Pages

Pages

Sunday, October 31, 2010

..

KASORO ZAJITOKEZA UCHAGUZI 2010 MWANZA.

KWA UKOSEFU WA VITI NA MEZA MAWAKALA NA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI KWA BAADHI YA VITUO KAMA KITUO HIKI CHA UVUVI IGOGO MWANZA WALITOA HUDUMA KATIKA MAZINGIRA MAGUMU. WAUNGWANA WANAHOJI JE ILIKUWA SI MBINU KUCHELEWESHA ZOEZI?

VYUMBA HEWAENEO HILI LILIKUWA NA VYUMBA 11 CHA AJABU NI KUWA VYUMBA 7 TU NDIVYO VILIKUWA VIKITENDA KAZI.

PICHANI UPIGAJI KURA UKIENDELEA MAWAKALA NA WASIMAMIZI WAKIWA WAMEKALIA MAWE KUJISITIRI, KASHESHE ILIKUWA WAKATI WA KUGONGA MIHURI KWENYE KARATASI ZA KUPIGIA KURA.

KWENYE MOJA YA VYUMBA VYA KUPIGIA KURA HADI INATUMU SAA NNE NA DAKIKA ZAKE MAJIRA YA ASUBUHI HAKUNA ALIYEPIGA KURA KWA KUKOSEKANA KWA SANDUKU LA KUWEKEA KURA ZA MBUNGE HALI ILIYOLETA TAFRANI KUBWA.

ASKARI WALITIA TIMU KITUO CHA UVUVI IGOGO ILI KUTULIZA GHASIA NAKUFANIKIWA KUMTIA NGUVUNI KWA MUDA MWENYEKITI WA ENEO HILO AMBAE ALISADIKIKA KUVUNJA KANUNI KWA KUWASHAWISHI WATU WALIOKUWA WAKIFIKA KUPIGA KURA KUELEKEZA KURA ZAO KWA WAGOMBEA CHAMA FULANI.

KITUO CHA MIRONGO NI NI MOJA YA VITUO AMBAVYO VILIPIGA KURA AINA MBILI TU YAANI YA URAISI NA UBUNGE ILE YA 3 YA UDIWANI HAWAKUPIGA, SABABU ZIKITAJWA KUWA NI KUCHELEWA KWA KARATASI ZA UDIWANI (KIUFUPI HAZIKUJA KABISAA). BAADAE WANANCHI WALIPEWA MAELEZO TOKA KWA WASIMAMIZI UPIGAJI KURA UKAENDELEA, HIVYO KURA HIZO KUMCHAGUA DIWANI WAO WATAPIGA BAADA YA MIEZI MITATU(MWEZI JANUARY 2011).

HUMU JOTO BALAA HAKUNA MAJI YA KUNYWA, WASIMAMIZI NA MAWAKALA WALIKUWA WAKIOMBA MUDA UISHE JIONI IFIKE.

No comments:

Post a Comment