Pages

Pages

Monday, January 31, 2011

    TIDO MHANDO KUTUPIWA ZENGWE JINGINE
BAADA ya kung’olewa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando amekumbwa na msukosuko mwingine kutokana na baadhi ya wanachama wa Chama cha Maendeleo Muheza (MDTF) kutaka sekretarieti ya chama hicho kujiuzulu. sasa.
Wanachama hao wametaka sekretarieti hiyo ing’oke kutokana na kudaiwa kushindwa kuleta maendeleo katika kipindi cha miaka miwili, hivyo kuhatarisha uhai wa chama hicho.
Kwa mujibu wa kundi hilo, wanachotaka ni uongozi wote wa sasa kujiuzulu, kwani uongozi uliopita ulifanikiwa kuleta maendeleo ikiwamo ujenzi wa kidato cha sita katika Shule ya Sekondari Muheza, ujenzi wa visima vya maji na Shule ya Sekondari Kelenge.
Walisema kasi ya ukuaji wa chama haionekani tangu kuingia madarakai sekretarieti mpya.
Akizungumzia suala hilo jana jijini Dar es Salaam, msemaji wa chama hicho, Ramadhan Semtawa, alikiri kuwapo kwa mpango huo wa mapinduzi.
“Ni kweli huo mpango wa mapinduzi nimeusikia. Jana nimezungumza na mkurugenzi anasema Tido yuko Uingireza na amepanga tukutane karibuni.
“Ninachosema sekretarieti haijashindwa kazi na sioni sababu ya kujiuzulu. Tunaomba utulivu kwani mipango inatekelezeka. Saccos tayari iko chini ya Mama Semainda ambaye alikuwa Mkurugenzi wa BoT, tawi la Mwanza.
“Tatizo mwaka jana kulikuwa na mambo ya uchaguzi, ila tutajitahidi na Balozi Adad Rajabu yupo kwa sasa atatupa mbinu,” alisema.
Katika sekretarieti cha chama hicho, Tido ni Mwenyekiti, Mary Chipungahelo (Makamu Mwenyekiti), Nehemia Mchechu (Mhazini), Albert Semng’idu (Katibu), Clement Mang’enya (Mkurugenzi Mtendaji) na Ramadhan Semtawa (Katibu Mwenezi).
Sekretarieti hiyo iliingia madarakani baada ya kuondoka uongozi chini ya uenyekiti wa Balozi Adad.
Hata hivyo, Semtawa kwa upande wake, alisema kama shinikizo hilo litaongezeka atajiuzulu kabla ya kutokea kwa mapinduzi.
“Shikinizo likiongezeka nitajiuzulu kabla ya mapinduzi,” alisema Semtawa.


MFANYAKAZI SHUPAVU WA GIRAFFE HOTEL AFARIKI DUNIA
   Mr.Gonzaga (mwenye suti katikati) enzi za uhai wake katika press conference ya uzinduzi wa unique model 2010.kulia kwake ni magese na kushoto kwake ni lehmtulah

Meneja ukumbi na matukio wa hoteli Giraffe ocean view ya jijini Dar es saalam amefarki dunia usiku wa kuamkia jana kwa ajali ya pikipiki,kifo chake kimestua wengi hususani mkurugenzi wa hoteli Bwana Charles Bekoni na wafanyakazi wa Giraffe hoteli.
  UNIQUE eNTERTAINMENT imesikitishwa sana na msiba huu kwani Bwana Gonzaga tumekuwa nae sambamba katika mchato mzima wa Unique model.

    MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU GONZAGA
   VURUGU ZA MACHINGA NA POLISI JIJINI MWANZA

JIJI la Mwanza jana lilikumbwa na machafuko baada ya machinga kufanya vurugu na kuandamana wakipinga kuondolewa kufanya biashara katika maeneo ya mjini kati. Vurugu hizo zilisababisha kufungwa kwa maduka katika maeneo mbalimbali mjini hapa, kuvunjwa vioo vya magari, maduka na baadhi ya barabara kutopitika kwa muda huku kituo kidogo cha Polisi Pamba, kikinusurika kuvamiwa na kuchomwa moto.MKUU WA MKOA WA MWANZA ABBAS KANDORO AKIZUNGUMZA NA WAANDAMANAJI HAO KUPITIA GARI LA FFU, KULIA MWENYE SHATI YA BLUE NI MWENYEKITI WA WAMACHINGA MZ.
Pamoja na vurugu hizo, serikali mkoani Mwanza imewataka wafanyabiashara hao kuheshimu sheria na kanuni za mipango miji zilizowekwa pia maafikiano yaliyofikiwa baina ya viongozi wao, uongozi wa mkoa na halmashauri ya jiji hilo .

Vurugu hizo zilizodumu kwa zaidi ya saa sita, zilianza saa tatu asubuhi baada ya mgambo wa jiji na askari wa kutuliza ghasia kuwatawanya wafanyabiashara hao katika maeneo ya Makoroboi, Mission na Soko Kuu. 
Nje ya jengo hilo , waliweka vizuizi vya mawe katika barabara zote zinazoingia jiji na kulazimisha pikipiki na magari yaliyokuwa yakipita kurudi yalikotoka huku wakiwa na chupa za maji ya kunawa kwa ajili ya kujikinga na moshi wa mabomu iwapo polisi wangewafyatulia mabomu ya machozi.
Hali hiyo ilisababisha polisi wa kutuliza ghasia na makachero kuweka ulinzi mkali katika lango kuu la kuingilia jiji hadi viongozi akiwemo Mkurugenzi wa jiji Wilson Kabwe na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro walipofika na kufanya mazungumzo na viongozi wa machinga hao.

Baada ya mazungumzo hayo, Kandoro aliwaambia machinga kuwa hapingani na sheria na kanuni za mipango miji kwa kuruhusu machinga wafanye biashara katika maeneo waliyoruhusiwa, isipokuwa wafuate masharti waliyopewa katika maeneo ya Makoroboi, Mirongo, Vitunguu Soko Kuu na Mlango Mmoja.

AJALI KATIKA PILIKA ZA KUNUSURU BIASHARA.
Baada ya kuondoka katika ofisi za halmashauri hiyo, machinga waliingia mitaani tena na kuanza vurugu wakivamia maduka na kuvunja vioo kwa madai kwa wafanyabishara wengine, hawatafanya biashara.

Sunday, January 30, 2011

VIDOSHO WAZIKIMBIA TATOO KWA DINI YA MASHETANI

 

 Vodosho kadhaa wameanza kuzipotezea tatoo(michoro ya mwilini) kwa kile kinachodaiwa michoro mingi ina alama za dini ya watu wamuabuduye shetani.

Hii imewastua wasichana wengi wa Tanzania ambao walikuwa wanajichora tu mwilini kwa michoro wasioijua ikiwa wao wanafuata tu fasheni mpya ya kujichora bila kujua mchoro huo una maana gani ama asili yake imetoka wapi.hii hatari isiyo na tahadhali kwa wasiojua.

Maandamano yaendelea Misri,watu wazidi kuawa,taasisi zachomwa moto

Maandamano dhidi ya serikali, yameendelea kwa siku ya tano mfululizo mjini Cairo.
Amri ya kutotoka nje ilitangazwa jana usiku katika miji ya Cairo, Alexandria na Suez, baada ya mapambano makali baina ya polisi na waandamanaji.
Waandamanaji
Waandamanaji mjini Cairo wanataka kiongozi Hosni Mubarak kung'atuka
Hata hivyo, maandamano yameendelea, na jeshi linashika zamu barabarani.
Waandamanaji hasa wamekuwa wakipiga kelele kuwa serikali sio halali, na pia rais Mubarak.
Ni wazi kuwa ahadi aliyotoa rais, kubadili baraza lake la mawaziri na kuleta mabadiliko, hayatoshelezi wananchi.
Wanataraji kuwa, wanaweza kumtoa kiongozi, kama ilivyotokea Tunisia.
Wengi wanasema, baada ya kuishi chini ya sheria ya dharura, inayozuia mkusanyiko wa watu hadharani, sasa wamepata moyo kumiminika barabarani, kutokana na yale yaliyotokea Tunisia.
Watu hawakupata kuonesha nguvu kama hii.
Rais Mubarak amehakikisha kuwa mataifa rafiki ya magharibi yaone kuwa tishio linatoka kwa kundi kubwa la upinzani, la Muslim Brotherhood.
Chama hicho kimepigwa marufuku, na awali kililaumiwa kwa makosa, kuwa kilihusika na maandamano.
Wanaharakati wa kisiasa, wanataka watu wapya wasiohusika na serikali, waruhusiwe kuwania uongozi.
Mohammed El Baradei, aliyewahi kuwa mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Atomiki, ametokeza kuwa kiongozi maarufu wa upinzani.
Lakini wengine wanamtaka Katibu Mkuu wa Jumuiya Nchi za Kiarabu, Jenerali Amr Moussa.


