Pages

Pages

Thursday, October 28, 2010

KANUMBA,MIRIAM GERALD NA ALI LEMTULAH KUWA MAJAJI KATIKA GIRAFFE UNIQUE MODEL 2010
   Mkurugenzi wa Unique  Entertainment Methuselah Magese ametangaza jopo la majaji ambao wameteuliwa na  kampuni hiyo  kuwa majaji katika hatua ya uchujaji na fainali kwa ujumla.
    Akiyataja majina hayo kuwa ni steven kanumba,Miriam Gerald,victoria martine na mbunifu mahili Ali lemtulah ambao watapata semina maalumu ya kuwanoa kabla ya kuanza kwa duru kubwa la kumsaka mwanamitindo mwenye sifa za kipekee.
     Aidha Bwana Magese aliitaja kamati ya yake ni  ya watu watatu ambapo meneja mradi ni Britney Urasa (miss Temeke  namba mbili), meneja utawala Michael Maulus(mhariri wa gazeti la Jambo) na Methuselah Magese ambaye ni mkurugenzi wa mashindano haya.
       Tunawashukuru wadhamini wote waliojitokeza na wanaoendelea kujitikeza katika shindano la  GIRAFFE UNIQUE MODEL 2010 ambapo inategemewa kuleta mapinduzi makubwa ya sanaa ya mitindo nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment