Pages

Pages

Thursday, February 17, 2011

MABOMU GONGO LA MBOTO: WATU 200 WAJERUHIWA,20 WAPOTEZA MAISHA

Hii ndiyo hali halisi ya ualibifu wa mali na makazi huko gongo la mbo jijini Dar es salaam
   Hapo jana mji ulikuwa namna hii full taharuki huku moto mkubwa ukionekana tokea gongo la mboto katika kambi ya jeshi.

Katika hali isiyo ya kawaida usiku wa tarehe 16 mida ya saa mbili na dakika ishirini ulianza kusika milio ya mabomu kutoka katika gara la siraha lililopo katika kambi ya jeshi ya gongo la mboto,aidha yapata zaidi ya watu 20 kupoza maisha ikiwa zaidi ya watu 200 wamejeruhiwa na mabumu na wengine wameumia wakati wakijinusur na mkasa huo.
   Hili ni moja ya bolilikutwa limelipuka jana usiku
  watun kadhaa waliojeruhiwa na mabomu wakipata msaada toka kwa askari na waugzi

WAKATI HUOHUO:
Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania limeairisha kiao chake cha leo kutokana na milipuko hiyo ambayo imekuwa janga la kitaifa baada ya watu kadhaa kupoteza maisha na uharibifu wa mali ikwa wengine wameibiwa na kupoteza ndugu zao kwa muda.

WAKATI HUOHUO:
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania MH. J.K.KIKWETE ameitisha kikao cha dharula cha kamati ya ulinzi na usalama leo.

Polisi wakabiliana na waandamanaji Bahhrain

Waandamanaji nchini Bahrain
Waandamanaji nchini Bahrain
Maafisa wa usalama katika Himaya ya Bahrain wametumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji wanaopinga Serikali ambao wamepiga kambi katika bustani kati kati mwa mji mkuu wa Manama.
Walioshuhudia maandamano hayo wanasema polisi waliwasili wakati waandamanaji walikuwa wakijiandaa kulala.
Makundi ya upinzani yanasema kuwa watu wawili walifariki na wengine wengi kujeruhiwa.
Wanasema polisi waliwasili mahala hapo na kuanza kuwarushia mabomu ya kutoa machozi na wakati huo huo kufyatua risasi za mipira; jambo lililowafanya watu kukimbilia mitaa iliyo karibu.
Jana maelfu ya waandamanaji walishiriki kwenye maandamano ya kupinga serikali kwa siku ya tatu mfululizo katika mji mkuu wa Manama.


ANNA MAKINDA ATAKIWA AJIUZULU AMA APIGE GOTI

SPIKA wa Bunge la Muungano, Anne Makinda, ametakiwa kuomba radhi au kujiuzulu nafasi yake kutokana na kutoa kauli ya kudhalilisha vyombo vya habari.
Akizungumza jana na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam, Mchungaji William Mwamalanga wa Kanisa la Pentekoste, lenye makao yake makuu mkoani Mbeya, alisema kuwa Makinda anapaswa aombe radhi kabla ya kuanza kwa kikao cha Bunge.
Alisema ni jambo la hatari kwa kiongozi kama Makinda kutoa kauli ya kudhalilisha vyombo vya habari wakati ndiyo sehemu ya wananchi ya kuwasilishia kero zao.
Mwamalanga alisema kuwa vyombo vya habari ni moyo wa nchi, hasa kwa kuibua kero mbalimbali na hata kufikiwa kwa maendeleo.
“Vyombo vya habari si moyo tu bali ni daraja la kufikiwa kwa maendeleo yoyote…hata wapo baadhi ya viongozi akiwamo Rais Jakaya Kikwete wanapata taarifa nyingi kupitia magazetini, hivyo kauli ya Makinda imelidhalilisha taifa,” alisema.
Alisema kauli hiyo ya Makinda imeonyesha taswira kuwa hatakuwa tayari kuendesha Bunge kwa masilahi ya wananchi bali atatekeleza matakwa ya wachache hasa mafisadi.
Alifafanua kuwa wananchi walitegemea kuona Spika Makinda akiwahimiza wabunge wasome na kupitia taarifa mbalimbali zinazotolewa na vyombo vya habari ili kuweza kujipanga namna ya kuchukua hatua.
“Nakumbuka aliyewahi kuwa Waziri Mkuu hayati Edward Sokoine alisikia taarifa za wananchi kunyimwa mbolea huko Makambako akalazimika kwenda wilayani humo na kuwasimamisha kazi baadhi ya viongozi, hii ilitokana na taarifa ya vyombo vya habari…sasa iweje Spika Makinda avidhalilishe vyombo hivyo?” alihoji.
Alisema kitendo hicho kimeashiria kuwa Bunge hilo litakuwa kama la walevi kutokana na kuvidharau vyombo vinavyowasaidia kujua kero za wananchi walioko katika majimbo yao.
Mwanzoni mwa wiki, Spika Makinda alitoa ufafanuzi wa makala ya gazeti moja la kila siku, (si Tanzania Daima), alisema gazeti hilo liliandika uongo na kupotosha ukweli, hivyo aliwataka wabunge kuyasoma magazeti kama barua nyingine za kawaida.

Waziri Habineza wa Rwanda ajiuzulu


Joseph Habineza
Waziri wa michezo na utamaduni nchini Rwanda Joseph Habineza amejiuzulu.
Hakuna sababu rasmi iliyotolewa kuhusu kujiuzulu kwake lakini hatua hiyo imefanyika siku chache tu baada ya kuhusishwa katika kashfa ya ngono.
Vyombo vya habari nchini humo vilisambaza picha kadhaa alizopigwa akiwa na wasichana kadhaa wakistarehe kwenye nyumba moja mjini Kigali.


FILAMU YA SHOGA YAPIGWA STOP !!

Bodi kuu inayoshughulikia masuala ya Filamu Nchini wametoa tamko la kuizuia Filamu ya SHOGA iliyoandaliwa na Msanii Hissani Muya Almaarufu Tino isiingizwe sokoni mpaka ikaguliwe kuona kwamba inakidhi Mila, Desturi na Tamaduni zetu za Kitanzania Ndipo iruhusiwe kutoka.

Wale wapenzi ambao walikuwa wanasubiria kwa hamu kuona nini kilichoandaliwa ndani ya filamu hiyo wanaombwa kuwa wastahimilivu mpaka ukaguzi huo utakapokamilika ndipo filamu hiyo itakopoachiwa na kuingizwa sokon

No comments:

Post a Comment