MSINISHANGAE HII NDIYO STAILI YA KUCHAJI IPOD YANGU

marisa_miller4MALLISA MILLER:moja ya wanamitindo maarufu wenye vituko kadhaa waakdhaa


            MH EDWARD LOWASA ATOBOA UKWELI

MBUNGE wa Monduli na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amelitaka taifa kujipanga kukabiliana na tatizo kubwa la ukosefu wa ajira ya vijana ili kuepuka maafa kama yale yanayotokea sasa katika nchi za Tunisia na Misri.
Lowassa, aliyekuwa akihutubia wakati wa mahafali ya kwanza ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii kilichopo Monduli, alisema wananchi wanapaswa kulijadili tatizo hilo linalozidi kukua kila siku wakati wanapojadili masuala mengine yanayogusa masilahi ya taifa kama Dowans na Katiba.
“Tuzungumze Dowans, tuzungumze Katiba, tuzungumze pia kuhusu tatizo la ajira ya vijana wetu. Ndiyo tunaweza,” alisema Lowassa.
Katika hotuba yake hiyo, Lowassa alitumia maneno yaliyotolewa wiki iliyopita na Rais wa Marekani, Barrack Obama, wakati akihutubia Bunge la nchi hiyo aliposisitiza kuhusu umuhimu wa kutengeneza ajira mpya kwa ajili ya vijana wa taifa hilo kubwa duniani.
“Iwapo nchi kubwa kama Marekani zinaona umuhimu wa kuwekeza katika ukuaji wa ajira, ubora wa ajira na tija ipatikanayo na muono huo, nchi changa kama Tanzania inapaswa kuwa na mikakati mipana zaidi,” alisema Lowassa akisisitiza kuhusu unyeti wa tatizo hilo.
Akifafanua, Lowassa alisema wadau mbalimbali wanapaswa kushirikiana na serikali katika kubuni njia ya kukabiliana na tatizo hilo la ajira ambalo iwapo halitadhibitiwa linaweza kuleta madhara makubwa.
“Sekta zinazoshughulikia tatizo la ukosefu wa ajira zijitahidi kupunguza tatizo hilo kwani ni bomu ambalo likilipuka hakutakuwa na amani na utulivu tulionao hivi sasa. Tuliwahi bomu hili kabla halijalipuka,” alisema.
Alisema pamoja na jitihada za serikali za kutatua tatizo hilo, bado kuna changamoto kubwa katika kuongeza tija za uzalishaji wa ajira hapa nchini.
Alisema hapo zamani takwimu zilikuwa zikionyesha kuwa vijana wengi waliokosa ajira ni wale ambao hawakuwa na elimu lakini hivi sasa mambo ni tofauti, kwani hata wenye elimu nao wamekumbwa.
Alisema ukosefu wa ajira hasa kwa watu wenye elimu ya kukidhi viwango ni hatari kwa taifa na iwapo jitihada za makusudi hazitachukuliwa kutatua hali hiyo, nchi inaweza kuingia katika matatizo makubwa.
“Ndugu zangu wananchi na wahitimu sote tutakumbuka mwaka 2005 CCM, ilitambua ukali wa tatizo hili ikaahidi kutengeneza ajira milioni moja ndani ya miaka mitano. Leo tunapogeuka nyuma na kuangalia namna ahadi na dhamira hiyo ilivyotekelezwa, jibu tunalopata liko wazi, kwamba bado tatizo lipo na ni kubwa,’’ alisema.
Aliongeza kuwa tatizo la jira kwa vijana hapa nchini ni kubwa na linazidi kukua siku hadi siku, hali iliyosababisha kushindwa kufikia malengo ya Mpango ya Kupunguza Umasikini na kukuza Uchumi (Mkukuta), ambayo yalitaka hadi kufikia mwaka jana kuwe kumepungua kwa tatizo hilo hadi kufikia asilimia 6.9.
Lowassa alisema takwimu zilizotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu mwaka 2006 zinaonyesha kuwa hadi wakati huo asilimia 11.7 ya vijana walikuwa hawana ajira ikilinganishwa na ilivyokuwa mwaka 2000 wakati idadi ilikuwa asilimia 13.
Akionyesha namna tatizo hilo lilivyo kubwa, alisema Septemba mwaka 2008, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Ladius Komba, aliwasilisha mada mjini Monrovia nchini Liberia na kunukuliwa akisema wastani wa vijana wasio na ajira mjini unafikia asilimia 16.5 ikilinganishwa na vijijini ambako ni wastani wa asilimia 7.5.
Akiendelea kumnukuu Komba, alisema takwimu hizo zilionyesha hali kuwa mbaya zaidi kwa Jiji la Dar es Salaam ambako idadi ya watu waliokuwa hawana ajira walikuwa ni asilimia 31.5.
Alisema kuwa ni wazi idadi hiyo ni kubwa ambayo inahitajika kutafutiwa ufumbuzi na wadau mbalimbali kabla suala hilo halijalipuka, kwani ni wazi kwamba tukiwa kama taifa tunapaswa kutambua tumekalia bomu linaloweza kulipuka wakati wowote.
Lowassa alitumia fursa hiyo kupinga kuwa hoja zinazotolewa na watu mbalimbali kuwa Tanzania ni nchi maskini na kusisitiza kuwa si maskini bali ni nchi changa kwasababu ina matatizo ya kutumia rasilimali nyingi ilizonazo.
“Nasisitiza sisi si maskini, ni wachanga, tuna utajiri mkubwa sana wa rasilimali bado tunahitaji muono mpana wa jinsi ya kutumia rasilimali hizo kukuza uchumi wa taifa,’’ alisema.
Alisema kuna ushauri mbalimbali uliotolewa na wataalamu ambao unapaswa kufuatwa kwa kubadili mitaala iliyopo ya elimu ili iwe inayomuwezesha muhitimu ajiajiri kulingana na fani aliyoisomea.
Katika mahafali hayo Lowassa aliahidi kutoa msaada wa kompyuta baada ya kusikia changamoto zinazokikabili chuo hicho.
Chuo hicho kilichoanzishwa mwaka 1978 kilipitia katika hatua tofauti kabla ya hivi sasa kugeuzwa na kuwa chuo cha maendeleo ya jamii na kufanya mahafali yake ya kwanza tangu kianze kutoa elimu ya maendeleo ya jamii.
MISS TANZANIA ASHUHUDIA MAKAMUZI YA REDSUN NEW MAISHA CLUB

  Redsun Gwiji la dance hall kutoka nchini Kenya akikamua mbele ya mashabiki wake katika usiku wa Versity Nite ndani ya New Club Maisha ambapo mrembo Geneviva Emanuel alikuemo usiku huo.


BIA ZA BURE ZAMTOKEA PUANI

katika pita pita zangu za Mtaa kwa Mtaa,leo niliibukia mitaa ya Tandale Uzuri na kukutan na kisa hiki ambacho mwanadada huyo aliekaa chini alijikuta akitembezewa kichapo na jamaa mmoja hivi ambaye aliingia mitini.kisa cha kutembezewa kichapo dada huyu,inasemekana ni kwamba alikunywa bia za mshkaji huyo alieingia mitini na kukataa kuondoka nae.hapo ndipo jamaa alipatwa na hasira na kuanza kumuangushia kichapo hicho hadi wasamalia wema walipoanza kukusanyika na kumfanya msela huyo kuingia mitini.hiki ndicho kisa cha Uswahilini leo.

Saturday, January 29, 2011


5 HOTTEST VICTORIA"S SECRET MODELs

1: Heidi Klum

A lot of debate went into this ranking, but when the dust settled we had to name Heidi Klum the hottest Victoria’s Secret model of all time. In all fairness however, any of the top seven would have fit, and I’m sure arguments could be made for many of the other girls in this list. In the end though, it has to be Klum. She’s managed to stay at peak hotness for something like fifteen years now, and for that alone she deserves the top spot.

 2: Laetitia Casta

 mEasily one of the most iconic faces in the history of Victoria’s Secret. Casta has been on the cover of more than 100 magazines and has been featured in Guess, Tommy Hilfiger, and XOXO campaigns.

3: Gisele Bundchen

 

The inspiration for this list, Bundchen has been hot tabloid fodder ever since she started dating Tom Brady. She’s the face of more than 20 brands internationally and is supposedly worth over $150 million. Actually dated Leonardo DiCaprio before hooking up with Tom Brady, which means DiCaprio might be the luckiest bastard on the face of the planet considering he landed Bar Refaeli following Gisele.

4: Alessandra Ambrosio

 Tyra Banks has anointed Ambrosio “The future of the modeling world” and it’s not too tough to see why. Actually had her ears pinned back when she was 11 years old, and has since sworn off plastic surgery after having numerous complications. Has made cameos on Entourage as well as the film Casino Royale. 

5: Adriana Lima

 A Victoria’s Secret angel since 2000, Lima is also well known for being a spokeswoman for Maybelline, as well as her numerous magazine cover appearances.




