Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Thursday, June 27, 2013

MISS KANDA YA NYANDA ZA JUU 2013 KUPATIKANA JUMAMOSI HII



Kinyang’anyiro cha kumpata Miss Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kinatarajiwa kufanyika kesho katika ukumbi wa Mikutano wa Mtenda SunSet uliopo Soweto Jijini Mbeya. Mratibu wa Shindano hilo Fredy Herbet, amesema baada ya warimbwende kutoka Mikoa yote inayounda Kanda kukaa kambini tangu Juni 25, Mwaka huu na kupata mafunzo mbali mbali wanatarajia kuivunja Juni 29, Mwaka huu baada ya Msindi kupatikana. Ameongeza kuwa Shindano hilo limeandaliwa na Lake Victoria Arts & Culture Promotion chini ya Udhamini wa TBL kupitia kinywaji chake cha REDDS, SBC kupitia Mountain Dew, Man Company, My Choice Botique, Ebony Fm na Bomba Fm radio. Amesema kinyang’anyiro hicho kitasindikizwa na burudani kutoka kwa bendi ya FM Academia ya Jijini Dar Es Salaam na kuongeza kuwa kiingilio kitakuwa shilingi 10,000/= kwa watu wa kawaida na 25,000/= kwa VIP. Amewataja washiriki wanaong’ang’ania kuibuka kidedea kwa kuiwakilisha Kanda katika shindano la kumpata Miss Tanzania Mikoa wanakotoka kwenye mabano na namba aliyoshinda Mkoani kwake kuwa ni pamoja na Lina J. Allan (Rukwa 1), Aneth B Mapugilo(Mbeya 2), Jesca Mikambi(Katavi 2), Nuru Baraka ( Katavi 1) na Neema Mality (Iringa 1). Wengine ni Lucy George (Iringa 3), Nuriath Suleiman (Njombe 1), Evamary Gamba( Rukwa 2) Lilian Samson (Iringa 2), Naba Magambo (Mbeya 4), Jacklin J Luvanda (Mbeya 1) na Winfrida Felix Miss Njombe namba 2. Kwa Upande wake Mwalimu wa Walimbwende hao Naomi Jones ambaye ndiye anayeshikilia taji hilo amesema kambi iko vizuri na washiriki wote wanafuata maelekezo vizuri hivyo Majaji wawe makini kumtafuta Msindi kutokana na wote kuwa na sifa zinazofanana.
Na:Mbeya yetu

RAIS OBAMA ATUA SENEGAL KWAAA ZIARA YA AFRIKA


Rais Barack Obama amewasili Senegal katika ziara yake ya wiki moja barani Afrika na anatarajia kuzuru Afrika Kusini na Tanzania akilenga kustawisha demokrasia na masuala ya uchumi.
Hii ni ziara ya pili ya Obama barani Afrika tangu achaguliwe Rais mwaka 2008.
Hata hivyo ziara yake inatarajiwa kufifishwa na hali mbaya ya afya inayomkabili aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela. Ikulu ya white house imesema kuwa itategemea uamuzi wa familia ya Bwana Mandela iwapo Rais Obama anaweza kumtembelea hospitalini.
Katika mkutano wake wa leo na rais wa nchi hiyo, Mackey Sall, Rais Obama anatajiriwa kuipa heko Senegal kwa rekodi yake nzuri ya uthabiti ikizingatiwa iko kwenya kanda yenya misukosuko ya kisiasa.
Maafisa wa Marekani wanasema kuwa muhimu katika ziara ya Obama ni kustawisha demokarsia na nchi zote tatu anazotembelea ziko na demokasria thabiti.
Ni ziara ya pili ya Obama katika bara la Afrika tangu kuwa rais wa Marekani mwaka 2008.

WIL.I.AM AGOTA KWA PHARRELL WILLIAM




Will.i.am has filed suit against Pharrell over his i am OTHER brand. According to the Black Eyed Peas member and Black Jetsons lookalike, he owns the copyright to the phrase “I AM” and that Pharrell’s logo is “confusingly similar.”
You know, that sounds petty as hell so since that’s the theme of the matter let me just say I’m siding with Pharrell because his music is better, he’s more attractive, and he’s way less embarrassing on national television when in mixed company.
That said, feel free to formulate your own opinion based on more information of the suit

TLC WAACHIA NGOMA"WATERFALLS" BILA LEFT EYE


"Waterfalls" without Lisa "Left Eye" Lopes' iconic verse? 
Sounds like blasphemy, right? Don't tell that to Chilli and T-Boz, the two living members of TLC.

Left Eye's family is upset with Chilli and T-Boz after a new version of the group's iconic song was released. The new version replaces Lisa with Japanese pop star Namie Amuro.
Liza's sister, Reigndrop Lopes — yes, that’s her real name — talked to TMZ about the record, and she revealed her disappointment:

WEMA SEPETU AZUA KASHESHE NYUMBANI KWAKE BAADA YA KUKUTA UHARIBIFU KWA GARI YAKE



STAA wa filamu za Kibongo asiyekaukiwa vimbwanga, Wema Isaac Sepetu amezua bonge la timbwili kwa wafanyakazi wake wa ndani wa kiume na kike akiwemo mlinzi, Amani linakuletea kisa na mkasa.
Tukio hilo lililonaswa na vifaa vyetu vya kisasa vya kunasia matukio ya mnato na video, lilijiri juzikati nyumbani kwa mwanadada huyo, Kijitonyama, jijini Dar na kusababisha majirani kufaidi sinema ya bure ya matusi ya nguoni.


Ilikuwa majira ya asubuhi ambapo Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006/07, akiwa ametinga dela, nywele bandia nyekundu na miwani nyeusi, alikuwa amejiandaa kwa ajili ya mtoko lakini alipoingia kwenye gari lake aina ya Toyota Lexus Harrier ndipo akagundua tatizo.



Cha kwanza alichogundua ni kwamba gari hilo lilikuwa limeibiwa power window (mashine ya kushusha na kupandisha kioo) zote.
Cha pili ni kwamba alipopiga ‘stati’ gari hilo lilikataa kuwaka kutokana na kuchokonolewa kwenye betri.

SHILOLE AMTIMUA MDOGO WAKE BAADA YA KUDUNGWA MIMBA


STAA wa sinema za Kibongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ (pichani) amemtimua mdogo wake aliyekuwa akiishi naye aitwaye Mary baada ya kunasa ujauzito.
Chanzo makini kilicho karibu na staa huyo kimepenyeza habari kuwa, Shilole alifikia maamuzi hayo baada ya kumuonya binti huyo aachane na mwanaume aliyemjaza mimba hiyo lakini hakusikia hivyo akaona bora amtimue.
 
“Kamtimua baada ya kumuonya mara nyingi bila mafanikio akaona isiwe tabu bora aepuke aibu,” kilisema chanzo hicho.

Alipoulizwa kuhusiana na ishu hiyo, mdogo huyo wa Shilole alikiri kutimuliwa na sasa amehamishia makazi kwa jamaa yake anayefahamika kwa jina la Tonny Montensi anayeishi Sinza, jijini Dar.

