Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Friday, February 15, 2013

UNIQUE MODEL CATHERINE ALIVYONG'ARA ONYESHO LA LADY IN RED 2013


Mshindi wa shindano la Unique model 2012Catherine Masumbigana akionyesha mavazi katika onyesho la mavazi la Lady in Red,onyesho hili lilifanyika Serena hotel jijini dar mwishoni mwa wiki iliyopita.

Monday, February 11, 2013

PENZI LA DIAMOND NA PENNIEL LAPAMBA MOTO!

 
Uvumi ulionea kuhusiana na muunganiko wa mapenzi kati ya Diamond Platnum na DTV VJ Penniel  kua ni  wapenzi baada ya kusambaa kwa picha kwenye mitandao ya kijamii inayowaonesha wakiwa pamoja kitandani na kula bata sehemu mbalimbali.
Juzi Diamond alithibitisha rasmi kuwa kwa sasa anajivinjari shuka moja na mdada huy huyo kwa kupost picha ya Penny kwenye mtandao wa Instagram na kuandika:.
 #MaBabyMama #De’MumOfMyBlood #MamaYounDiamond #YounPlatnumz #YoungPrezident…..

Mwenye macho haambiwi tizama,pia penniel amekuwa karibu sana na mama Diamond kwa kipindi hiki ambapo wachambuzi wa mambo ya kichokonozi wanadai ni katika hali ya kuweka mazingira ya kukubalika ukweni.

WEMA ATOKA NA MBABA


STAA wa filamu mwenye jina kubwa Bongo, Wema Abraham Sepetu, juzikati alitupia picha yake akiwa kimahaba zaidi na mwanaume aliyedai kuwa ni ‘mume’ wake.

Picha hiyo ambayo aliiweka kwenye mtandao wa BBM inamuonesha msanii huyo akibusiana na mwanaume huyo lakini wakionekana kuanzia kwenye kidevu hadi kwenye kiuno.

Baada ya kuitupia picha hiyo, Wema aliandika: ‘Miss you mume wangu, wewe ndio kila kitu katika maisha yangu, watasema sana lakini mambo yetu yanatuendea vizuri.” 


Maneno hayo yanaashiria kuwa Wema anampenda sana mwanaume huyo ambaye siyo Diamond.

RED CARPET YA GRAMMY AWARDS 2013



The Roots arrive at the 55th Annual Grammy Awards at the Staples Center in Los Angeles, CA on February 10, 2013.

Alicia Keys.

Rihanna.
Kelly Rowland.
Beyonce.
Jennifer Lopez.
Adelle.
Janelle Monae.
Ashanti.
Tamia.
Taylor Swift.
Chrissy Teigen and John Legend arrive at the 55th Annual Grammy Awards at the Staples Center in Los Angeles, CA on February 10, 2013.
LL Cool J and wife Simone Johnson.
Faith Hill and Tim McGraw.
Jack Antonoff, Nate Ruess, and Andrew Dost.
Justin Timberlake.
Drake.
Chris Brown.
Nas.
Neyo.

Wiz Khalifa and Amber Rose.

Rick Ross.
Jennifer Lopez and Casper Smart.

Friday, February 8, 2013

MSANII MATUMAINI HOI KWA MARADHI ATUA JIJINI TOKA MSUMBIJI

MSANII wa vichekesho ambaye alikuwa nchini Msumbiji, Tumaini Mwakibibi ‘Matumaini’ jana alipokelewa na wasanii wenzake kibao baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar akiwa hoi kutokana na kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.
 
Matumaini alitua uwanjani hapo jana majira ya saa 9:30 alasiri ambapo kutokana na hali yake kuwa mbaya wasanii walimbeba mgongoni na kumfikisha kwenye gari ambapo walimpeleka moja kwa moja hospitali ya Amana alikolazwa mpaka sasa akiendelea kupatiwa matibabu.