 WATANZANIA KUSHTAKIWA UINGEREZA
WAMILIKI wa mashine za kuchambua pamba nchini wamefunguliwa kesi katika mahakama ya Usuluhishi ya Pamba iliyoko Liverpool, Uingereza, kutokana na kuporomoka kwa uzalishaji.
Watanzania hao walifikishwa katika mahakama hiyo baada ya zao hilo kuporomoka kwa asilimia 30 katika kipindi cha kilimo cha msimu uliopita wa mwaka 2010 hatua iliyosababisha kushindwa kukusanywa kwa tani 260,000 za zao hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam Mbunge wa Kasulu Mjini Moses Machali (NCCR-Mageuzi) alisema amelazimika kuwasilisha hoja binafsi bungeni kujadili suala hilo.
“Matokea ya kuadimika kwa zao hilo ni kwamba wamiliki wa mashine za kuchambulia pamba wanadaiwa na wanunuzi toka nje na tayari wengi wao wameshashtakiwa kwenye Mahakama ya Usuluhishi wa zao la Pamba Liverpool Uingereza,” alisema Machali.
Machali aliitaka serikali kupitia Wizara ya Kilimo na Chakula kutoa maelezo ya kina juu ya suala hilo ambalo linaweza kuitikisa nchi kama ilivyo kwa sakata la Dowans.
Alisema wamiliki hao wachache waliofikishwa mahakamani wanadaiwa zaidi ya sh bilioni 10 huku kukiwa na uwezekano wa kuongezwa wamiliki zaidi ya 38 jambo ambalo litaigharimu nchi.
Alisema aliwasilisha barua kwa Katibu wa Bunge kutaarifu dhamira aliyonayo kwa ajili ya kuwasilisha hoja binafsi katika Bunge litakaloanza Februari 8 mwaka.
Mbunge huyo alisema kama hoja hiyo haitajadiliwa mapema na kutolewa ufafanuzi kuna hatari kwa wamiliki wote ambao ni zaidi ya 38 kufikishwa kwenye mahakama hiyo na kufilisiwa mali zao jambo ambalo ni hatari kwa uchumi wa taifa.
Alieleza tatizo lingine linaloweza kulikumba taifa ni kwa wakulima wa zao hilo wanaotarajia kulima kutakata tamaa na kuachana nalo hivyo kupunguza kasi ya kukuza pato la ndani.

HUKU NDIKO MTAANI KWATU
 siku hizi ndo staili za kutegana kijiweni
Hizi ni bata  ama laana ...dunia imekwisha!!

.

   WATU 13 WARIPOTIWA KUFA KATIKA VURUGU ZA MAANDAMANO NCHINI MISRI

Mpaa kufikia jana usiku ni zaidi ya watu 1000 walikuwa wamejeruhiwa na zaidi ya watu 13 walikuwa wameripoyiwa kufariki dunia wakati kituo kimoja cha radio kilikuwa kimelipuliwa pamoja na ofisi moja ya chama kinachotawala wakati maeneo mengi ya jimbo la suez yakiwa si shwari
 na mapigano kati ya raia na polisi yakiendelea.

Polisi wamepambana na maelfu ya waandamanaji kwenye mji mkuu wa Misri, Cairo, baada ya sala ya Ijumaa wakitaka Rais Hosni Mubarak ajiuzulu.
Polisi walirusha mabomu ya machozi na kutumia mizinga ya maji kusambaza watu, waliokuwa wakirusha mawe.
Watu hao pia waliandamana katika miji ya Suez na Alexandria.
         polisi wakizuia maandamano nchini misri
Serikali ilisema iko tayari kwa mjadala, lakini pia imeonya kuchukua "hatua madhubuti".
Mawasiliano ya kupata huduma za wavuti na simu za mkononi yamekatizwa.
Kulikuwa na ripoti za kuanza upya kwa mapigano, pamoja na viongozi wa upinzani kukamatwa.
Pia kulikuwa na hatua kali za kinidhamu dhidi ya kundi la kiislamu lililopogwa marufuku, the Muslim Brotherhood, baada ya kusema itaunga mkono maandamano hayo siku ya Ijumaa.
Siku ya Alhamis, mpinzani wa Misri na mshindi wa tuzo ya Nobel Mohamed ElBaradei alirejea Cairo, akiahidi naye kuandamana.
Takriban watu saba wameuawa na takriban 1,000 wamekamatwa tangu maandamanao hayo yalipoanza.
Maandamano hayo yameanza baada ya kuwepo ghasia Tunisia, yaliyosababisha kukimbia kwa Rais Zine al-Abidine Ben Ali.

Friday, January 28, 2011

Naomi campbell atoa tamko

NAOMI CAMPBELL has spoken out about the accusations of perjury levelled at her by her former agent's company. Carole White has accused Campbell of lying on the stand during a civil litigation between her company, Moodform Mission, and the supermodel.

"The allegations are unequivocally denied," Campbell said today. "I am personally saddened that Ms White has chosen to make such a serious and utterly false claim against me, my lawyer and my advisor. We all vehemently deny the allegations. The allegations are completely without merit and should never have been made. We are completely satisfied that the truth will prevail."



. Candice Swanepoel--she look like Asia Dachi(unique model 2010/2011)
candice_swanepoel
New York:
IMG
Copenhagen:
Elite Copenhagen
Barcelona:
Elite Barcelona
Hamburg:
MODELWERK
With her classic good looks and approachable, bombshell next door allure, Candice Swanepoel is a natural choice for Victoria's Secret. The South African beauty has become one of the mega-brand's most visible faces.



WATANZANIA WAFUNGWA JELA ZIMBABWE

SIKU moja baada ya Mtanzania Ahmed Ghailan kuhukumiwa kifungo cha maisha jela nchini Marekani, wengine wawili wamefungwa miaka saba kila mmoja nchini Zimbabwe.
Watanzania, Juma Ally Juma (30) na Masumbuko Abdallah Munguni (38), wamefungwa baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya cocaine kutoka Zambia kuelekea Afrika Kusini wakipitia nchini hapa.
Watanzania hao walikamatwa mwaka jana wakiwa na vidonge hivyo vya cocaine vyenye thamani ya dola za Marekani 203,810 walivyokuwa wamevimeza tumboni.
Walikamatwa wakiwa ndani ya basi wakisafiri kutoka nchini Zambia kupitia Zimbabwe kuelekea nchini Afrika Kusini.
Katika maelezo yao mahakamani wamekaririwa wakisema waliahidiwa pesa dola za Marekani 1000 kila mmoja na mfanyabiashara wa nchini Tanzania waliyemtaja kwa jina moja la Malik.
Wamesema mfanyabiashara Malik angewapa kiasi hicho cha pesa kama wangefanikiwa kusafirisha hadi Afrika ya Kusini.
Taarifa zimeeleza kwamba wawili hao walimeza vidonge hivyo wakiwa nchini Tanzania kwa lengo la kukutana na mwenzao aliyefahamika kwa jina la Francis Williams, ambaye hata hivyo hukumu yake bado haijasomwa nchini Zambia.
Watuhumiwa walichukua usafiri wa basi kutoka Lusaka na kufanikiwa kukatisha mpaka wa Zambia na Zimbabwe bila kukamatwa.
Taarifa hizo zimeongeza kwamba wakiwa safarini mmoja wa watuhumiwa hao alianza kupata maamivu kutokana na moja ya vidonge kupasuka tumboni kabla ya kukamatwa na polisi na kutolewa vidonge 159 kwa wote wawili.
Juzi mahakama ya Jimbo la Manhattan nchini Marekani ilimhukumu Mtanzania, Ahmed Ghailani, kifungo cha maisha gerezani kwa kuhusika na mashambulizi ya kigaidi.
Jopo la majaji lilikaririwa likisema Mtanzania huyo amekutwa na hatia ya kufanya njama ya kuharibu majengo ya serikali.
Jaji katika kesi hiyo Lewis A. Kaplan amesema aliridhishwa na ushahidi aliopata kwamba Ghailani alijua kwamba watu wangekufa kutokana na vitendo vyake.


Lil Kim anatoka na kitu cha Black Friday "MIXTAPE"

Mwanadada Lil Kim anaendeleza beef lake na Nick Minaj…. Alianza na ngoma inayoitwa Black Friday …akaja na Video na sasa ni kitu cha Mixtape…ambayo itatoka siku ya Valentine’s Day. 2/14/11...“Black Friday the mixtape – 2/14/11- WHO THE F*** WAR? #ItsBlackFridayHoe LEGOOOO!!!!! hayo ni maneno ya lil kim alioandika kwenye tweeter. 
      
