigana anatarajiwa kuonekana kwa mara kwanza karika runway ya lady in Lady baada ya kunyakua taji hilo mwishoni mwa mwaka jana.
 Catherine Masumbigana ndiye atakaekuwa yule mwanamitindo atakaetoka na vazi la LADY IN RED usiku wa tarehe 9 february.
 Mipango na mikakati ya mwanamitindo huyu ni kusonga mbele katika tasnia ya mitindo na kuhamasisha tasnia ya mitindo kwa wanamitindo wachanga kukua siku hadi siku katika sanaa.

NICKI MINAJ APATA BOYFREND MPYA

.

011013_minaj_launch

Nicki Minaj has a new man, and the undeniable proof is ... missing. But we do have this video -- which is 100% partial evidence ... that she left a restaurant!! See? Totally banging a new bf.

FLORAH MBASHA ATINGA UBALOZI TANZANIA UK


Mheshimiwa Balozi, Peter Kallaghe, akipokea zawadi ya CD na DVD kutoka kwa Wanainjili hao Dada Flora Mbasha na Mumewe Bwana E. Mbasha. Wanainjili hao wakiwa nchini Uingereza, walitembelea Miji ya Glasgow, Chemsford na Reading na wanatarajiwa kurejea Tanzania kesho siku ya Ijumaa 11/01/2013
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe, akiwa kwenye picha ya pamoja na wanamuziki maarufu wa Kimataifa wa nyimbo za Injili Dada Flora Mbasha na Mumewe Bwana E. Mbasha (Kulia), Askofu Ernest Irungu, ambaye ni Kiongozi wa nyimbo za Injili na ni Mkuu wa Chuo cha Vision College of Theology kilichopo London, Uingereza, mama Zest Irungu (mke wa Bishop Irungu) na Bibi. Mwambola, walipotembelea Ofisi za Ubalozi jana. Bwana na Bibi Mbasha wapo nchini Uingereza, wakitokea Amerika kujitangaza na kutangaza Injili.

OMBAOMBA ALIEJIFANYA MLEMAVU ATIMUA MBIO BAADA YA KUGUNDULIKA SIO MLEMAVU

Baada ya kugundua wananchi wamemshtukia baada ya kumhoji maswali na kushindwa kujibu aliamua kutimua mbio kukwepa kamera ya Francis Godwin isimpate picha yake, kama unavyomuona hapo mdau mguu gafla umetokea kimiujiza pamoja na mkono, yote hiyo alikuwa ameificha kwa kutumia koti lake na Suruali alizovaa. 
Baada ya hali kuwa tete alijikuta anazisahaumpaka kandambili zake, kama unavyoziona. 
Huyu ni omba omba anayeigiza kutokuwa na mkono mmoja na mguu Mmoja akiwa amekaa eneo la M.R Iringa mjini akisubiri kuomba chochote kutoka kwa wapita njia leo.

Ule usemi wa wahenga kuwa ukistaajabu ya mussa utayaona ya firauni leo umetimia katika eneo la M.R mjini Iringa baada ya wananchi waliokuwepo eneo hilo kupigwa na butwaa baada ya mzee janja ambaye amekuwa akishinda eneo hilo na kujifanya mlemavu asiyekuwa na mkono mmoja na mguu mmoja kutimua mboni kukwepa kamera ya mtandao huu.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 8 mchana baada ya camera ya mtandao huo kufika eneo hilo la kushuhudia umati wa wananchi wakiendelea kumpa fedha mzee janja huyo ambae alijifanya mlemavu wa vuongo na kuongea kwa shida .

Hata hivyo baada ya mmoja kati ya wananchi kufika eneo hilo alionyesha kufichua mbinu hiyo chafu ya mzee huyo kujifanya ni mlemavu wakati asubuhi alikutana nae maeneo ya mjini akiwa mzima wa afya njema na katika kumhoji zaidi ndipo kamera ya mtandao huu ilipoamua kufanya kazi yake ya kunasa kituko hicho na ndipo mzee huyo alipoanza kuongea kwa sauti vizuri tofauti na alivyokuwa akijifanya kuwa hawezi kuongea kabisa (bubu)

Wakati mabishano yakiendelea eneo hilo ghafla mzee huyo alisimama kwa miguu yake yote miwili pamoja tofauti na  awali alivyokuwa akijifanya ni mlemavu asiye na mguu mmoja ila baada ya watu kutaka apigwe picha ndipo mzee huyo alipoanza kutimua mbio huku ulemavu aliokuwa nao akiusahau hapo pamoja na kandambili zake na hakuna mtu aliyeweza kumfukuza na kufanikiwa kumkuta.

