Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Thursday, May 9, 2013

ALIBINO AFUKUZWA SHULE KWA MADAI NI MCHAWI JIJINI MBEYA


.

KATIKA Hali isiyokuwa ya Kawaida Uongozi wa Shule ya Sekondari Hollwood iliyoko Mlowo Wilayani Mbozi Mkoa wa Mbeya imemsimamisha shule Mwanafunzi wa kidato cha tatu kwa takribani Miezi Miwili kwa madai kuwa anajihusisha na imani za Kishirikina.
  
Mwanafunzi huyo aliyejulikana kwa jina la Amina Mwankinga(20) ambaye ni mlemavu wa ngozi(Albino) alisimamishwa shule na uongozi wa Shule hiyo tangu Machi 9, Mwaka huu baada ya uongozi wa Shule hiyo kupata taarifa kutoka kwa Wanafunzi wakimtuhumu Mwenzao huyo kuwa ni Mshirikina.
  
Uongozi wa Shule hiyo baada ya kupata taarifa hizo ulimwamuru mhanga wa tukio hilo kuondoka Shuleni hapo pasipo kufuatilia na kujua ukweli wa jambo hilo na kupata udhibiti hivyo kumwacha Mwanafunzi huyo akizurura mitaani asijue hatma ya maisha yake.
  
Mhanga wa tukio hilo Amina Mwankinga alisema tangu tarehe tisa alipofukuzwa bwenini na wanafunzi wenzie wakitaka aondoke shuleni hapo majira ya usiku hali iliyomlazimu kuomba hifadhi kwa mlinzi aliyemkubalia na kukesha naye hadi asubuhi  hali iliyopelekea kupigwa na baridi kali kutokana na kukosa nguo za kujisitiri kama Shuka nk.

Anasema kutokana na hali hiyo Walimu pamoja na uongozi wa Shule hiyo haukuchukua hatua yoyote jambo lililomlazimu kuondoka Shuleni hapo  baada ya kukosa msaada ambapo alirejea Jijini Mbeya anakoishi na Binamu yake.
  
Binti huyo anayesomeshwa na Shirika la Under the SameSun  iliyoko Jijini Dar Es Salaam aliwaambia waandishi wa habari kuhusu mkasa uliompata huku akiomba msaada kwa wasamaria wema kumtafutia Shule ili aendelee na masomo kwa ajili ya kujiandaa na mtihani wa kidato cha nne Mwakani.
  
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya HollyWood Ambukeghe Mtafya, alipopigiwa simu kuhusu tuhumahizo alikiri kulijua suala hilo na kwamba walimrudisha mwanafunzi huyo nyumbani ili kumnusuru na kipigo kutoka kwa wanafunzi wenzie na kuongeza kuwa aliambiwa atafute shule nyingine ili ahamie.
  
Naye katibu wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya, Wiliamu Simwale  alisema alikuwa  halijui suala hilo na kwamba kama lingekuwa suala liko nyeti angejulishwa yeye juu ya hatua zilizofikiwa ambapo Uongozi wa Shule umeendelea kupokea fedha za malipo ya Mwanafunzi pasipo kutoa taarifa kwenye shirika linalolipa.