                 MODEL OF THE WEEK
Photograph shows model Camille McDonald, wearing designs by Ashakai.on carribia fashion week

HAMIS MALIKI WA MSONDO AFARIKI DUNIA

Mwanamziki wa bendi ya msondo ngoma Music ,Hamisi Maliki 'Super Maliki' picha ndogo amefaliki Dunia mwanamziki huyo aliyekuwa akiimba sauti ya kwanza amefaliki katika hospital ya Agrikan Malapa Dar es salaa alfajiri ya kuamkia leo akisumbuliwa na limonia mazishi yatafanyika kesho mwanamziki huyo aliyejiunga na kundi hilo mwanzoni mwa mwaka 2010 alikuwa akiimba nyimbo za sauti ya kwanza

Mandela aruhusiwa kutoka hospitali

Bw Nelson Mandela
Aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela ametolewa hospitali ambapo alikaa kwa siku mbili.
Daktari General Vejaynand Ramlakan alisema Bw Mandela, mwenye umri wa miaka 92, ambaye alikuwa na maradhi mbalimbali yaliyo ya kawaida kwa watu wa umri yake anaendelea uzuri.
Makamu wa Rais Kgalema Motlanthe- akitumia jina lake la ukoo la Bw Mandela-alisema "Madiba anaendelea vizuri."
Siku ya Ijumaa Bw Ramlakan alisema Bw Mandela alipata matatizo ya kupumua, lakini alikuwa akiendelea vizuri na atakuwa anapata matibabu akiwa nyumbani.
Alisafiri kutoka Cape Town hadi Johannesburg siku ya Jumatano kwa kile serikali kilichoita uchunguzi wa "kitaalamu".
Hatua hiyo ilichochea wasiwasi upya juu ya afya dhaifu ya kiongozi huyo.
Marafiki na familia walimtembelea licha ya kuwepo kwa usalama wa hali ya juu siku ya Alhamis.
Afisa mwandamizi wa polisi alisema mfululizo wa magari ulikuwepo nyuma ya eneo la kuingilia katika hospitali ya Milpark mjini Johannesburg, yakijiandaa kumchukua Bw Mandela nyumbani kwake Houghton.
Shujaa huyo wa ukombozi wa Afrika Kusini-anayejulikana miongoni mwa Waafrika Kusini kwa jina lake la ukoo, Madiba- tangu ajiuzulu na masuala ya umma mwaka 2004 ameonekana kuwa dhaifu katika mara chache anazoonekana hadharani.

JIBABA SHOGA MAARUFU NCHINI UGANDA lAUAWA .

Mwanaharakati wa kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja wa Uganda ambaye mwaka jana alilishtaki gazeti lililomtoa kwa jinsia yake hiyo amepigwa mpaka kufa. Polisi wamethibitisha kifo cha David Kato (pichani kulia) na kusema wamemkamata mshukiwa mmoja.
Gazeti la Uganda la Rolling Stone lilichapisha picha za watu kadhaa ambao walisema ni wapenzi wa jinsia moja na huku pembeni kukiwa na kichwa cha habari "WANYONGENI"

Kumekuwa na wimbi la matukio ya "mauaji kutumia chuma" huko Mukono, alipokuwa akiishi Bw Kato, ambapo watu wamekuwa wakiuliwa na vipande vya chuma. Walioshuhudia wanasema kwamba mtu mmoja aliingia nyumbani kwa Bw Kato karibu na Kampala, na kumpiga mpaka kumwuua kabla hakuondoka. Polisi wamesema licha ya kumkamata mshukiwa mmoja, mshukiwa mkuu- ambapo wanasema alikuwa akiishi naye amekimbia.


GAZETI LILILO MWAGA DATA:-Kundi lake liitwalo (Smug) limesema Bw Kato alikuwa akipata vitisho tangu jina, picha na anwani yake kuchapishwa na Rolling Stone mwaka jana. Nae Frank Mugisha, mkurugenzi mtendaji wa kundo hilo, amesema kuwa "ameshtushwa" kupata habari hizo kutoka New York. "Marehemu alikuwa na wasiwasi na vitisho alivyokuwa akivipata hivi karibuni".

Mapenzi ya jinsia moja ni kinyume na sheria Uganda, na adhabu ya miaka 14 jela. Hivi karibuni mbunge mmoja alijaribu kuongeza adhabu kwa kuwepo kwa hukumu ya kifo kwa baadhi ya makosa.

Shirika la kutetea haki za binadamu (HRW) lilitoa wito wa kufanyiwa uchunguzi kwa kifo chake.

TUZO ZA MUZIKI WA INJILI MWEZI WA PILI TAREHE 27

                             Wasanii wa muziki wa kizazi kipya kushoto mwasiti akifuatiwa na prof. Jpamoja na mratibu wa tuzo za injili Halisi Kapiga
          Mwasiti na prof Jize

Thursday, January 27, 2011

JE MTU MNENE ANAWEZA KUWA MWANAMITINDO?

                                        WABONGO MPOOOOOOOOO...!!!!!!!

Adebayor ajiunga Real lMadrid kwa mkopo

Mshambuliaji wa Manchester City Emmanuel Adebayor amejiunga kwa mkopo na klabu ya Real Madrid hadi mwishoni mwa msimu huu.
Emmanuel Adebayor
Emmanuel Adebayor
Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa yaTogo, anatazamiwa kuelekea Hispania siku ya Jumatano kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa afya yake katika klabu hiyo.
Madrid watakuwa na uchaguzi kama watahitaji kumnunua moja kwa moja Adebayor mwenye umri wa miaka 26 mwishoni mwa msimu, wakati mkataba wake wa mkopo utakapomalizika.
Adebayor alijiunga na Manchester City akitokea Arsenal kwa kitita cha paundi milioni 25 mwaka 2009 na ameshafunga mabao 19 katika michezo 36 ya ligi na mashindano mengine katika Manchester City.
Anakuwa mshambuliaji wa pili mwandamizi wa Manchester City kuondoka katika klabu hiyo katika kipindi cha miezi sita, baada ya Robinho kwenda AC Milan na anaonekana atamsaidia meneja wa Real, Jose Mourinho kuziba pengo la mshambuliaji Gonzalo Higuain, anayesumbuliwa na matatizo ya mgongo.
Kabla ya kumtupia jicho Adebayor, Real ilijaribu kumsajili mshambuliaji wa Hamburg, Ruud van Nistelrooy, huku dau lao la paundi milioni 39 likikataliwa kwa kutaka kumchukua mpachika mabao wa Atletico Madrid, anayechezea pia timu ya taifa ya Argentina, Sergio Aguero.
Adebayor ataweza kucheza mashindano ya Ligi ya Ubingwa wa Ulaya na pia ligi ya Hispania, maarufu La Liga, Reala Madrid wakiwa wanashikilia nafasi ya pili, na iwapo mambo yake yatakwenda vizuri huko Bernabeu, anaweza kusaini mkataba wa kudumu kwa dau la uvumi la paundi karibu milioni 15.


