Pages

Pages

Tuesday, October 26, 2010


Meneja udhamini wa Vodacom Tanzania, Rukia Mtingwa akiwaonyesha waandishi wa habari magari 30 kati ya 100 yanayotolewa kwa washindi wanaoshiriki shindano la shinda Mkoko linaloendeshwa na kampuni hiyo tangia tarehe 2 mwezi wa nane na mpaka sasa magari yamebaki 15 yakiwa tayari kwa kunyakuliwa na mteja yeyote Yule wa Vodacom Tanzania.
Magari aina ya Hyundai i10 yanayotolewa kwa washindi wa shindano la Shinda Mkoko linaloendeshwa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania yakipita chini ya bango la kampuni hiyo lenye ujumbe Habari ndiyo hii katika makutano ya barabara za Kawawa na Uhuru ya Ilala Boma leo.
Miongoni mwa magari hayo yapatayo 30 ambayo yamehifadhiwa katika ghala la kampuni ya kuuza magari ya FK Motors leo yalipitishwa katika maeneo mbalimbali jijini ili kuwaonyesha wananchi juu ya uhakika wa shindano hilo la Shinda Mkoko kutoka Vodacom Tanzania ambalo linaendeshwa kila siku na mshindi kujishinda gari moja la Hyundai I10 kila siku.
Jumla ya magari matatu yameshatolewa kwa washindi wa shindano hilo kutoka mkoani Dar es salaam, Dodoma na Ruvuma na magari mengine yataendelea kutolewa kwa washindi kwa utaratibu uliopangwa na Vodacom Tanzania ambapo kwa sasa taratibu mbalimbali za usajili wa magari hayo zinaendelea
Magari aina ya Hyundai I10 yanayotolewa na kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania katika shindano lake la kila siku la Shinda Mkoko yakiwa katika msururu wakati yalipokuwa yakipelekwa katika maegesho yaliyopo kwenye kampuni ya kuuza magari ya FK Motors iliyopo barabara ya Nyerere.
 

No comments:

Post a Comment