Thursday, February 7, 2013

MTOTO MCHANGA ATUPWA KWENYE DAMBO BAADA YA KUZALIWA

 (Tunaomba radhi kwa picha hii si nzuri,ila tunaiweka kukemea matendo ya kinyama dhidi ya watoto)
 
ZIKIWA zimepita  siku takriban tano toka kukutwa kwa mwili  wa mtoto mchanga katika eneo la Semtema jirani na makazi ya  wanafunzi wa chuo kimoja cha dini mkoani Iringa, simanzi na majonzi zimeendelea kutanda katika Manispaa hiyo baada ya mtoto mwingine wa jinsi ya kike kutupwa katika dampo la taka eneo la Stendi ya M.R mjini Iringa.

Wakizungumzia  matukio hayo ya wanawake wasiofahamika  kufanya vitendo hivyo vya ukatili dhidi ya watoto wanaowazaa, baadhi ya akina mama wamelitaka jeshi la polisi na jamii nzima kusaidiana kuendesha misako dhidi ya  wanawake  wanaofanya vitendo hivyo vya kikatili.

Sarah Sanga, mkazi wa Miyomboni mjini hapa alisema kuwa  matukio ya wanawake kutoa mimba na kutupa watoto  yameendelea na kuwa ni tishio katika Manispaa ya Iringa.

Bwana Said alishauri wanawake kuwafichua wenzao ambao siku za karibuni walionekana na mimba na ghafla mimba hizo kutoweka kwani  wanaweza kuwa wahusika lakini akawalaumu wanaume kwamba wanaweza kuwa chanzo cha tatizo hilo.

Mkuu  wa Wilaya  ya Iringa, Dk. Leticia Warioba akizungumzia tukio hilo amewataka mabinti na vijana wilayani hapo kuepuka  kupeana  mimba bila kuwa na uhakika wa ndoa.

“Serikali ya wilaya itaendelea kutoa elimu zaidi kwa vijana ili  kupunguza tatizo la watoto  kutupwa katika wilaya ya Iringa,” alisema

Jeshi la  Polisi Mkoa wa Iringa, limethibitisha kutokea kwa matukio hayo na kuahidi  kuendelea na msako mkali  ili kuwakamata  wahusika.

Mpekuzi.

FLAVIAN MATATA ABANGUA DILI LA DIESEL+EDUN


Mwanamitindo wa kimataifa kutoka nchini Tanzania Flaviana Matata ameshiriki katika kampeni za matangazo makubwa ya makampuni ya nguo ya DIESELna EDUN.

Kampeni ya DIESEL + EDUN ilianzishwa mwaka jana mwezi wa kwanza ambapo muanzilishi wa kampuni ya DIESEL – Renzo Rosso – na waanzalishi wa kampuni ya EDUN – Ali Hewson na Bono walisafiri hadi nchi za Uganda na Mali na kukutana na wakulima wa pamba barani Africa.

Waliingia makubaliano ya kutengeneza nguo maalum zitakazotokana na pamba ya wakulima hawa wa Afrika na hivyo kuwanufaisha moja kwa moja. Hivyo basi nguo hizi zinatangazwa kama kampeni ili kunufaisha bara la Afrika.

Nguo hizo zitaanza kupatikana mwanzoni mwa mwezi wa tatu katika maduka mbalimbali nchini Marekani na duniani. Pia nguo za DIESEL + EDUN zitauzwa kupitia mitandao mbalimbali.