WATANZANIA WAISHIO MIKOANI WAPIGWA MARUFUKU KWENDA DAR WAKATI WA ZIARA YA RAIS OBAMA

Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe amewashauri watu walioko mikoani kusitisha safari za kuja Dar es Salaam wakati wa ziara ya Rais wa Marekani, Barrack Obama kutokana na wingi wa wageni katika jiji hilo.
Ugeni huo pamoja na ule wa viongozi kumi na moja kutoka nchi mbalimbali duniani watakaohudhuria mkutano wa kimataifa wa Smart Partnership utakaofunguliwa kesho na Rais Jakaya Kikwete kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, umesababisha kuimarishwa kwa ulinzi katika maeneo mbalimbali hasa katika hoteli za kitalii ambazo zimeanza utaratibu wa upekuzi kwa wageni wake.
Akizungumza na katika mahojiano na Redio ya Clouds jana, Membe alisema jiji limefurika kwa wingi wa wageni. 
“Hoteli na nyumba za wageni zimefurika wageni na magari mengi yamekodiwa. Kwa ujumla, huduma za kijamii zitakuwa shida,” alisema. 
Rais Obama na mkewe Michelle watawasili nchini Jumatatu na tayari wapambe na maofisa usalama kutokana Marekani wameanza kuwasili. Mbali ya ujio huo, wake wa marais kutoka nchi 14 za Afrika watakaokutana na Laura Bush, mke wa Rais wa zamani wa Marekani, George Bush. Pia Michelle atahudhuria mkutano huo utakaofanyika Jumanne na Jumatano ijayo.
“Jiji la Dar es Salaam litakuwa na mambo mengi kwa hiyo wale wenye kuja kutaka kustarehe wafute safari zao,” alisema na kuongeza: “Kama kuna watu ambao hawapo Dar es Salaam na hawana sababu za kuja mjini waache tu mpaka wageni watakapoondoka kwa sababu jiji la litakuwa limejaa na baadhi ya barabara zitachukuliwa zitumike na wageni hao.”
Alisema katika kipindi cha siku tano zijazo, baadhi ya barabara za Jiji la Dar es Salaam zitakuwa na shughuli nyingi na nyingine zitalazimika kufungwa. Barabara itakayofungwa ni pamoja na ile ya Mwai Kibaki na ile ya Bagamoyo itakuwa na shughuli nyingi pia wakati Michelle atakapokwenda Jumba la Makumbusho, Jumanne ijayo.
Wasafiri wa mikoani
Wasafiri wa mikoani wataathirika zaidi Jumanne ijayo wakati Rais Obama atakapokwenda kutembelea mitambo ya kufua umeme ya Kampuni ya Symbion Ubungo.
Kituo hicho kipo Barabara ya Morogoro, ambayo ndiyo inayotumiwa na magari yanayoingia na kutoka mikoani.
Rais Obama atakwenda katika kituo hicho yapata saa 4.00 asubuhi na kwa kiasi kikubwa itaathiri magari ya usafirishaji wa mizigo na abiria yatakayokuwa yanatoka na kuingia Dar es Salaam kabla na wakati huo.

Wednesday, June 26, 2013

ATEKETEZA NYUMBA KUKIWA NA WATOTO WA JIRANI KISA MAPENZI.


MWANAMKE mmoja anayefahamika kwa jina la Taraji Muenzi, 31, mkazi wa kijiji cha Mwatasi, wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, anashikiliwa na jeshi la Polisi mkoani humo kwa kosa la kuichoma nyumba ya jirani yake na kuwateketeza watoto wawili waliokuwa ndani mwake pamoja na vitu vyote katika nyumba hiyo kwa kilichoelezwa wivu wa mapenzi.

Habari kutoka mkoani humo zinasema watoto walioteketezwa wakiwa ndani ya nyuma hiyo ni Faraji, 6 na Jacob, 3 ambao walikuwa watoto pekee wa Subira Kisitu aliyekuwa akituhumiwa na mtuhumiwa huyo kuwa anatembea na mumewe.

Inaelezwa kuwa Taraji kwa muda mrefu alikuwa akimtuhumu jirani yake kumuibia mume na kumchimba mkwara kwamba atamfanyizia, kiasi cha uongozi wa eneo lao kuitisha kikao na kumtwanga faini ya Sh 10,000 aliotakiwa kuilipa juzi, Juni 22 siku aliyofanya tukio hilo.Inaelezwa uongozi wa kitongoji hicho kiliamua kumtoza faini baada ya wiki iliyopita kumvamia jirani yake nyumbani kwake na kumwagia mboga na kusisitiza kuwa kuna kitu atakachomfanyia ambacho hatasahau maishani kama siyo kwa kumuua kwa sumu basi kwa kumchomea moto nyumba yake.

Hata hivyo inaelezwa kuwa jana juzi usiku akiamini kuwa jirani yake yupo ndani na wanawe aliamua kuichoma moto nyumba hiyo, ila kwa bahati mbaya jirani zake alikuwa klabuni akipata kinywaji na hivyo watoto pekee waliokuwa wamelala ndani ndiyo waliougua na kufa pamoja na mali zote.

Kamanda wa Polisi wa Iringa, Ramadhani Mungi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza wanamshikilia mwanamke huyo ili kumfikisha mahakamani kwa kitendo alichokmifanya ambacho kimeacha gumzo kijiji cha Mwatasi, huku familia ya watoto ikiwa katika majonzi makubwa ya kupoteza watoto wao.
chanzo:.