MATOKEO KIDATO CHA NNE: Wasichana wang’ara

JUMLA ya watahiniwa 177,021 waliofanya mtihani wa taifa wa Kidato cha Nne Oktoba mwaka jana wamefaulu huku wasichana wanane wakishika nafasi kumi bora kitaifa.
Kwa mujibu wa matokeo hayo, kiwango cha ufaulu kimeporomoka kwa asilimia 22.11 ikilinganishwa na matokeo ya mwaka juzi.
Shule za binafsi hususan seminari zimeendelea kung’ara wakati zile za umma zikifanya vibaya na kushika nafasi za mwisho.
Katika matokeo hayo, wanafunzi wanne wamefutiwa matokeo kutokana na kuandika lugha ya matusi katika mitihani ya masomo ya Biolojia, Historia, Kemia na Jiografia.
Akitangaza matokeo hayo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani, Joyce Ndalichako, alisema shule kumi bora zilizofanya vizuri katika mtihani huo ni zile zilizokuwa na watahiniwa kuanzia 40 na zaidi, ambazo ni Uru Seminari (Kilimanjaro), Marian Wasichana (Pwani), St Francis (Mbeya) na Canossa (Dar es Salaam).
Nyingine ni Msolwa (Morogoro), Feza Wavulana (Dar es Salaam), St Mary Goreti (Kilimanjaro), Abbey (Mtwara), St Joseph’s Iterambogo (Kigoma) na Barbro - Johnson (Dar es Salaam).
Aliwataja wanafunzi walioshika nafasi kumi bora kitaifa kuwa ni Lucylight Mallya, Maria –Dorin Shayo wa Shule ya Wasichana ya Marian, Sherryen Mutoka wa Barbro - Johansson, Diana Matabwa na Neema Kafwimi wa Shule ya Wasichana ya St Francis.
Wengine ni Beatrice Issara wa St Mary Goreti, Johnston Dedani wa Ilboru, Samwel Emmanuel wa Moshi Technical, Bertha Sanga wa Marian na Bernadetha Kalluvya wa St Francis.
Hata hivyo, pamoja na wasichana kung’ara katika nafasi kumi za kwanza kitaifa, bado wavulana wameendelea kufaulu kwa wingi.
“Wasichana waliofaulu ni 69,996 sawa na asilimia 43.47 na wavulana ni 107,025 sawa na asilimia 56.28,” alibainisha Ndalichako.
Alizitaja shule kumi za mwisho kitaifa zilizokuwa na watahiniwa 40 na zaidi kuwa ni Changaa, Kolo, Kikore, Hurui, Thawi, (Dodoma), Pande Darajani (Tanga), Igawa (Morogoro), Makata (Lindi), Mbuyuni na Naputa (Mtwara).
Ndalichako alisema shule kumi bora zilizofanya vizuri kitaifa ambazo zipo katika kundi la watahiniwa chini ya 40 ni pamoja na Don Bosco (Iringa), Feza wasichana (Dar es Salaam), Maua Seminari (Kilimanjaro) na Queen of Apostle Ushirombo (Shinyanga).
Nyingine ni Sengerema Seminari (Mwanza), Sanu Seminari (Manyara), Bethelsabs Wasichana (Iringa), St Joseph –Kilocha Seminari (Iringa), Dungunyi Seminari (Singida) na Mafinga Seminari (Iringa).
“Pia zipo shule za mwisho ambazo zimefanya vibaya zilizokuwa na watahiniwa chini ya 40 kati ya hizo ni Sanje ya mkoani (Morogoro), Daluni (Tanga), Kinangali (Singida), Mtanga (Lindi), Pande (Lindi), Imalampaka (Tabora), Chongoleani (Tanga), Mwamanenge (Shinyanga), Mipingo (Lindi) na Kaoze (Rukwa)”, alisema.
Jumla ya watahiniwa 311 na watahiniwa wawili wa kujitegemea wamefutiwa matokeo yao baada ya kubainika kufanya udanganyifu katika mtihani huo.
“Baraza pia limefuta usajili wa kituo cha watahiniwa wa kujitegemea P1189 cha Biafra kutokana na kukiuka taratibu za uendeshaji mitihani…maana kituo hicho kilikuwa na watahiniwa wengi kuliko uwezo wake, jambo lililosababisha usumbufu,” alisema.
Pia baraza hilo limetangaza kusitisha matokeo ya wanafunzi 1,448 ambao walifanya mitihani bila ya kulipa ada ya mtihani, ambapo watatakiwa kulipa na faini katika kipindi cha miaka miwili ili waweze kupewa matokeo hayo.
“Wanafunzi wawili wamefanya mtihani kwa sifa zinazofanana, hivyo tumesitisha matokeo yao hadi wakuu wa shule hizo watakapowasilisha nyaraka kuthibitisha uhalali,” alieleza.
Ndalichako alisema watahiniwa 35 wa Shule ya Sekondari Bara wamefutiwa matokeo na kuondolewa katika usajili baada ya kutumia majina ya watahiniwa ambao walichaguliwa kujiunga na shule hiyo lakini hawakwenda kuripoti.
Alisema watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani huo kwa mwaka 2010 walikuwa 458,114 wakiwamo wasichana 216,084 sawa na asilimia 47.17 na wavulana 242,030 sawa na asilimia 52.83, ikilinganishwa na mwaka 2009 ambao walikuwa 351,152, hivyo idadi ya watahiniwa imeongezeka kwa watahiniwa 106,962.
“Watahiniwa waliofanya mtihani huo ni 441,426 sawa na asilimia 96.36 na watahiniwa 16,688 hawakufanya mtihani sawa na asilimia 3.64 ya waliosajiliwa,” alifafanua.

Tunisia yataka Ben Ali akamatwe

Tunisia
Waziri wa sheria wa Tunisia amesema nchi hiyo imetoa hatia ya kimataifa ya kukamatwa kwa Rais aliyekimbia Zine al-Abidine Ben Ali na familia yake.
Lazhar Karoui Chebbi alisema Tunisia imeiomba shirika la polisi la kimataifa Interpol kumkamata Ben Ali, aliyekimbilia Saudi Arabia mapema mwezi huu kufuatia maandamano makubwa nchini humo.
Bw Chebbi alisema Bw Ben Ali ashtakiwe kwa wizi wa mali na kuhamisha patoa la taifa la fedha za kigeni.
Aliyasema hayo huku maandamano ya kuipinga serikali yakiendelea.
Mwongoza Watalii Makumbusho ya Kale, Katika Kanisa la Catholic Pwani, Justin Roman Lui, akifafanua jambo na kuwaonyesha namna chumvi inavyopakiwa kwenye mifuko washiriki wa Miss Utalii waliopembelea Mradi wa Chumvi wa Nunge,Bagamoyo Mkoani Pwani leo.
Baadhi ya Washiriki Miss Tourism wakiwekachumvi katika vifurushi, Nunge Bagamoyo Pwani,Wakati wa ziara ya Washiriki hao walipotembelea Mradi wa Chumvi wa Nunge,Bagamoyo Mkoani Pwani leo.
Picha ya Pamoja wa Warembo hao.


Warembo wa Tanapa-Miss Utalii Tanzania 2011, jana walitembelea maeneo mbalimbali ya vivutio vya Utalii ikiwa ni katika mchakato wa kujifunza masuala mbalimbali yanayohusian na Utalii wa Ndani wa Tanzania, katika mkoa wa Pwani Bagamoyo.

Katika matembezi hayo warembo waliweza kujifunza namna Uzalishwaji wa Chumvi unavyotengenezwa kutokana na mabwawa ya maji kutoka bahari ya Hindi(Maji chumvi).

Akizungumzia Mradi huo wa Chumvi, Meneja wa Mradi, Nicolaus Meliha, alisema kuwa Chumvi hiyo inatengenezwa kutokana na mabwawa yatokanayo na maji chumvi yanayopatikana kutoka bahari ya Hindi.

“kiujumla mradi wetu huu ndiyo unaozalisha chumvi nyingi hapa nchini pamoja na kwamba pia zipo sehemu zingine kama Mikoa ya Lindi na Zanziba, lakini hapa kwetu chumvi zaidi ya tani mia kwa wiki huku soko la ajira kwa wakazi wa mkoa wakiendelea kunufaika na mradi huu, ila kwenu washiriki wa shindano hili mkiwa kama mabarozi mnapaswa kuutangaza kama moja ya kivutio cha Utalii kutokana na kwamba upo maeneo ya kale ya kihistoria”alisema Meliha

Na kuongeza kwamba hadi chumvi inapatikana inatokana na kukaushwa kwa maji chumvi yatokanayo na maji ya bahari ya hindi, ikiwa ni baada ya kukaa eneo moja lisilorusu maji kutoka na pia inategemeana sana na jua ili maji kukauka ba baada ya hapo chumvi upatikana.

Fainali za mwaka huu zitarushwa moja kwa moja (live) na kituo bora kabisa cha runinga StarTV cha jijini Mwanza. Zitafanyika Februari 5, 2011 ambapo wasichana zaidi ya arobaini watakuwa wakimsaka mmoja anayestahili kuvikwa taji la umalkia wa taifa wa Utalii nchini ambaye pamoja na kuwa balozi wa kimataifa wa utalii wetu pia atapata mkataba wenye thamani ya shilingi milioni mia moja na hamsini.

Kambi ya warembo hawa iliyopo hoteli ya Kiromo View Resort, imekuwa gumzo kubwa la jiji la Dar sasa kutokana na ukweli kuwa, utulivu, umakini na madhari ya hoteli hii vimekuwa kielelezo tosha cha kufanya ushindani uwe mkubwa miongoni mwa washiriki ambapo pia watawania tuzo (awards) zingine zaidi ya ishirini na nane zitakazowawezesha kushiriki mashindano mengine ya kimataifa na kuwakilisha mikoa au maeneo yao vema.

Kauli mbiu ya mashindano ya Miss Utalii mwaka huu ni “Ewe Mtanzania tembelea na tangaza hifadhi za taifa, utalii ni maisha na utamaduni uhai” ambayo kimsingi ndicho kielelezo yakini cha shindano kikilenga kuhamasisha utalii wa ndani miongoni mwa Watanzania ambaio wengi wao hawajui kabisa maana vivutio vya kitalii na kitamaduni vilivyopo nchini.

Hoteli ya Kiromo ambako Shindano hili litafanyika ni ya kitalii na yenye hadhi ya nyota tatu na iko umbali wa kilometa kumi tu toka mjini Bagamoyo. Kadhalika, inatoa Huduma zote za kisasa kwa umakini na ustadi mkubwa.

Aidha, wadhamini wakuu wa shindano ni Kiromo View Resort na Sahara Media Group inayomiliki kituo cha runinga cha StarTV, Radio Free Africa, Kiss FM na gazeti la Msanii Afrika.
 

