Pages

Pages

Tuesday, November 2, 2010

MGOMBEA WA CHADEMA AZIRAI BAADA YA KUTANGAZWA USHINDI

  Haya ni baadhi ya maumivu na kutoamini baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi ambako kulimpelekea mgombea kuzimia ...ni hatari jamani inauma sana


HATIMAYE Chama cha Mapinduzi (CCM) kimefanikiwa kutwaa jimbo la Tarime ambalo lilikuwa likishikiliwa na chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa miaka mitano,huku mgombea wa CHADEMA, Mwita Mwikwabe akiangua kilio hadi kuzirai. Mgombea huyo alizirai baada ya matokeo kuhesabiwa tena na kubaini kuwa ameshindwa ,ambapo mgombea wa CCM, ambaye ni mtunzi wa vitabu, Nyabari Nyangwine,amefanikiwa kushinda kwa tafauti ya kura 730.
Akitangaza mataokeo hayo msimamizi mkuu wa uchaguzi jimbo la Tarime, Fedelis Lumato,alisema kuwa Mgombea wa CCM,Nyambari Nyangwine ameshinda kwa kura 28,064 huku mgombea wa Chadema Mwita Mwikwabe akipata kura 27334 ambapo aliyekuwa anatetea kiti hicho Charles Mwera wa CUF akiambulia kura 7368.
Lumato alisema kuwa mgombea wa NCCR-Mageuzi ,Peter Wangwe amepata kura 7811,mgombea wa UDP, Mchungaji Jacob Mwita ameambulia kura 185 akifuatiwa na mgombea wa TLP ambaye ni mwandishi wa habari na Mwanasheria Kichere Nyaronyo aliyepata kura 45 tu.
Aidha CCM imefanikiwa kutwaa halmashauri hiyo baada ya kupata madiwani 17 dhidi ya Chadema waliopata madiwani 12 na CUF wakiambulia kiti kimoja kutoka kwa aliyekuwa mbunge wa Jimbo hilo Mwera aliyepewa aliyepata kujifariji.
Kwa upande wa matokeo ya Rais Mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete, amepata kura 34930 sawa na asilimia 49 dhidi ya Mgombea wa Chadema 32470 sawa na asilimia 46 huku akifuatiwa na mgombea wa CUF aliyepata kura 1804 na mgombea wa APPT-Maendeleo Piter Kuga Maziray akiambulia kura 889sawa na asilimia 1.3.

Asilimia 42.5 ya wapiga kura katika jimbo la Tarime ambao walijitokeza kupiga kura katika jimbo lenye wapiga kura 160867 ambapo waliojitokeza ni 70907 jambo ambalo msimamizi wa jimbo hilo alisema inahitaji utafiti kwasababu katika miaka ya hivi karibuni wapigakura wamezidi kukosa muamko.
Hata hivyo licha ya kwamba CCM wameshinda shamrashamra zao ni za mashakamashaka kwani watu waliojitokeza kusherekea ni wachache walionekana hawajiamini kama wameshinda jimbo hili ambalo wamefanya kazi ya ziada na ngumu na hatimiye kufanikisha ushindi huo. Pamoja na zoezi hilo kumalizika hali ilikuwa tete tangu usiku wa kuamkia jana baada ya milio ya mabomu na risasi kusikika sehemu mbali mbali hadi jana mchama ambapo polisi walikuwa wanafanya kazi ya kutawanya makundi ya vijana wanadaiwa kuwa ni wafuasi wa CHADEMA waliokuwa wakiandama kupinga matokeo.

No comments:

Post a Comment