Monday, May 6, 2013

BLOGGERS TULIVYOJIACHIA NA TIGO NEW AFRICA HOTEL

Baadhi ya wamiliki wa Mitandao ya Kijamii (BLOGGERS), wakishindana kucheza muziki kuwania Ipad na simu wakati wa hafla waliyoandaliwa na Kampuni ya Tigo jana kwenye Hoteli ya New Africa, Dar es Salaam.
Mmiliki wa Kajuna Blog, akikabidhiwa zawadi ya IPAD, na Ofisa wa Biashara  na masoko wa Tigo, Gaudance Mushi (kulia)  baada ya kuwa mshindi wa kwanza wa kucheza muziki katika hafla hiyo.
Blogger mwanamke aliyeshinda kucheza muziki akipatiwa zawadi ya Ipad mpya
Mablogger wanawake wakishindana kucheza muziki katika hafla hiyo
Mmiliki wa Blogu ya Kamanda wa Matukio, Kamanda Richard Mwaikenda (aliyevaa shati la drafti kushoto) akiwa na mabloga wenzake wakishuhudia mpambano huo
 Mablogger, Kutoka kushoto ni Adam Mzee (CCM Blog), William Malecela (Wananchi Blog) na John Bukuku wa Fullshangwe Blog wakiwa na furaha wakati wa hafla hiyo.
 Mhariri wa gazeti la Michezo la StaaSpoti, Julius Kihampa (kushoto) akiwa na John Kitime (katikati) pamoja na
 Mmiliki wa Blog ya Habari Mseto, Francis Dande (katikati) akiwa na mablogger wengine.
 Mablogger wakibadilishana mawazo pamoja na maofisa wa Tigo
 Tanzanite Band ikitumbuiza katika hafla hiyo ya kukata na shoka
 Mablogger wakisikiliza wakati mtoa mada Raymond Maganga akielezea jinsi ya kuboresha Blog kibiashara
 Boss wa kampuni ya DeSiaMore I.T & Arts, Raymond Maganga (kushoto), akitoa mada ya jinsi ya kuboresha Blog.
Boss wa kampuni ya DeSiaMore I.T & Arts, Raymond Maganga (kushoto) na Emmanuel Feruz ambaye ni Google Student Ambassador wa IFM, wakifurahia jambo wakati wa hafla hiyo.
                                    Akina dada mablogger wakishindana kucheza muziki


 Blogger wa kike akipatiwa zawadi ya simu baada ya kuwa mshindi wa pili
Mablogger wanaume wakishindana vikali kucheza muziki kuwania zawadi za IPAD na Simu

Sunday, May 5, 2013

NANCY MOSHI NDIYE REDD'S MISS ARUSHA CITY CENTRE 2013


Redd’S Miss Arusha City Centre 2013, Nancy Moshi akipunga mkono mara baada ya kutawazwa mshindi wa Taji hilo katika shindano lililofanyika Usiku wa kuamkia jana jijini Arusha. Nancy aliwashinda warembo wenzake 10 waliokuwa wakiwania nae taji hilo.

Redd’S Miss Arusha City Centre 2013, Nancy Moshi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Glory Steven (kushoto) na mshindi wa tatu Neema Kessy mara baada ya warembo hao kutangazwa kuwa ndio washindi wa shindano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia jana jijini Arusha.

Warembo wanaliokuwa wakiwania taji la Redd’s Miss Arusha City Centre 2013 wakicheza show ya ufunguzi wa shindano hilo jijini Arusha usiku wa Kuamkia leo.
 Wadau mbalimbali wa sanaa ya Urembo mjini Arusha wakifuatilia Onesho hilo la Redd's Miss Arusha 2013.
Mwandaaji wa shindano hilo Bi Upendo (kulia) na rafiki yake.
 Warembo walimfanyia tukio la kipekee Mwandaaji wao kwa Keki ya Birthday, na hapa Upendo akizima mishumaa hiyo...
 Warembo wa tano kati ya 11 waliokuwa wanawania taji la Redd’s Miss Arusha City Centre 2013 wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutangwaza kufuzu hatua hiyo. Kutoka kushoto ni Minael Anderson, Neema Joel, Nancy Moshi, Neema Kessy na Glory Steven.
Mwana dada Rachel ndiye aliyekuwa msanii kinara wa show hiyo na hapa akicheza na mashabiki wake.

Friday, May 3, 2013

REDD'S MISS KIBAHA WAENDELEA KUJIFUA

Mkufunzi wa Warembo wa Miss Kibaha Rehema Uzuwiya akizungumza na warembo hawo wakati wa mazoezi yao yanayo endelea katika ukumbi wa Vijana Kinondoni 
Warembo wa miss kibaha wakiwa katika pozi wakati wa mazoezi yao
Warembo watakao wania taji la Miss Kibaha wakiwa katika pozi wakati wa mazoezi yao yanayoendelea katika ukumbi wa vijana Kinondoni Dar es salaam. Picha

Tuesday, April 30, 2013

REDD'S MISS NYAMAGANA 2013 NDIO HABARI YA JIJINI MWANZA

Kumekucha...Redds Miss Nyamagana 2013 mchakato umeanza...shindano kufanyika Jumamosi ya tarehe...11/05/2013 JB Belmont Hotel Mwanza..Show nzima Itasimamiwa na mchekeshaji Zembwela..huku burudani ikikamilishwa na Recho kutoka THT. Warembo Zaidi ya 20 watapanda jukwani...wakiwa na hamu sio tu kulichukua taji la Miss Nyamagana lakini pia Taji la Miss Tanzania 2013/14. Tiketi zitauzwa mapema, wahi tiketi yako..kwani ni chache mno!! Karibu.