Tuesday, January 25, 2011

Uwanja wa ndege mjini Moscow walipuliwa

Uwanja wa ndege wa Domodedovo wa Moscow umetikisika baada ya kutokea mlipuko wa bomu ambapo msemaji wa uwanja huo alisema watu 35 wamefariki dunia.
Zaidi ya watu 100 wamejeruhiwa- 20 wakiwa katika hali mbaya sana kutokana na mlipuko huo, ambapo ripoti zinasema shambulio hilo limefanywa na mtu aliyejitoa mhanga.
Mchunguzi mkuu wa Urusi alisema magaidi ndio wamehusika na shambulio hilo.
Uwanja huo, ambao una shughuli nyingi katika mji mkuu wa Urusi, upo kilomita 40 kusini-mashariki mwa mji huo.
Urusi
Mwathirika wa mlipuko wa bomu, Moscow
Rais Dmitry Medvedev alisema waliohusika na shambulio hilo watasakwa mpaka wapatikane.
Ameamuru kuwepo na usalama zaidi kwenye mji mkuu, kwenye viwanja vya ndege na vituo vengine vya usafiri, na pia ameitisha mkutano wa dharura na maafisa waandamizi.
Pia imebidi kuahirisha safari yake ya kuhudhuria mkutano wa uchumi duniani huko Davos.
Mwandishi wa usalama wa BBC Gordon Corera alisema mashaka moja kwa moja yataelekezwa kwa wapiganaji kutoka mji wa Caucasus.
Corera alisema, wapiganaji wanaopambana Caucasus wanajua namna mwonekano wa Rais na waziri mkuu wa kuwa na jamii salama ilivyo muhimu kwao, na hivyo kuutikisa usalama huo ni lengo lao kuu.
Mwezi Machi mwaka jana mfumo wa treni za chini ya ardhi kwenye mji mkuu wa Urusi ulitikiswa na wanawake wawili waliojitoa mhanga kutoka mji wa Dagestan, na kusababisha vifo vya watu 40 na kujeruhi zaidi ya 80.


              FASHION MODEL
Izable Goulart is one of Victoria’s Secret beautiful models.  This Brazilian beauty seems to be in love with Victoria’s Secret new Bare Bronze Body-Perfecting Spray Tint: “I like to tan all year long, so this sexy tint is my new best beauty friend.”
Izabel Goulart
Brazilian Model-Izabel Goulart.
Sexy, radiant skin is always in! Introducing two new ways to get glowing with an all-over body bronzer and shimmering fragrance mist. Both are part of the new Victoria’s Secret Bare Bronze Collection of glowing bronzers, daily glow moisturizers and makeup. The perfect way to capture a sexy sun-kissed glow all year long.


WAGE AKILI KUMPA RUSHWA JERY MURRO 

SHAHIDI wa pili upande wa Jamhuri katika kesi ya kuomba rushwa ya sh milioni 10 inayomkabili aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la (TBC1) Jerry Murro, na wenzake Michael Wage amekiri kutoa rushwa ya sh milioni moja baada ya kutishiwa bastola na pingu.
Wage alitoa maelezo hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Gabriel Mirumbe wakati akiongozwa na Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Boniface Stanslaus.
Alidai kuwa alilazimika kutoa rushwa hiyo kwa sababu alitishwa na Murro na mshtakiwa wa pili Kapama aliyejitambulisha kuwa ni Kaimu Mkurugenzi wa PCCB na mshtakiwa wa tatu Deo Mgassa alijitambulisha kuwa ni msaidizi wa mkurugenzi huyo.
Shahidi huyo ambaye alikuwa mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kabla ya hajasimamishwa kazi na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Januari mwaka jana, alidai kuwa washtakiwa hao wote watatu Januari 31 mwaka jana, katika Hoteli ya Sea Cliff walimtaka awapatie sh milioni 10 ama sivyo wangembambikia kesi kama alivyobambikiwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu, Amatus Liyumba, kwa kumwambukiza maradhi mpenzi wa rafiki wa Kapama ndiyo maana akabambikiziwa kesi iliyomfanya ahukumiwe kwenda jela miaka miwili.
Wage aliieleza Mahakama kuwa Januari 28 mwaka jana akiwa nyumbani kwake Bagamoyo alipokea simu kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kuwa mtangazaji wa TBC1 na hakuwa hakimfahamu, akimtaka kesho yake aje Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano kwani amepata taarifa kuwa anakabiliwa na tuhuma za ufisadi katika Halmashauri ya Bagamoyo.
Katika hilo Wage alieleza kuwa alikubaliana na ombi hilo na Januari 29 mwaka jana, saa tano asubuhi alifikia katika mgahawa wa Califonia ulioko jijini hapa akiwa na dereva wake.
Alisema akiwa njiani alimpigia simu Murro ili aje aungane naye na baada ya dakika chache Murro aliwasili katika mgahawa huo akiwa na gari ndogo na akamweleza watafute meza nyingine ili wakae mbali na dereva wake na walipohamia kwenye meza nyingine ndipo Murro alipoanza kumueleza tuhuma za ufisadi zinazomkabili na kwamba anataka kuzitangaza kwenye kipindi cha Usiku wa Habari kinachorushwa na TBC1.
“Baada ya Murro kunieleza tuhuma hizo akaniambia mahojiano kamili yangefanyika katika Hoteli ya Sea Cliff kwani huko ndiko walikokuwa mabosi wake na kunitaka nimwache dereva wangu kwenye mgahawa huo nikapande gari lake twende nae Sea Cliff na nilifanya kama alivyonielekeza nikapanda na tulipokuwa njiani akampigia simu mtu akawa anazungumza naye na akanitaja jina langu… alivyokata simu nikamuuliza ni kwa nini alikuwa akitaja jina langu akasema alikuwa akizungumza na Kaimu Mkurugenzi wa PCCB (Kapama) naye pia atanihoji.
“Kitu kingine wakati nilipokuwa ndani ya gari hilo tukielekea Sea Cliff, Murro aliniambia yeye ni ofisa wa jeshi na ana nyota tatu na amechukua mafunzo nchini Marekani na Afrika Kusini na ana madaraka ya kunikamata… na baada ya hapo alifungua dashibodi ya gari lake akatoa pingu akaniambia nikimletea vurugu atanifunga na pingu na kisha akanionyeshea bastola pia akaniambia nikifanya vurugu atanifyatulia risasi ili kunidhibiti,” alieleza.
Wage aliendelea kueleza kuwa walipofika tu Hoteli ya Sea Cliff walipokelewa na mtu aliyejitambulisha kuwa ni Kaimu Mkurugenzi wa PCCB, anaitwa Mussa ambapo hata hivyo Wage alimtambua mtu huyo mahakamani kuwa ni Mugassa na akaongeza mtu mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Dokta ambaye Wage jana alimtambua mahakamani kuwa ni Kapama na kuongeza kuwa baada ya hapo mahojiano yakaanza na Dokta akaanza kumueleza kuwa yeye ni fisadi mkubwa na kwamba kama alihitaji msaada wao angesema mapema ili mahojiano yao yasiweze kurushwa kwenye kipindi cha Usiku wa Habari cha TBC1.
“Niliwajibu mimi siyo fisadi; ndipo yule Dokta (mshtakiwa wa pili) akaniambia kuwa hata Liyumba alifungwa jela kwa kuonewa kwani ile kesi ya matumuzi mabaya ya ofisi ya umma, alibambikiziwa kwa kuwa alikuwa akitembea na mpenzi wa rafiki yake anayefanya kazi BoT akamwambukiza maradhi… nilipokea taarifa hiyo kwa mshtuko mkubwa na nikaona wanaweza kunibambika kesi watu hao na siku hiyo nilikuwa na sh milioni moja mfukoni ikabidi nimpatie kiasi hicho cha fedha Kaimu Mkurugenzi wa PCCB (Kapama), mshtakiwa wa pili, ndani ya gari na Murro alikuwa nje ya gari na kuwaahidi kesho yake Januari 31 mwaka jana ningewaletea sh milioni tisa zilizokuwa zimebaki.
“Baada ya kumaliza kuwapatia sh milioni moja, niliingia kwenye gari la Murro akaenda kunishusha mgahawa wa Best Bite na tutakubaliana kesho yake tukutane kwenye mgahawa wa City Garden ulioko mtaa wa Mkwepu… Nikapanda kwenye gari langu nikaenda nyumbani kwangu Bagamoyo nikawaeleza ndugu zangu kuhusu tukio la mimi kutishiwa bastora na kuombwa rushwa; wakaniambia nikatoe taarifa polisi….na kweli Januari 31 mwaka jana, nilivyokuja Dar es Salaam nilifikia moja kwa moja kituo kikuu cha Polisi Kati huku mfukoni nikiwa na sh milioni tisa,” alidai Wage.
Alisema mara baada ya kutoa taarifa hizo polisi wakamtaka ampigie simu Murro na amweleze kuwa tayari ameishafika kwenye mgahawa wa City Garden.
Wage alieleza kuwa alifanya hivyo na baada ya dakika chache Murro aliwasili kwenye mgahawa huo lakini alivyomuona Wage ameambatana na watu wengine watatu alishtuka na polisi waliwahi kuzuia gari lake lisitoke katika viwanja vya mgahawa huo na askari kanzu hao walimwamuru aendeshe gari lake na kulipeleka kituo cha polisi Kati na Murro alitii amri hiyo na wote walifika kituoni hapo.
Alisema Murro alipoulizwa kama alikuwa akimfahamu Wage alikana kumfahamu na polisi hao walipopekuwa gari la Murro walikuta bastola, pingu na miwani ya kusomea ambayo Wage alidai ni yake na aliisahau jana yake wakati alipopanda katika gari hilo wakati anapelekwa Sea Cliff.
Vitu hivyo vyote pingu, bastola na miwani ilipokelewa mahakamani hapo kama utambulisho. Kwa upande wake wakili wa Murro, Richard Rweyongeza, na Majura Magafu, anayemtetea Kapama na Muggasa akimhoji shahidi huyo alidai kuwa shahidi huyo haoni kwamba Murro alikuwa akitangaza habari za hatari hatari za kuligusa jeshi la polisi na alikuwa akitaka kurusha tuhuma za ufisadi zinazomkabili Wage ndiyo maana alishirikiana na polisi kumbambikizia kesi mteja wake, hoja hiyo ilipingwa vikali na shahidi huyo. Leo shahidi wa tatu atahojiwa.