WAANDISHI WA HABARI WAWEKA KAMBI KARIBU NA HOSPITALI ALIKOLAZWA NELSON MANDELA


Rais mstaafu wa Afrika Kusini NELSON MANDERA bado anahali mbaya ingawa bado madaktari yana pigania uhai wake baada ya afya yake kuzorota mwishoni mwa wiki......Richa ya hivyo imeonekana kuwa watu wamepoteza matumaini na kujiandaa kwa loloye ambolo linaweza kutokea mda wowote.
Waandishi na vyombo vya habari viko karibu kabisa na hospitali hiyo kusubiri lolote litakalotokea .

ZANTEL YAZINDUA HUDUMA YA DAKTARI KWENYE SIMU YA MKONONI

Mkuu wa Kitengo cha Rasirimali Watu cha Zantel, Francis Kiaga akifafanua jambo wakati wa ushirikiano na Kampuni ya BR Solution na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ili kuwawezesha watanzania kupata huduma ya ‘Daktari kwa njia ya simu’ ikiwa na lengo la kupata ushauri kwa masaa 24 mahali popote nchini. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa BR Solutions, Richard Toba na Ofisa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan. (Picha na Habari Mseto Blog)
Mkurugenzi Mkuu wa BR Solutions, Richard Toba (kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
 Ofisa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan.
Dk. Aidan Njau akifafanua jambo, Sajid Khan. 

KAMPUNI ya Simu za Mkononi ya Zantel imezindua ushirikiano na Kampuni ya BR Solution na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ili kuwawezesha watanzania kupata huduma ya ‘Daktari kwa njia ya simu’ ikiwa ni kupata ushauri kwa masaa 24 mahali popote nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Zantel jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa Kitengo cha Rasirimali watu cha Zantel Francis Kiaga alisema, wameamua kuingia ubia na Wizara pamoja na BR ili kuwasaidia watumiaji wa Zantel kuongea moja kwa moja na madaktari endapo watakuwa na tatizo linalowasumbua ambalo wanahitaji ushauri.

“Huduma hii ya ‘Daktari kwa njia ya simu’ sisi kama Zantel tunaimani itawanufahisha watanzania kupata ushahuri kwa bei laisi juu ya matatizo yanayowasumbua na ndio maana tumeamua kubolesha maisha ya wateja wetu kwa teknolojia ya simu za mikononi kwa kuwa tunatambua Watanzania wengi wanatumia simu,”alisema Kiaga.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa BR Solution Francis Njau alisema, huduma hiyo itashughulikia magonjwa kama, Ukimbi, Cancer, Moyo, Malaria, Afya ya Uzazi na huduma ya kwanza ambayo bado wanajipanga zaidi jinsi ya kuwafahamisha watanzania jinsi ya kufanya tofauti na kumwelekeza mgonjwa kwenda duka la madawa bila ya kwenda hospitalini kwanza.

“Tukumbuke Zantel walishawahi kushinda tuzo za ubunifu katika kutumia teknolojia katika kubolesha afya na huduma kupitia huduma yake ya Mobile Baby katika tuzo la kongamano la Makampuni ya simu mwaka jana,”alisema.

Kwa upande wa Daktari Aidan Njau wa Aghakan Hospitali alisema, wamejipanga kuhakikisha wanawapa ushauri mzuri watanzania ambao watapiga simu au kutuma meseji ambayo itatangazwa hapo badae na kudai kuwa huduma hiyo itakuwa sio kumpata dawa mgonjwa kwa kuwa fani yao hairuhusu kumpa mgonjwa dawa bila ya kumpima.

“Katika kipengele cha huduma ya kwanza kuna ushahuri ambao tutamwambia mgonjwa atakapopiga simu, ila kumwambia tumie dawa ni ngumu kwa kuwa mtu anaweza kupiga simu anasema anaumwa kichwa ukamwambia tumie Diklofenak alafu kumbe ana vidonda vya tumbo ambapo ni hatari zaidi,”alisemaTumaini.