Sunday, April 28, 2013

ASNATH KUTOKA CHUO KIKUU MZUMBE ATWAA TAJI LA REDD'S MISS HIGHER LEARNING MOROGORO 2013

Mshindi wa Shindano la Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro, Anitha Mwakitwange kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe akipunga mkono mara baada ya kuvikwa taji hilo usiku wa kuamkia jana katika shindano lililofanyika Mjini Morogoro. Anitha aliwashinda warembo wenzake 10 aliokuwa akiwania nao taji hilo.
 
Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro, Anitha Mwakitwange(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Rosemary Aloyce (kulia) na Mshindi wa Tatu Tarchisic Mtui mara baada ya warembo hao kutawazwa kuwa ndio washindi wa Shindano hilo usiku wa kuamkia jana katika shindano lililofanyika Mjini Morogoro. Anitha ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe aliwashinda warembo wenzake 10 aliokuwa akiwania nao taji hilo.


 Majaji wa shindano hilo wakiwa tayari katika meza yao kusubiri washiriki wa Redd's Miss Higher Learning Morogoro kupanda jukwaani kuwania taji hilo.
 Mashabiki na wapenzi wa Sanaa ya Urembo kutoka Mkoa wa Morogoro na wengi wao wakiwa ni wanafunzi kutoka Vyuo vya Mzumbe, SUA, Jordan, St Joseph na MSJ wakisubiri kuanza kwa shindano hilo la Redd's Miss Higher Learning 2013.



Washiriki wa shindano la  Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro wakicheza show ya ufunguzi wa shindano hilo lilifanyika usiku wa kuamkia jana na kushirikisha warembo 11 kutoka vyuo mbalimbali vya elimu ya Juu mkoani humo.
 Mwakilishi wa Kamati ya Miss Tanzania ambaye ni Afisa Habari wa Kamati hiyo, Hidan Rico akizungumza machache.
 Huyu alibuni vazi lake kwa Kitenge na makaratasi.
 Huyu alitumia Majani ya mti wa Muashock...
 Kiroba nacho kilichukua nafasi yake kwa mrembo huyu ....
 Miss Higher Learning yeye aliamua kutumia majani ya maua kutengeneza kauni lake maridani la ubunifu.
 Wapenzi wa sanaa ya urembo wakifuatilia kwa umakini onesho hilo.
 Msanii chipukizi wa Mkoa wa Morogoro, ambaye ni mwanafunzi wa Chuo cha St Joseph ajulikanae kama Jose alitumbuiza..
 Ulifika wasaa wa kivazi cha Ufukweni na kila mmoja alienda Mindu kuogelea kwa kivazi chake...
 Huyu aliingia hivi katika maji...
 Huyu alivaa hivi...
 Ilikuwa ni raha kwa mashabiki usiku huo ndani ya Savoy mjini Morogoro...
 Miss Tanzania namba Eugenia mbili nae alikuwepo kushuhudia shindano hilo

 Ilikuwa ni shangwe kwa wapenzi na mashabiki wa sanaa ya urembo Morogoro hasa meza hii ya Mzumbe ambayo ilishajua wazi kuwa taji ni lao mapemaaa...
 Vazi la usiku lilipita na kisha tano bora ikatangazwa...


Warembo waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora ya Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja maara baada ya kutwajwa wakati wa shindano hilo lilifanyika usiku wa kuamkia jana na kushirikisha warembo 11 kutoka vyuo mbalimbali vya elimu ya Juu mkoani humo. Kutoka kushoto ni Tarchisic Mtui, Rosmary Aloyce,Hellen Mhando, Tausi Idd na Asnath Mwakitwange. 
 Washiriki wote ndio hawa hapa...
 Mzee wa Magube Gube!! Barnaba Boy aliwapagawisha vilivyo wapenzi wa sanaa ya urembo hasa wanafunzi hawa kutoka vyuo mbalimbali vya Elimu ya Juu Mkoani Morogoro.  
Walijiachia vilivyoo...katika sho hiyo kali