Muandishi: Othman Michuzi | Tarehe: Monday, January 24, 2011
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe akizungumza na vyombo vya habari leo katika mkutano wa ufunguzi wa rasmi wa mchakato wa tuzo za Muziki Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa TBL.kushoto ni Mratibu wa tuzo kutoka BASATA,Angelo Luhala na kulia ni Meneja wa Bia ya Balimi,Edith Bebwa.


KILIMANJARO PREMIUM LAGER na BASATA leo wamezindua rasmi mchakato wa kuwatafuta na kuwa tunza wasanii wa Tanzania waliofanya vizuri kupitia kazi zao za Muziki kwa mwaka wa 2010.

Mwaka jana Tunzo hizi za Muziki nchini Tanzania zilifanyiwa mabadiliko makubwa ambayo yataendelezwa na kuboreshwa zaidi mwaka huu. Mchakato wa kuwapata vinara hao utapitia hatua zifuatazo:

1. ACADEMY:
ACADEMY ya Tunzo za Muziki Tanzania ni mkusanyiko wa wadau wa muziki mia moja (100) kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania ambao huwekwa pamoja katika eneo moja kuwawezesha kuchanganua na hatimae kupata wateule (Nominees) wa vinyang’anyiro (categories) mbali mbali. Utaratibu huu haujabadilika na mwaka huu utafanyika tarehe 12 na 13 Februari 2011.

2. Majaji:
Majaji hua na kazi moja kubwa ya kuhakiki uteuzi wa Nominees uliofanyiwa na Academy ikiwa ni pamoja na kura zitakazopigwa na wananchi. Wao hutumia zaidi vigezo halali vinavyopatikana na mkusanyiko wa rekodi za wasanii zilizotoka kwa mwaka 2010, kazi zao za mwaka 2010, Mafanikio n.k n.k. Jopo hili hujumuisha wadau wa muziki 15.

3. KURA:
Kura za wapenzi wa Muziki nazo hujuishwa katika kuchangua washindi. Mwaka huu kura za wapenzi na mashabiki wa wasanii zitabeba asilimia 50 na majaji asilimia 50. Njia za kupiga kura ni pamoja na:
- SMS.
- Email.
- Magazeti.
- Fliers.

Wawezeshaji:
Kilimanjaro Premium inaendelea kufanya kazi na makampuni matatu katika mchakato na uwezeshaji wa Tunzo za Muziki. Makampuni haya ni pamoja na:
1. Digital Arts – Wasimamizi wakuu wa mchakato wa Tunzo.
2. 1Plus Communications – Wasimamizi wa mawasiliano ya wasanii pamoja na umma.
3. Entertainment Masters – Wasimamizi wa burudani na mahitaji yake.
4. Deloitte Management Consulting – Wasimamizi na wahakiki wa mchakato wa upatikanaji wa wateule pamoja na washindi wa Tunzo za Muziki Tanzania.

Maelezo ya ziada:
Mwaka huu Kilimanjaro kama mdhamini imeamua kuwarudishia wadau na wapenzi wa muziki wa Tanzania usiku wa tunzo. Burudani yote ya usiku huo itatolewa na wasanii wa hapa nyumbani tu. Hapatakuwa na msanii kutoka nje ya nchi kwa vile wasanii wetu wa ndani wanaweza na wanatosha ukizingatia ni Tunzo zao.
 

KASHFA NZITO YAIBUKA MWAUWASA: MILIONI 340 ZATAFUNWA NA WAJANJA.

Bodi ya mamlaka ya maji na maji taka jijini Mwanza (MWAUWASA) imeonyeshwa kuchukizwa na upotevu wa shilingi milioni 340 na imekusudia kutomuongezea muda wa mkataba Mkurugenzi wake Justus Rwetebula baada ya kuelekea kumalizika .HUDUMA YA MAJI NYUMBA ZA VILIMA VYA mwanza.

Mmoja kati ya wajumbe ambaye hakupenda jina lake litajwe amesema kuwa kwa ujumla Bodi imechukizwa na namna Mkurugenzi huyo alivyoshindwa kutoa taarifa kwa Bodi juu ya wizi huo uliofanywa na mhasibu wa MWAUWASA Moses Ndaki.

“Mara baada ya wizi huo kutokea Mkurugenzi aliamua kwenda likizo na kumwachia maelezo nusunusu aliyemwachia ofisi, unaweza kuona ni namna gani Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA asivyo makini na kazi yake ndiyo maana wajumbe wa Bodi kwa kauli moja tumeamua kutokumwongezea muda wa kazi baada ya kipindi chake kumalizika hivi karibuni wakati hatua nyingine za kiutendaji zikichukuliwa na mamlaka husika ambazo zimepewa jukumu la kuchunguza wizi huo na kuchukua hatua” alisema mjumbe.

Mjumbe huyo ameongeza kuwa kuna mtandao mkubwa wa wafanyakazi uliofanikisha wizi huo kwani fedha hizo inaonyesha zilikuwa zikiibiwa kwa awamu huku baadhi ya viongozi wakiwa kimya wakijua mchezo
.

Kwa upande wake Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Nonosius Komba amesema kuwa jeshi lake bado linamsaka mhasibu Moses ndaki aliyedaiwa kutoweka kazini baada ya kubainika wizi huo wa milioni 340.

Komba ameongeza kwa kusema kuwa polisi pia kwa kushirikiana na uongozi wa MWAUWASA bado wanachunguza kwa makini tukio zima ili wahusika waweze kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma za wizi huo.

Monday, January 24, 2011

Miss Utalii Tanzania 2010/11 kujizolea milioni 150
Wakati fainali za taifa za shindano la Miss Utalii Tanzania zimepangwa kufanyika usiku wa Februari 5, 2011, mrembo atakayenyakua taji la taifa la Miss Utalii mwaka huu ataondoka na faida kubwa ya zawadi ya mkataba wenye thamani ya shilingi milioni mia moja na hamsini. 

Taarifa iliyotolewa na Rais wa Miss Utalii Tanzania, Gideon Chipungahelo imeeleza kuwa, shindano la mwaka huu litafanyika kwenye hoteli ya kitalii ya Kiromo View Resort iliyopo umbali wa kilometa kumi tu toka Bagamoyo mjini ambapo pia kutakuwa na burudani kadhaa zitakazosindikiza usiku huo adhimu na ya kihistoria katika tasnia nzima ya urembo na utalii hapa Tanzania. 

Akaendelea kusema; washiriki wote wa fainali za Miss Utalii Tanzania 2010/11 wako katika hali nzuri kiafya na kisaikolojia kwa ajili ya shindano na kufafanua kuwa mbali ya kitita hicho kwa Malkia wa mwaka huu, warembo wengine wataweza kujitwalia mataji yatakayowakilisha hifadhi za taifa 16 zilizo chini ya mamlaka ya hifadhi za Taifa (TANAPA). 

Kadhalika, Chipungahelo amesema kuwa mbali ya mataji ya hifadhi, pia, kutakuwa na tuzo zingine toka baadhi ya makampuni na taasisi zilizodhamini shindano hili ili kuyawakilisha katika suala zima la kuutangaza utalii kupitia hifadhi za taifa na utamaduni wa Mtanzania na hivyo kuongeza hamasa zaidi kwa washiriki ambao nao wameonesha kujawa shauku ya kufanya vema.
“Fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania 2010/11, zitakuwa tukio kubwa zaidi la kitaifa la kitamaduni na urembo nchini, ambalo kishindo chake kitaleta mageuzi makubwa katika sanaa ya urembo nchini, barani Afrika na duniani kwa ujumla. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kwa mara ya kwanza dunia itashuhudia idadi kubwa ya warembo wakiwa jukwaa moja wakitangaza na kuonesha utamaduni kupitia mavazi ya asili, ya kitalii, ya mitindo, ya ubunifu. Pia, warembo hao wataonesha vipaji vya kuimba na kucheza nyimbo na ngoma za asili za mikoa au kanda wanazowakilisha,’ amesema Rais wa Miss Utalii Tanzania. 