MASTAA WA KIKE WAKATA MAUNO KUFUNDWA KWA NATASHA

Baadhi ya waalikwa wakijiachia pamoja na Natasha (kushoto) wakati wa sherehe

HUKU siku za kufunga ndoa zikihesabika, mkongwe kwenye filamu za Kibongo, Suzan Lewis ‘Natasha’ amefanyiwa sherehe ya kufundwa kabla ya kwenda kwa mumewe ambayo huko mitaani inajulikana zaidi kwa jina la singo.Shughuli hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, Tandika Maghorofani, Dar ambapo iliandaliwa na shostito wa Natasha aliyejulikana kwa jina moja la Nuru.

APEWA SOMO
Natasha aliwekwa ndani kwa muda wa saa moja akipewa somo la ndoa na watu maalumu walioandaliwa kwa ajili ya shughuli hiyo kabla ya kutoka nje kuungana na wageni waalikwa.
Alipotoka nje, alikutana na waalikwa ambapo kati yao ni mastaa mbalimbali Bongo kisha wakaungana kwenye zoezi zima la kucheza ngoma.
KIASILI ZAIDI
Waalikwa walipata nafasi ya kupakwa urembo mbalimbali wa kiasili usoni na kuifanya hafla hiyo iwe ya kipekee kutokana na vivutio hivyo.
Baada ya yote hayo kukamilika, msafara wa kuelekea nyumbani kwa Natasha, Yombo ulianza huku ngoma zikiendelea kupigwa na mastaa mbalimbali wakikata mauno ndani ya gari.
Akizungumzia shughuli hiyo, Natasha alisema: “Nashukuru sana jamani kwa kupita hatua hii ya kwanza kuelekea kwenye ndoa yangu. Siwezi kuacha kumshukuru zaidi rafiki yangu Nuru kwa kunifanikishia.”

Tuesday, June 25, 2013

SUGU ATIWA MBARONI NA KUACHIWA KWA SHUTUMA ZA KUMTUKANA MH.PINDA

Kw habari zilizotufikia hivi sasa zinadai kuwa Mbunge wa Mbeya mjini Mh Joseph Mbilinyi amekamatwa na jeshi la polisi kwa kile kinachodaiwa ni uchochezi na kumkashifu Waziri Mkuu Mzengo Pinda.  
Hivi  karibuni, Mh. Sugu  alidai  kuwa  Tanzania  haijawahi  kuwa  na  waziri  mkuu  mpumbavu  kama  Mizengo  pinda.
 NEW:
Sugu alikamatwa na kupelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Dodoma na baada ya kuhojiwa aliachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuripoti kituoni hapo kesho asubuhi kwa mahojiano mengine.

BARNABA AZIRAI KATIKA MAZIKO YA MAMA YAKE MZAZI


Msanii Barnaba akiwa amezirai baada ya kuona maiti ya mama yake mzazi.

Baada ya kuzinduka akisaidiwa kuingia kwenye gari kuwaishwa Hospitali.Barnaba alifiwa na mama yake mzazi.

WATOTO YATIMA WA NGEZE EDUCATION CENTER KUJUMUIKA NA WATOTO WENZAO KATIKA MICHEZO YA WATOTO TAMASHA LA RAHA ZA JANA NA LEO

 Watoto yatima wa kituo cha Ngeze education center kilichopo maeneo ya kinondoni kwa  msisiri watajumuika na watoto wenzao katika tamasha la Raha za jana na leo linalojumuisha burudani ya bendi za muziki wa dansi.

Wasanii nguli wa filamu na bongoflava wanaokubalika kwa watoto watakuepo kula,kuimba na kucheza na watoto wote watakaodhulia katika tamasha hilo amabapo kiingilio kwa watoto wadogo kitakuwa ni bure ambapo wazazi wao watalipa kiasi cha tshs 8,000 tu.

Jumla ya bendi sita zitapanda jukwaani moja kuonyesha ukali wake,pia zile nyimbo mpya kutoka katika bendi hizo utazisikia zikipigwa live,bendi hizo ni Twanga Pepeta"African Stars",Mashujaa musica Band ikiongozwa na Chalz baba " wazee wa tuzo tano",Bantu group ikiongozwa na   ikiongozwa na "komandoo Hamza kalala".

