Pages

Pages

Sunday, October 31, 2010

...

CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO CHATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI

CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kinatoa pole kwa klabu ya Simba na wanamichezo wote hapa nchini katika kuomboleza kifo cha kocha mahiri Syllersaid Mziray.
TASWA imeshtushwa taarifa za kifo cha Mziray, hivyo tunatoa pole kwa familia ya kocha huyo na wanamichezo wengine katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mwanamichezo huyo mahiri.
Mziray atakumbukwa na waandishi wa habari za michezo kutokana na ukaribu wake na alikuwa na ushirikiano wa kutosha pale alipoombwa kufanya hivyo.
TASWA inamkumbuka zaidi Mziray kwani mara kadhaa alipata kushiriki kwa kufundisha kwenye semina ambazo ziliandaliwa na chama chetu ama na watu wengine kwa ajili ya waandishi wetu.
Tunaomba wanamichezo tumuenzi Mziray kwa masuala mbalimbali aliyokuwa akiyatilia mkazo ikiwemo kusimamia ukweli kwa kile alichokiamini na ndio maana tunasema tutaendelea kumkumbuka daima.
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA

No comments:

Post a Comment