Wednesday, February 6, 2013

KAULI YA SPIKA ANNA MAKINDA KUHUSU VURUGU ZA FEB 4 BUNGENI

Spika wa bunge Anne Makinda amesema taasisi ya bunge inalaani vurugu zilizojitokeza bungeni february 4 2013 na kusababisha kuahirishwa kwa kikao cha bunge wakati wa mjadala wa mbunge wa Ubungo John Mnyika (Chadema) kuhusu upatikanaji maji katika jiji la Dar es salaam.
Baada ya kipindi cha maswali na majibu february 5 2013 Spika Makinda kasema katika kikao cha dharura cha kamati ya uongozi kilichofanyika feb 4, kimelaani hizo vurugu na kuamua kupeleka hiyo ishu kwenye kamati ya haki, kinga na madaraka ya bunge ili kufanya uchunguzi na kuwasilisha bungeni matokeo ya uchunguzi huo.
Jingine lililojadiliwa na kufanyiwa maamuzi ni kamati kusitisha uwasilishwaji wa hoja zote binafsi za wabunge zilizotakiwa kuwasilishwa katika mkutano huu wa bunge ili kuepuka vurugu zinazoweza kutokea tena.
Baada ya hayo maelezo wabunge kadhaa walisimama na kuomba muongozo wa spika akiwemo mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari aliyehoji kuenguliwa kwa hoja yake, pia mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu aliyetaka kujua hatua zilizofikiwa katika rufaa za wabunge zilizokatwa kupinga maamuzi mbalimbali ya spika.
Namkariri mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari akisema “sasa kama fujo zinatokea bungeni na kupelekea hoja yangu kuondolewa, kamati iliyopaswa kukaa kuzungumza ni kamati ya maadili sio kamati ya uongozi, kamati ya uongozi kimsingi haina mamlaka ya kuondoa hoja yangu kwenye ratiba ya shughuli za leo, mh Spika naomba muongozo wako”
Mbunge Tundu Lissu alisema “kwa taratibu za kanuni za bunge, mbunge ambae haridhiki na uamuzi wa spika anatakiwa akate rufaa na naomba muongozo wako, rufaa zaidi ya 10 ambazo zimekatwa dhidi ya maamuzi ya kwako spika na muheshimiwa naibu spika… za tangu mwaka 1011, za mwaka jana,

RAPPER PREZZO KUFUNGA NDOA NA GOLDIE JUMAMOSI HII


Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali nchini Nigeria, rapper Jackson Makini aka Prezzo anatarajia kufunga ndoa na mwanamuziki wa Nigeria Goldie February 9.


Habari hiyo pia imeandikwa na website ya Big Brother Africa. Harusi hiyo itafanyika jijini Lagos, Nigeria.

Katika hatua nyingine mwakilishi wa mwaka jana wa Nigeria kwenye shindano la Big Brother Africa, anatarajia kuanzisha Reality TV show yake.Goldie anaanzisha show hiyo iitwayo ‘Tru Friendship’. ‘Tru Friendship’ itaonesha maisha ya kila siku ya muimbaji huyo wa Skibobo, Goldie, yote kama mtu maarufu na kama Susan Harvey.

Tuesday, February 5, 2013

KITALE ATWAA JIKO PEUPEE!

 Msanii wa Filamu za kuchekesha hapa nchini maarufu kama Kitale, jana amesherehekea siku yake muhim, kwa kufunga ndoa na mpenzi wake, ambae leo hii tunamuongelea kama mkewe, Bi Fatma Salum. 
Ndoa hiyo ilifungwa majira ya Saa nane mchana maeneo ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam, na kuhudhuriwa na watu kibao wakiwemo marafiki, ndugu na jamaa.

Friday, February 1, 2013

MAMA SHARO MILIONEA AMTOSA MTOTO ANAEDAIWA NI WA SHARO


MAMA wa aliyekuwa msanii wa muziki na filamu Bongo, Hussein Ramadhan Mkieti ‘Sharo Milionea’ amefungukia gari aliloacha mwanaye pamoja na mimba ambayo inadaiwa ni yake.

Akizungumzia  suala la gari, Mama Sharo amesema: “Kuhusu gari lile Toyota Opa aliloacha marehemu mwanangu naliuza kwani siwezi kuliendesha na haliwezi kukaa bila kufanya kazi yoyote.

“Kwa upande wa Marry Lucas wa Sumbawanga msichana aliyejitokeza baada ya Sharo kufariki na kusema ana ujauzito wake, siwezi kumtambua kwa sababu enzi za uhai Sharo hakuniambia kuwa ana mchumba wala mpenzi.”