Bendi zingine ni King kikii"wazee sugu",OTTU jazz band"MSONDO",King Kikii "wazee sugu" na DDC Mlimani park "SIKINDE" tamasha hilo linatarajiwa kufanyika tarehe 6 mwezi wa saba katika viwanja vya posta vilivyopo kijitonyama jijini Dar es salaam.

 Milamgo ya viwanja hivyo itafunguliwa saa tano asubuhi ambapo michezo ya watoto itaanza na kuisha saa kumi na mbili jioni ambapo burdani za bendi zikiendelea mpaka usiku wa manane.

MISS KANDA YA MASHARIKI 2013 KURINDIMA JUNE 29

aaaaaaa

MASHINDANO ya Redds Miss Kanda ya Mashariki yatafanyika Juni 29 Nashera Hotel mkoani Morogoro kwa kushirikisha jumla ya warembo 14.
Mkurugenzi wa kampuni ya Nikalex Ltd, Alex Nikitas aliwataja warembo hao ambapo wapo kambini hotel ya Starwing Hotel chini ya mkufunzi, Kudra Lupatu kuwa ni Muzne Abduly (19), Ummy Mohamed (21), Sabra Islam (19) na Diana Laizer ambao wote wanatoka Morogoro.
Warembo ambao wanatoka Mtwara kwa mujibu wa Nikitas ni Ivony Stephen (22), Purkeriah Ndovi (21), Zulfa Semboja (19) na wa Lindi ni Janeth Awet (19), Zainab Shaaban (23) na  Sophia Mganga (21). Wanaotoka mkoa wa Pwani ni Elizabeth Perty (22), Suleiyah  Abdi (22)  na Easther Albert (20).
Nikitas alisema kuwa maandalizi ya mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Redds Original, Dodoma Wine, CXC Africa, Nyumbani Park, Usambara Safari Lodge, Michuzi Blog, Clouds Media Group, Chilakale Resorts, Nashera Hotel, Starwing Lodge, Simple car Rental, Big Solution na Mikocheni Resort Centre yamekwisha kamilika na warembo watatembelea sehemu mbali mbali mkoa wa Morogoro na kufanya kazi za jamii.
“Tumejiandaa vziuri na warembo kwa sasa wapo kambini wakijifua kwa ajili ya shindano hilo, warembo watatu wataiwakilisha kanda hiyo katika mashindano ya Redds Miss Tanzania ambayo yatafanyika mwezi Septemba,” alisema Nikitas.
Alisema kuwa wamejipanga vilivyo kwa ajili ya mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kuwa na ushindani mkali kutoka kwa warembo wote.

MWANAMKE ALIOLEWA NA WANAUME WAWILI HUYU HAPA


MWANAMKE mkazi wa kijiji cha Ikandamoyo, wilayani Katavi, Veronica Saleh ‘Mama Kaela’ (50), amefanya uamuzi adimu wa kuolewa na wanaume wawili ambao anaishi nao kijijini hapo.
Kijiji hicho kipo umbali wa takribani kilometa 30 kutoka mjini hapa katika Jimbo la Katavi linalowakilishwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Pamoja na ndoa hiyo iliyowezeshwa na mume mkubwa kukubali kuishi na mume mdogo, imeelezwa kuwa mwanamke huyo ndiye ‘aliyewaoa’ wanaume hao kwa zaidi ya miaka saba sasa, huku akiwa na amri kuu katika nyumba, kama ilivyo katika ndoa za kawaida.
Wanaume hao ni Paulo Sabuni ‘Baba Kaela’ (60) ambaye ndiye mume mkubwa na Arcado Mlele (45) ambaye ni mume mdogo.
Taarifa za kuwapo kwa ndoa hiyo ya aina yake, ziliifikia Globu ya Jamii na kufanyiwa uchunguzi kwa zaidi ya wiki tatu, na hatimaye katikati ya wiki hii, wahusika walikubali wao wenyewe kuzungumzia suala hilo. Kwa mujibu wa maelezo ya mwanamke huyo ambaye alionekana kuwa msemaji wa familia hiyo, yeye na mumewe mkubwa, walifika kijijini hapo miaka 24 iliyopita, wakitoka kijiji cha Usumbwa mpakani mwa Chunya, Mbeya na Tabora.
Wakiwa kijijini hapo mume wake aliendelea kufanya kazi ya ukulima wakati yeye mama (Veronica), pamoja na kilimo hujihusisha na upishi na uuzaji wa pombe ya kienyeji iitwayo kayoga.
 