Baadhi ya wananchi wameuomba uongozi wa Manispaa ya Iringa kuwabana omba omba hao ambao wamekuwa wakidanganya watu kuwa wao ni walemavu kumbe ni wazima na kutaka kuwepo kw

Thursday, January 10, 2013

WANAFUNZI WA KIKE WALIONGOZA MATOKEO DARASA LA SABA HAWA HAPA

Wanafunzi walioongoza mtihani wa taifa wa darasa la saba wa mwaka 2012, Janeth Kijazi (kushoto) Justina Kalala (katikati)na Kellen Mudogo wakiwa shule ya sekondari ya wasichana, St Marian Bagamoyo, jana, walikoanza kidato cha kwanza. Wanafunzi hao walihitimu elimu ya msingi katika Shule ya Tusiime ya jijini Dar es Salaam. Picha Florence Majani

MATEKA 50 WA IRANI WAACHIWA HURU NA WAASI WA SYRIA


Waasi nchini Syria wamewaachia huru raia 50 wa Iran waliowakamata mwaka uliopita, kwa masharti la kubadilisha na zaidi ya raia 2000 wanaoshikiliwa na serikali ya Rais Bashar al Assad.

Raia 48 wa Iran wanaotuhumiwa kuwa wafuasi wa kundi la Islamic Revolutionary Guard Corps waliotumwa kupigana upande wa serikali wameonekana katika hotel mjini Damascus wakiwa katika hali nzuri kiafya.

 Iran, mshirika wa karibu wa serikali ya Assad, alisema kuwa watu hao ni mahujaji wa madhehebu ya Shia waliokuja nchini Syria kufanya ibada katika maeneo tukufu.
Wakati huohuo, Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kwenye mzozo wa Syria Lakhdar Brahimi yuko mbioni  kukutana na maafisa wa ngazi za juu wa Marekani na Urusi mjini Geneva kesho Ijumaa.
Mkutano huu unafanyika ikiwa ni siku kadhaa baada ya Rais Assad kutoa hotuba yake ambayo ilitaka kuwepo kwa majadiliano ya amani yatakayomaliza machafuko nchini humo. Hata hivyo Jumatano iliyopita bwana Brahimi aliita hotuba hiyo ya Assad kuwa ni ya kidini na yenye kupendelea upande mmoja.

AJALI YA BUNDA EXPRESS ILIVYOTOKEA JANA WILAYANI MAGU

Eneo la katikati ya Lugeye na Nyanguge basi la abiria la 'Bunda Express' lenye namba za usajili T 782 BKZ likitokea Musoma kuelekea Mwanza muda wa saa mbili asubuhi jana lilipata ajali mbaya, mazingira yanaonesha kuwa idadi kubwa ya watu wamekutwa na umauti na wengine kuwa majeruhi na mvua kubwa ilikuwa ikinyesha. Eneo la magu basi la abiria la 'Bunda Express' lenye namba za usajili T 782 BKZ likitokea Musoma kuelekea Mwanza muda wa saa mbili asubuhi jana lilipata ajali mbaya, mazingira yanaonesha kuwa idadi kubwa ya watu wamekutwa na umauti na wengine kuwa majeruhi na mvua kubwa ilikuwa ikinyesha.

Wednesday, January 9, 2013

KESI YA MAUAJI YA KUCHOMWA MOTO MWIZI YAMTESA JOSE CHAMELEONE

Gazeti la Sunday Mail la Uganda limeripoti kwamba Polisi wa nchi hiyo wanaendesha uchunguzi ambapo huenda wakamfungulia mashitaka ya mauaji mwanamuziki Joseph Mayanja, mke wake Daniella na kundi la muziki la Leon Island.
Ni kutokana na kifo cha Robert Karamagi (27) aliyefariki katika Hospitali ya Mulago baada ya majeraha aliyoyapata nyumbani  kwa mwanamuziki huyo huko Seguku Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Kajjansi Ibrahim Saiga alisema wamechukua ushahidi mbalimbali kutoka kwa majirani na mashuhuda walioona, ushahidi ambao unapingana na ule uliotolewa na familia ya Mayanja.

Pamoja na kusema faili la uchunguzi huo litapelekwa kwa Mwendesha Mashitaka wa Serikali (DPP) kwa ushauri,  Saiga alisema pia baba wa Karamagi alikana kwamba mwanaye alijimwagia mafuta na kujiwasha moto, pia alisema mwanaye alipomwita hospitalini alimwambia aliteswa, akafungwa kamba, akamwagiwa mafuta na kuchomwa moto na mwanamuziki huyo pamoja na wenzake wa kundi lake.

Jose Chameleone akihojiwa na NTV Uganda na kusema kwamba hilo swala wameliacha kwenye mikono ya polisi, gazeti la sunday mail limeripoti pia kwamba alhamisi iliyopita Jose Chameleone alihojiwa na wapelelezi kwa muda mrefu lakini aliachiwa kwa dhamana.