Sharo Milionea alifariki dunia Nov 26, mwaka jana kwa ajali ya gari iliyotokea mkoani Tanga.


Siku chache baadaye, Marry aliibuka na kudai alikuwa mpenzi wa Sharo na ana ujauzito wake.

Thursday, January 31, 2013

UNIQUE MODEL CATHERINE AKIWA NA JUDIE SANGU

 Unique model Catherine akiwa katika pozi na Judie Sangu kipindi cha kambi ya shindano la unique model 2012.
Mandhali tulivu katika fukwe za hoteli ya Giraffe ocean view iliyopo jiini Dar es salaam.

WEMA SEPETU ALIVYOJIMWAGA KWA SERENGETI BOY WAKE

Wema Sepetu  ameamua  kuhamishia majeshi  yake  kwa  kiserengeti  boy  ili  kulipiza  kiasi  kwa X wake  wa zamani, DIAMOND.....
Huyu  ni  Haidary Cavilla  ambaye  ni mchumba  wa  miss  Tanzania namba  2 ,mwaka  2000, aitwaye  Mercy Galabawa....
Kama kawaida, jamaa  ni  mdogo kiumri akilinganishwa na Wema, lakini  inasemekana  kwama  Haidary  anamiliki  mkwanja mrefu  ulioichanganya  akili  ya  Wema Sepetu  hasa  baada  ya  kununuliwa gari aina  ya Audi Q7.....

Picha  hizi  zilipigwa  nyumbani  kwa wema  sepetu na  hatimaye  kuvuja  mitandaoni,hali inayoashiria  kulipiza  kisasi kwa Diamond  baada  ya kunaswa  akiwa  na  Penny....
  Wema sepetu ni mrembo anayekabiliwa na   skendo  chafu ya kubadiliwanaume kama  nguo.Alianza na..

KITALE KUFUNGA PINGU ZA MAISHA JUMAPILI HII

Msanii wa Filamu na uchekeshaji maarufu  kitale baada ya kupata maswali mengi sana kwa mashabiki wake,sasa jumapili hii anatarajia rasmi kupata jiko au lugha fasaha anatarajia kuoa.
Kwa mujibu wa Kitale alisema japokuwa amepitia katika changamoto mbalimbali za ki maisha na amejifunza mengi na ndiyo sababu ya kuvuta jiko.

KIWANDA CHA CHEMICOTEX-AFRICANA CHATEKETEA KWA MOTO


Habari tulizozipata hivi punde ni kuwa kiwanda cha Chemical Kotex chateketea kwa moto jana jioni, chanzo cha moto huo bado akijajulikana, kwa habari kamili tutazidi wajuza hapo baadae.
 

Wednesday, January 30, 2013

ALLY DAXX KWA MARA NYINGINE TENA

Yote haya ni katika drum magazine ,model mtanzania anaefanya vema anga za mandela, Ally daxx

UNIQUE MODEL CATHERINE MASUMBIGANA KUFUNGUA LADY IN RED FASHION SHOW 2013


Tuesday, January 29, 2013

MAITI YA KICHANGA YAGEUKA JOGOO HOSPITALI YA MWANANYAMALA



BADO tupo mwanzoni mwa mwaka lakini tukio la maiti ya kichanga kugeuka jogoo ndani ya chumba cha kuhifadhia maiti kwenye Hospitali ya Mwananyamala, jijini Dar es Salaam linaweza kuongoza mengine yote ya ajabu yanayoweza kujiri ndani ya 2013.

Mwananyama ni hospitali yenye hadhi ya mkoa kitabibu, ina rekodi za kuwa na matukio ya ajabu, ila hili siyo tu kwamba linaingia miongoni mwa hayo bali pia linaweza kutia fora.
Asubuhi ya Jumatano iliyopita, ilikuwa kizaazaa pale jokofu lililotumika kuhifadhi maiti ya kichanga cha mtoto, kukutwa kuna jogoo.