Mwanamke huyo ambaye amesema ana watoto wanne, Alfred (20), binti mwenye miaka 16 (ambaye ameolewa) na wengine wawili wa kiume, mmoja akisoma darasa la sita na mdogo ana miaka saba, amesema hana shida na waume wake.
 
Ingawa wanandoa hao walizungumza kwa hadhari, majirani walikiri kuwa mwanamke huyo anaishi na wanaume hao wawili kwa amani na kwamba mwanamke huyo ndiye mwenye sauti na si waume zake.
 
“Si siri tena sasa, tumeshawazoea, kwani wanaishi kwa amani ila yule mume mdogo anaishi kwenye nyumba aliyoachiwa na marehemu baba yake, lakini anashinda kwa mume mkubwa, ambapo inajulikana kijijini hapa kuwa ni nyumba kubwa. “Basi pale ni mambo yote, kula na kunywa, mama huyu amewapangia zamu wanaume hao kama afanyavyo mume mwenye wake wengi. 
 
Ama kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni,” alisema mkazi mmoja kwa masharti ya jina lake kutoandikwa gazetini. Ilielezwa, kwamba wanaume hao wana akili timamu na hawatumii kilevi cha pombe kama ilivyo kwa mke wao.
 
Hata hivyo, mume mkubwa anapewa sifa za upole tofauti na mume mdogo anayetajwa kuwa mkorofi kiasi cha mara kadhaa kumchapa makofi mkewe anapomuudhi.
 
Majirani wanadai kwamba Mama Kaela na mumewe Paulo, walipofika kijijini hapo, walipokewa na kuishi maisha ya kawaida, lakini baadaye mama huyo alianza kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Arcado, ambaye naye alilazimika kuachana na mkewe wa ndoa anayefahamika kijijini hapo kwa jina la Mama Pere.
 
Ilielezwa na mashuhuda hao kwamba mume mkubwa alipobaini uhusiano huo, alikuja juu, lakini mwanamke huyo inadaiwa alimweleza mumewe huyo, atake asitake lazima wataishi wawili, vinginevyo ataachana naye, ndipo mume mkubwa alipokubali kuishi na mume mwenza.
 
Katika maisha ya kawaida katika familia hiyo, inaelezwa kwamba katika baadhi ya siku ikitokea kuwa mama huyo amechoka kupika, mume mdogo huchukua jukumu la kupika na kumwandalia chakula na maji ya kuoga mume mkubwa.
 
“Lakini mara nyingi kwa mfano, ikiwa ni zamu ya mama huyo kulala kwa mumewe mkubwa, basi humfulia nguo zake kisha anakwenda kwa mumewe mdogo nako anamfulia nguo. 
MICHUZI BLOG

BBA: NANDO(TZ) NA SELLY(GHANA) WATUPA MBICHI KIDEONI

Mshiriki wa  kiume   wa  Tanzania, Nando  ametutia  aibu  baada  ya  uvumilivu  kumshinda  na  kuamua  kufanya  tendo la  ngono  hadharani  akiwa  katika  jumba  la  big  brother....

Kamera  za  BBA zinamuonesha  wazi  Nando  akikata  mauno  kwa  mwanadada  Selly wa  Ghana  mithili  ya  mtu  ambaye  hajawahi  fanya  tendo  hilo  kwa  miaka  200  iliyopita

Monday, June 24, 2013

JOYCE KILIA AANDAMANA NA WATOTO KUMTAFUTA MUMEWE ALIKO

4
Mtangazaji wa televisheni ya Chanel 5 EATV Joyce Kiria akiwa amewashikilia watoto wake Lingatone Kileo kulia na Lincorn wakati alipozungumza na waandishi wa habari katika mtaa wa Samora na kupaza sauti kuomba msaada
kwa Rais Jakaya Kikwete na watanzania kwa ujumla ili kusaidiwa na kujua aliko mume wake Henry Kileo ambaye inadaiwa amepelekwa Igunga akituhumiwa na kesi huko Joyce Kiria amesema mpaka sasa hajaambiwa kama mume wake yuko wapi hivyo hata kama ana makosa anaomba afahamishwe kwani hajui kinachoendelea mpaka sasa