MWANDISHI WA HABARI APIGWA RISASI NA KUNYOGWA HADI KUFA MKOANI KIGOMA

Mwansidhi wa Habari wa Kituo cha Redio Kwizera wilayani Kakonko, Mkoa wa Kigoma, Issa Ngumba (45) enzi za uhai wake.
 MWANDISHI wa Habari wa Kituo cha Redio Kwizera wilayani Kakonko, Mkoa wa Kigoma, Issa Ngumba (45), ameuawa kwa kupigwa risasi na kunyongwa na watu wasiofahamika.

Habari zilizopatikana jana zimeeleza kuwa mwili wa mwandishi huyo ulikutwa porini, siku tatu tangu alipotoweka nyumbani kwake katika mazingira ya kutatanisha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Frasser Kashai alithibitisha tukio hilo, lakini akasema asingeweza kulizungumzia kwa undani kwa kuwa polisi walikuwa bado eneo la tukio.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema mwandishi huyo alikutwa jana akiwa amekufa, huku mwili wake ukiwa na majeraha ya risasi na ukiwa umenyongwa na pembeni yake kulikuwa bastola iliyokuwa imetelekezwa pamoja na simu zake mbili za mkononi.

“Mwili wake ulipatikana jana katika Pori la Mlima Kajuluheta ulioko katika Kijiji cha Muhange, Kakonko asubuhi baada ya wananchi kufanya msako wa siku tatu tangu Jumapili iliyopita ikiwa ni siku moja baada ya kupotea katika mazingira ya kutatanisha,” alisema mmoja wa  mashuhuda hao.

Imeelezwa kuwa pamoja  na vifaa hivyo, pia katika eneo hilo la tukio kulikutwa risasi tano na katika mfuko mmoja wa suruali ya marehemu, kulikuwa na noti moja ya Sh10,000.

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Kigoma (KPC) Deogratius Nsokolo alisema: “Sisi ndiyo kwanza tunaelekea eneo la tukio, lakini waandishi wa Wilaya ya Kibondo ambao waliwahi kufika eneo la tukio na kushuhudia uchunguzi wa daktari, wameeleza kuwa marehemu amekufa kwa kunyongwa na kupigwa risasi mkono wa kushoto.”

“Tunaelekea Wilaya ya Kakonko kutoka Kigoma Mjini, lakini daktari amesema maiti inaonekana kunyongwa shingo na kupigwa risasi mkononi.”

Alisema mwili huo ulifanyiwa uchunguzi na daktari Primus Ijumaa wa Hospitali ya Wilaya ya Kibondo.

Kamanda Kashai alisema jeshi lake linasubiri taarifa ya daktari aliyefanya uchunguzi wa mwili wa marehemu pamoja na taarifa za awali za uchunguzi kabla ya kutoa taarifa kamili kwa waandishi wa habari.

Naibu Mhariri wa Kituo cha Redio Kwizera kinachorusha matangazo yake kutoka wilayani Ngara mkoani Kagera, Seifu Upupu alisema mwandishi huyo alipotea tangu Januari 5, mwaka huu saa kumi na moja jioni.

“Simu zake zilikuwa zikiita bila kupokewa kwa muda wote na hadi jana (juzi) zikawa hazipatikani kabisa,’ alisema Upupu na kuongeza:

DIGITALI YAINGIA KWENYE BAJAJI

Mfumo wa Digitali umeingia kwa bajaji....ni kwamba haina chenga unamuona abiria kama alivyo..ni rahisi kupanda na kushuka kwa upande wowote unakaa kama uko bar kwa raha zako na haikuzuii kupata upepo toka mwelekeo wowote ule,haya ndiyo mambo ya digitali bhana..!!.

DARAJA LINALOKARIBIA KUCHUKUA ROHO ZA WATU NA SERIKALI IKO TULII


Wakati serikali ikiahidi kukamilisha ujenzi wa madaraja yapatayo 10 sehemu mbalimbali nchini huku ujenzi na ufunguzi wa madaraja hayo ukiendelea kufanyika hali iko hivi katika daraja la Sukuma lililopo katika barabara kuu inayounganisha vijiji vya wilaya ya Magu mkoani Mwanza.


Daraja hili mbao zake zimesagika kabisa kiasi cha kufanya magari yanayopita kutumia daraja hili muhimu kupita kwa mwendo wa kusuasua yakihofia kukumbwa na maafa. 


Mbao zilizo chomoka zimeegeshwa tu, mawe yametumika kuziba mashimo ya uwazi kati ya nondo na nondo hii ni hatari si kwa magari tu bali hata kwa waendao kwa miguu hali inayosababisha hata waendeshao baskeli kushuka na kuzikokota baiskeli zao wakihofia usalama wao.