Mshangao zaidi ni kwamba ndani ya lile jokofu, pembeni ya yule jogoo, kulikuwa na hirizi pamoja na tunguri.


Habari kutoka vyanzo vyetu, zimewekwa wazi kuwa Jumanne iliyopita, saa 7 mchana, polisi walipigiwa simu, wakataarifiwa kuhusu maiti ya mtoto iliyokuwa imetelekezwa eneo la Kigogo, Mbuyuni, Dar es Salaam.


Vyanzo vyetu vimebainisha kuwa polisi baada ya kupata taarifa hizo walifika eneo la tukio na kukuta maiti hiyo ya kichanga ikiwa imefunikwa kwa kuzungushiwa sanda.


Kwa mujibu wa Moses Madilu, mkazi wa Kigogo, aliyedai kushuhudia tukio hilo, polisi walipofika eneo la tukio waliikagua maiti hiyo na kubaini kwamba ni ya kike.


Chanzo chetu kikaeleza kuwa baadhi ya mashuhuda, hususan wanawake, walitokwa na machozi kwa masikitiko kwamba itakuwa mtu alijifungua halafu akakinyonga kichanga hicho kabla ya kukitelekeza eneo hilo.


“Baada ya kujiridhisha kwa kazi yao, polisi waliichukua maiti hiyo ya kichanga, wakaipakia kwenye ‘difenda’, wakaipeleka Hospitali ya Mwananyamala,” kilieleza chanzo chetu.


HOSPITALI YA MWANANYAMALA
Ndani ya hospitali hiyo, mwandishi wetu alielezwa kuwa polisi walipofika, walishusha maiti hiyo na kumkabidhi mganga wa zamu aliyejulikana kwa jina moja la Dk. Liwa.


 “Dk. Liwa aliwaambia wale polisi wapeleke maiti hiyo mochwari.
“Polisi walifanya hivyo lakini kule mochwari walimkuta msimamizi mkuu, Omar Buyoya aliyekataa kuipokea kwa vile daktari hakuthibitisha kama kile kichanga kilikufa au kilikuwa hai.


“Polisi na Buyoya walivutana kwa muda mrefu, alitokea mhudumu mwingine wa mochwari aliyekuwa akijuana na polisi mmoja aliyebeba ile maiti, alikubali kuupokea mwili huo na kuingiza ndani kwenye jokofu la kuhifadhia maiti.”


Muuguzi huyo aliendelea kusema kuwa siku iliyofuata, Dk. Liwa alifika mochwari na alipofungua jokofu na kufunua sanda, badala ya kukuta maiti ya kichanga, alikuta jogoo, tunguri na hirizi.


“Dk.Liwa alipatwa  na mshangao mkubwa huku jasho likimtoka kutokana na uoga, aliwaita wafanyakazi ambao walijazana hapo  mochwari kushuhudia.


“Baadhi ya wafanyakazi walipigwa na butwaa huku wengine wakicheka hadi kudondoka chini na wakawa wanajiuliza kama kweli polisi wanaweza kupeleka jogoo hospitali au ni mambo ya kishirikina,” alisema muuguzi huyo.


Dk. Liwa na wafanyakazi wenzake waliondoka mochwari na kuacha hilo jogoo katika chumba cha maiti huku wakishindwa la kufanya.


KAULI YA MGANGA MKUU.....
Uwazi  ilimtafuta Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Dk. Sophinias Ngonyani ambaye alikiri  kuonekana kwa jogoo badala ya maiti ya kichanga.

“Polisi walituletea kifurushi wakiamini kuwa ni maiti ya kitoto kichanga ambapo tulikipokea lakini ilipotazamwa na daktari, tulikuta jogoo, hirizi na tunguri, tuliamua kumchoma moto kwa sababu kile ni chumba cha kuhifadhi maiti siyo cha kuhifadhia mizoga ya kuku, ng’ombe au mbwa,” alisema Dk. Ngonyani.