Joyce Kiria akifafanua mambo mbalimbali mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam huku akiwa amewabeba watoto wake na ndugu zake wengine wakiwa na mambongo yenye ujumbe mbalimbali

Joyce Kiria akendelea kujibu maswali kadhaa ya wanahabari wakati akizungumza nao leo jijini dar es salaam. Na bukuku

ZITO KABWE - TUNAJIANDAA KUIPINDUA NCHI ENDAPO....!!


Zitto  Kabwe  amefunguka  na  kudai  kuwa  kwa  sasa  wanajiandaa  kufanya  mapinduzi  ya  nchi  endapo   watu  walioficha    mabilioni  uswiswi    hawatashughulikiwa  ipasavyo....

Suala la baadhi ya Watanzania kuhifadhi mabilioni ya fedha nchini Uswisi limechukua sura mpya, baada ya tume maalumu kuwahoji vigogo 200 wakiwamo wabunge, wanasiasa na wafanyabiashara.
  
Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa tume hiyo inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema tayari imeshafanya kazi hiyo kwa miezi miwili sasa.
 
Tume hiyo maalumu iliyoundwa na Serikali kwa Azimio la Bunge lililotolewa mwishoni mwa mwaka jana, inatarajiwa kukamilisha uchunguzi huo wakati wowote kuanzia sasa na kuwasilisha ripoti hiyo katika kikao kijacho cha Bunge.

Zitto  Kabwe  anatoa  angalizo  katika  hatua  hiyo  ya jaji Werema   kwa  kusema  kuwa  hatua  hii  isiwe  "zima  moto"   na  daganya  toto  ili  kuwafumba  macho  watanzania...

Ubabaishaji  wowote  kwa  mujibu  wa  Zitto  Kabwe  utasababisha  mapinduzi  ya  nchi.....

Hii  ni  post  yake   twitter

MIMBA YA DIAMOND KWA PENNY YADAIWA KUCHOMOKA

TAARIFA ya ndani zinazodai kwamba, mimba ya mchumba wa Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nassibu Abdul ‘Diamond’, Peniel Mgilwa ‘Penny’ imechoropoka zimevuja....

Kwa mujibu wa chanzo makini kilichojitambulisha kwa jina la wifi 10 cha jijini Dar hivi sasa  hana ujauzito tena kama wengi wanavyodhani.
 
“Penny hana mimba jamani, yupo fiti kabisa na sidhani hata kama anatarajia kushika ujauzito leo wala kesho,” kilisema chanzo hicho.

Hata hivyo, wifi huyo alisema kwamba awali kulikuwa na dalili zilizoonesha kwamba Penny alikuwa ni mjamzito kutokana na mtangazaji huyo kutumia vitu vichachu kama vile maembe na mara kwa mara alikuwa akiumwa hadi kufikia kulazwa hospitali.
Inadaiwa kwamba Penny alipotoka hospitali alionekana kuwa fiti zaidi na hakuwa na dalili zozote za kuwa na ujauzito kama ilivyokuwa siku za nyuma.
Baada ya kupata habari hizo, mwandishig wetu alilimpigia simu Penny ili kuthibitisha madai hayo:

Mwandishi: Mambo vipi, Penny pole sana.
Penny: Pole ya nini sasa?

Mwandishi: Si nimesikia kwamba unaumwa jamani na ukakumbwa na mkasa mwingine? 
Penny: Mkasa gani huo unaousema maana mimi niko fiti tu.

Mwandishi: Nilisikia kwamba baada ya kuumwa na kulazwa hopsitali mimba yako ikatoka?
 
Penny: (Kimya kwa dakika 3) Asante ni mipango ya Mungu.

Mwandishi: Sasa unatarajia lini utapata tena mimba nyingine? 
Penny :(Kwachuuuuuu). Simu ilikatwa na hata ilipokuwa ikipigwa tena haikuwa ikipokelewa.
GPL