Pages

Pages

Wednesday, November 3, 2010

VICTORIA MARTIN APENYA MCHUJO WA SWAHILI FASHION WEEK 2010


Male Models waiting to audition at the model casting at the Southern Sun Hotel,victoria martin mwanamitindo maarufu nchini Tanzania amepita katika mchujo huo ni kazi na umuhimu wake atauwakilisha katika Giraffe unique model 2010 kama jaji mwanamitindo. 
                                            Selected Female Models for SFW 2010
Wajasirimali zaidi ya 50 watajumiika pamoja katika kuuza na kuonesha bidhaa za aina mbalimbali wanzozizalisha katika maonesho yanyojulikana kwa jina la Swahili Fashion Week Shopping Festival, maonesho yanayokwenda sambamba na onesho kubwa la mavazi linalowakutanisha wabunifu wa mavazi kutoka nchi za Afrika zinazozungumza lugha ya Kiswahili.
 
Swahili Fashion Week Shopping Festival itafanyika kuazia tarehe 4th hadi 6th ya mwezi wa November 2010 katika bustani ya Karimjee, na kuwashirikisha wajasiriamali kutoka Zanzibar na Tanga, Kirimanjaro, Mtwara na Dar es salaam.
“Hii ni mara ya kwanza kwa Swahili Fashion Week Shopping Festival kufanyika, lengo ni kutoa fursa kwa watu wa aina mbalimbali ambao watafika katika fashion show waweze kupata ladha ya tofauti na maonesho ya mavazi kwa kuona na kununua bidhaa mbalimbali ambazo ni adimu”. pia kuchangia kukuza dhana ya kupenda bidhaa zinazozalishwa Tanzania. Alisema Hamis Omar, Afisa masoko na mauzo wa Swahili Fashion Week.
Katika maonesho kutakuwepo na bidhaa kama vile nguo, mapambo ya aina mbalimba, vifaa vya mapishi, henna na vingine vingi. Maonesho yatakuwa wazi kuanzia asubuhi hadi jioni kwa muda wa siku  tatu, yaani tarehe 4, 5 na 6 ya mwezi huu kwa Novemba 2010.
“Wazo la kufanya maonesho haya limekuja kufuatia tathimini tulioipata mwaka jana, ambopo tuliona kwamba pamoja na kuwepo maonesho yalifanywa na wabunifu wa mavazi ya kuonesha nguo zao,  ambapo watu mbalimbali  waliofika katika maonesho walitaka kununua, ndio maana tukaja na tukio hili ili watu wa aina mbalimbali wawaeze kufurahi na kupata vitu adimu.” Aliongezea Hamis Omar.

No comments:

Post a Comment