KAULI YA POLISI ...
Naye Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Charles Kenyela alipoulizwa juu ya sakata hilo alisema kwamba wao kama jeshi la polisi walipigiwa simu na raia mwema kuwa  kuna maiti ya kichanga ambapo askari waliondoka hadi eneo la tukio na kuichukua mpaka Hospitali ya Mwananyamala.


“Polisi waliichukua hadi Hospitali ya Mwananyamala kwa wataalamu na baada ya kuikabidhi waliondoka na kuendelea na shughuli nyingine, nami nashangaa kusikia kwamba madaktari walikuta  jogoo,” alisema Kenyela.


MASWALI MATANO
Je, ni kweli polisi waliikagua maiti na kugundua ni kichanga cha kike?


Kama ndiyo, ilikuwaje kikageuka jogoo?


Kwa nini daktari hakuipima ile maiti, badala yake akaelekeza ipelekwe mochwari?


Je, au polisi walibeba mzoga wa jogoo, wakampakia kwenye difenda wakidhani ni maiti ya kichanga?


Mkweli nani, polisi wanaodai kupeleka maiti ya kichanga, au hospitali wanaosema walipelekewa mzoga wa kuku, tunguri na hirizi?

Na Mpekuzi

RICK ROSE ANUSURIKA KUPIGWA RISASI ZA TUMBO


Imeripotiwa kwamba nyota Rick Ross, anusurika kujeruhiwa  baada ya mtu mmoja aliyekuwa na silaha kurusha risasi kadhaa kwenye gari yake aina ya Rolls Roys

Ndani ya gari hilo aliyekuwemo yeye na msichana mmoja na kusababisha kugonga nyumba akijaribu kuongeza mwendo,taarifa zilizotolewa na mashahidi

Taarifa za polisi zinasema kuwa asubuhi ya leo (jumatatu) wamepokea simu nyingi kutoka kwa wakazi ambao wanaishi maeneo ya Las Olas baada ya kusikia mlio wa risasi

polisi wanasema gari lingine lilisimama karibu na gari la nyota huyo  na mtu mmoja aliekuwa ndani ya gari hilo kuanza kurusha risasi kwenye gari la Ross

Nyota huyo  hakupatwa na risasi hata moja wakati wa tukio hilo na hakuna mtu yoyote aliyejeruhiwa ndani ya gari hilo.

Mpaka sasa hakuna alietuhumiwa, kugundulika wala kushikiliwa juu ya tukio hilo, polisi wanaendelea kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo

Thursday, January 24, 2013

WANANCHI WACHOMA NYUMBA ZA ASKARI POLISI MKOANI PWANI

KUNDI la wananchi wanaodaiwa kuwa na hasira, wamevamia kituo cha Polisi cha Kibiti Wilayani Rufiji na kufanya vurugu kubwa baada ya raia mmoja kufa kwa kile kilichodaiwa kipigo cha Polisi.

Chanzo chetu cha Habari kutoka Kibiti kinaipasha kuwa kijana aliyefariki kutokana na kipigo hicho ni Hamis Mpondi, ambaye mauti yamemfika wakati akipatiwa matibabu Hospitali ya Muhimbili.

Habari zaidi zinapasha kuwa hivi sasa wananchi hao wanaendelea kuteketeza nyumba za Askari Polisi hao zilizopo jirani na kituo hicho, licha ya Polisi kuendelea kufanya juhudi za kuwatawanya kwa mabomu katika eneo hilo.

Aidha wananchi hao wameanza kufunga barabara kuu ya Kilwa iendayo Mikoa ya Kusini, Lindi na Mtwara kwa mawe, magogo na kuchoma matairi ikiwa ni umbali wa kama kilometa moja kutoka kituo cha Polisi Kibiti.

Hali inaelezwa kuwa inazidi kuwa tete huku Polisi wa Kibiti wakiendelea na jitihada za kudhibiti hali hiyo kwa kufyatua mabomu hewani kujaribu kutawanya umati huo wa watu.  Vurugu zinaendelea, Habari kwa hisani ya Father Kidevu.