Aidha, amewataja wadhamini wakuu wa shindano la taifa la Miss Utalii 2010/11 ni Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) ,Business Times Limited, Kiromo View Resort na Sahara Media Group Limited,inayomiliki kituo cha runinga cha Star TV, Radio Free Africa, Kiss FM na gazeti la Msanii Afrika. Wengine ni Zizzou Fashion, Alaisy Travel, Auckland Tours, Tintona TankStation, Tesco Furniture, Mlonge By Makai Enterprises,Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Coco Beach.
Warembo hao wameanza ziara rasmi za kutembelea na kutangaza vivutio vya utalii ,kwa kutembelea maeneo ya kihistoria yaliyopo Mkoani Pwani,ambapo juzi walitembelea Maeneo ya Kihistoria yaliyopo wilayani Bagamoyo ikiwemo Magofu ya Kaole,wakiongozwa na katibu tawala wa wilaya ya Bagamoyo. Aidha jana warembo wote 60 walitembelea na kutangaza Fukwe za Bahari ya Hindi zilizoko mkoani Dar Es Salaam wakiongozwa na Mbunge wa Kinondoni Mh, Idd Azan. wakiwa katika Fukwe wa Coco Beach warembo hao wakiwa wamegawanywa katika timu nne za mpira wa miguu walishindana kusakata kabumbu la Ufukweni hali iliyopelekea kuwa kivutio kikubwa na kusababisha ufukwe huo kufurika mamia ya watu wakishuhudia warembo hao wakionyesha vipaji vya hali ya juu ya kusakata kandanda. michuano baina ya timu hizo za warembo zilizopewa majina ya hifadhi za Taifa ulikuwa mkubwa na kuamsha shangwe za mara kwa mara kwa wapenzi waliojazana kushuhudia mechi hizo. katika mchezo wa kwanza timu ya soka ya warembo wa Ngorongoro iliweza kuibwaga timu ya soka ya Selous kwa mabao 4-2 wakati katika mchezo wa pili ambao ulizikutanisha timu za Serengeti National Park dhidi ya Maunt Kilimanjaro na matokeo timu ya Mlima Kilimanjaro kuibuka kwa ushindi wa mabao 3-1. Mbunge wa Kinondoni Mh, Idd Azan kwa kufurahishwa na viwango vilivyoonyeshwa na timu hizo za warembo wa  miss Utalii Tanzania 2010- 2011 ambao tarehe 5 mwezi wa pili watapanda jukwaani kuwania taji la Miss Utalii Tanzania 2010- 2011 katika Hotel ya Kitalii ya Kiromo Bagamoyo, alinunua kila goli kwa shilingi elfu kumi(10,000) hivyo aliweza kutoa shilingi laki moja kwa magoli kumi yaliyofungwa. naye mfanyabiashara maarufu nchini Zizzou Fashion alitoa seti nne za jezi kwa warembo wote 60. wakati huohuo warembo hao wanatarajia kuanza ziara ndefu ya kutembelea na kutangaza hifadhi za taifa wakiambatana na waandishi wa habari, wapiga picha za Video na Television huku wakitengeneza filamu na makala ya kutangaza hifadhi hizo za taifa Kimataifa na Kitaifa katika ziara itakayoanza jumatano hii iliyopewa jina la Tanzania Great Safari & Tour 2010\2011 


MENGI ATOA ONYO KWA VIONGOZI WA DINI 
MWENYEKITI Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, amewataka viongozi wa dini nchini kuacha kuhubiri kwa kutoa maneno ambayo yanaweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Mengi alisema hayo jana jijini Dar es Salaam katika hafla ya chakula cha mchana na watu wenye ulemavu.
“Ninawaomba viongozi wa dini zote nchini kutohubiri kwa kutoa maneno ambayo kwa namna moja ama nyingine yanaweza kuwa chanzo cha kuhatarisha amani na utulivu wa nchi,” alisema.
Mwenyekiti huyo alisema pindi kunapotokea uvunjifu wa amani kundi la walemavu huwa la kwanza kuathirika.
Alisema amani na utulivu uliopo nchini unatakiwa kuwa endelevu ili nchi iendelee kusifiwa ndani na nje.
Aliongeza kwamba walemavu wanaweza kupata fursa sawa na kundi lingine la jamii endapo suala la amani na utulivu litazidi kushamiri nchini.
“Kwa niaba ya kundi hili na wengine wote nchini, ninatoa rai ya kuwataka kudumishwa kwa amani na utulivu nchini,” alisema Mengi.
Awali, Mwakilishi wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (Shivyawata), Lupi Naswanya, alisema wanahitaji Katiba mpya kwa maslahi ya taifa na jamii hiyo kwa ujumla.
Lupi alisema serikali haina budi kuwashirikisha katika mchakato wa kuandaa Katiba mpya kama moja ya jamii ya Watanzania.
“Tunahitaji kushirikishwa katika mchakato wa kuandaa Katiba mpya, Katiba iliyopo inahitaji mabadiliko makubwa kutokana na kutotupa fursa sawa katika jamii,” alisema.
Aliongeza kwamba endapo Katiba itakuwa nzuri, jamii yote itaboreka, hivyo bado kunahitajika maboresho katika Katiba ya sasa,” alisema.
Mengi amekuwa na utaratibu wa kila mwaka wa kuandaa tafrija kwa ajili ya jamii ya watu wenye ulemavu na kupata nao chakula cha mchana na kubadilishana nao mawazo.


Don't Wear British!

OSCAR DE LA RENTA has criticised Michelle Obama for wearing an Alexander McQueen gown to the state dinner with Chinese President Hu Jintao. Obama also wore a dress and coat by London-based designer Roksanda Ilincic during the visit.
SEE MICHELLE OBAMA'S STYLE CHOICES

"My understanding," de la Renta said, "is that the visit was to promote American-Chinese trade — American products in China and Chinese products in America. Why do you wear European clothes?"
But de la Renta - who has criticised Mrs Obama's fashion choices before - insists it isn't a case of sour grapes.
"I'm not talking about my clothes, my business," he told WWD. "I'm old, and I don't need it. But there are a lot of young people, very talented people here who do."

Best Dressed Of The Week - 21/01/2011

WITH awards season in full swing, there was plenty of red carpet fashion moments this week. At the Critics' Choice Awards in LA, Livia Firth showed that ethical fashion can look as good as it is for the planet, while 12-year-old Elle Fanning (in Valentino), Emily Blunt (in Azarro), and Tilda Swinton (in Lanvin), also impressed us. 
 
  GEMMA ARTERTON-AMERICANSEXY FASION MODEL

Bw" Ghannouchi" atakiwa kujiuzulu-Tunisia

Maandamano ya kuipinga serikali ya mpito nchini Tunisia yanaendelea kumshinkiza Waziri Mkuu Mohammed Ghannouchi kuachia madaraka.
Waandamanaji Tunisia
Waandamanaji Tunisia
Waandamanaji takriban 1,000 kutoka maeneo ya vijijini nchini Tunisia wamefika mji mkuu Tunis, na kujiunga na waandamanaji wengine wakitaka waziri mkuu Mohamed Ghannouchi na baraza lake wajiuzulu.
Watu hao walianza kuandamana katika eneo la asili la Mohamed Bouazizi, kijana ambaye kifo chake ndicho kilichoanzisha ghasia zilizosababisha Rais Ben Ali kukimbia siku kumi baadae.
Waratibu wa maandamano hayo wamesema wataendelea kukaa nje ya makao makuu ya serikali mjini Tunis, mpaka mawaziri wote wenye uhusiano na Bwana Ben Ali watakapotolewa madarakani.
Bw Ghannouchi ameahidi kung'atuka madarakani baada ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika baada ya miezi sita.
Chama cha wafanyakazi maarufu nchini Tunisisa, UGTT, kimeunga mkono maandamano hayo yaliyoanza Jumamosi mjini Menzekl Bouzaiane - mji ulioshuhudia kifo cha kijana huyo mwezi wa Disemba.
'Lengo la maandamano haya ni kuiangusha serikali,' alisema Rabia Slimane, ambaye ni mwalimu na anashiriki katika maandamano hayo.
Waombolezaji Tunisia
Waombolezaji Tunisia
Maombolezi yanafanyika leo Jumapili kwa waliofariki dunia katika vurugu zilizosababisha Ben Ali kukimbia.
Kuna hisia kuwa maandamano ya aina hii yataanza katika nchi zingine.
Nchini Algeria, polisi waliwatawanya takriban waandamanaji 300 waliokuwa wakitetea haki ya kuwa na uhuru zaidi, siku ya Jumamosi.
Pia, kumekuwa na maadamano nchini Yemen dhidi ya utawala wa Rais Ali Abdullah Saleh.


MAMBO YA MAPACHA WATAU -MZALENDO PUB
Hizi ni bata za weekend hii na bendi ya mapacha watatu