Pages

Pages

Sunday, October 31, 2010

breaking news.....

RATTIBA YA GIRAFFE UNIQUE MODEL 2010 (season one)  KUTANGAZWA

   Miriam Gerald moja ya majaji wa Giraffe unique model 2010
 
  Ratiba ya shindano la mitindo nchini Tanzania lijulikanalo kama Girrafe unique model 2010 imetangazwa leo jumapili na mkurugenzi wa Unique Entertainment Bwana Methuselah Magese.
   Magese amesema jumatatu ya tarehe 1  novemba kutakuwa na mkutano wa waandishi wa habari katika hafla fupi ya ufunguzi wa Shindani hilo katika hoteli ya Giraffe ocean view iliyopo Dar es salaam.
   Tarehe 20 Novemba utafanyika mchujo wa wanamitindo katika ukumbi wa Jet 1 uliomo ndani ya Hoteli ya Giaffe ambapo majaji watachuja na kupata wanamitindo kumi tu ambao watabahatika kuingia moja kwa moja kwenye kinyang'anyiro cha kumsaka mwanamitindo mwenye sifa za kipekee.
   Desemba 1 kutakuwa na mkutano mkubwa wa waandishi wa habari palepale Giraffe hotel kuhusu kuwatangaza washiriki rasmi walioteuliwa na majaji,pia itakuwa ni siku ya kuwangaza wadhamini rasmi wa shindano hilo ambayo itaambatana na utangazaji wa zawadi kwa Mshindi na washiriki wengine.
   Aidha Bwana Magese aliongeza kuwa kambi ya washiriki itaanza Desemba 13 katika Hoteli ya Giraffe ambapo wakuwa mazoezini chini ya matroni na mwalimu wa catwalk model hidaya.
   Fainali za Giraffe unique model zitakuwa usiku wa mkesha wa krismasi Desemba 24 katika hoteli ya Giraffe ambapo show itaanza mishale ya saa mbili usiku.
  Wakati huo huo wadhamini wawili wameongezeka ikiwa ni lubiarac paints na Gazeti la Jambo Leo.

No comments:

Post a Comment