Pages

Pages

Wednesday, February 16, 2011

LIBYA YAKUMBWA NA MAANDAMANO MAKUBWA


Muammar Gaddafi, Rais wa Libya
Mamia ya watu wamepambana na polisi na wale wanaoiunga mkono serikali katika mji wa Benghazi nchini Libya.
Walioshuhudia wameiambia BBC ghasia hizo zilizoibuka usiku zilitokana na kukamatwa kwa mkosoaji mkubwa wa serikali.
Wakili wa mkosoaji huyo baadae alisema kuwa ameachiliwa huru lakini maandamano yakaendelea.
Maandamano ya kuunga mkono demokrasia yameibuka nchi kadhaa za kiarabu katika wiki za hivi karibuni, iliyowalazimisha viongozi wa Tunisa na Misri kuachia madaraka.
Wito umetolewa kwenye mtandao kuwepo kwa maandamano nchini Libya siku ya Alhamis.

'Polisi kujeruhiwa'

Hakuna uthibitisho wa kuwepo maandamano Benghazi, lakini walioshuhudia wanasema katika hatua moja takriban watu 2,000 walihusika.
Walisema polisi walitupiwa mawe ambao inasemekana walijibu mapigo kwa kuwamwagia maji, mabomu ya machozi na risasi za mpira.
Baadae picha ya video ya ghasia hizo iliwekwa kwenye mtandao.
Sehemu ya video hiyo iliwekwa kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook- ambapo imewekwa na mtu anayedai ilirekodiwa siku ya Jumanne- ilionyesha watu wakishangilia nje ambapo palionekana kama kituo cha polisi.
Milio ya risasi ilikuwa ikisikika, na baadae anaonekana mtu mmoja aliyejeruhiwa akiondoshwa kwenye ghasia hizo.
Televisheni ya taifa ya Libya ilionyesha mamia ya watu huko Benghazi wakiunga mkono serikali.
Mpaka sasa serikali haijatoa kauli yeyote kuhusiana na matukio ya mji huo wa bandari, uliopo takriban kilomita 1,000 mashariki mwa mji mkuu wa Tripoli.
Gazeti la binafsi la Libya kupitia mtandao Quryna limeripoti kuwa, watu 14 walijeruhiwa, wakiwemo maafisa wa polisi 10.


MH.SHIBUDA AULA  !!
http://www.ippmedia.com/media/picture/large/Shibuda(5).jpg
BUNGE limempitisha bila kupingwa Mbunge wa Maswa Mashariki, John Shibuda (CHADEMA), kuwa mwakilishi wao katika Bodi ya Mpango wa Tathmini ya Utawala Bora Afrika (APRM).
Kabla ya kupita bila kupingwa Shibuda alikuwa akishindana na Mbunge wa Viti Maalum Martha Umbula (CCM), aliyeamua kujitoa muda mfupi kabla ya uchaguzi.
Pamoja na Shibuda ulifanyika uchaguzi wa Makamishna wa Tume ya Utumishi ya Bunge ambapo waliogombea nafasi hiyo ni wabunge 14 kati ya wabunge 350 waliopo.
Uchaguzi huo ulifanyika juzi jioni ambapo idadi ya wabunge waliokuwepo wakati wa kupiga kura ni 294 huku waliochaguliwa wakiwa ni wabunge watano, wanne kutoka CCM na mmoja kutoka NCCR-Mageuzi.
Waliochaguliwa kuwawakilisha ni Mbunge wa Mbozi Mashariki Godfrey Zambi (CCM) aliyepata kura 250; Mbunge wa Mafia Abdulkarim Shaha (CCM) aliyepata kura 270; Mbunge wa Viti Maalum Dk. Maua Daftari (CCM) aliyepata kura 243; na Mbunge wa Kilindi Beatrice Shelukindo (CCM) aliyejinyakulia kura 221.
Kwa upande wa wapinzani walioshindana ni Mbunge wa Kasulu Mashariki, Agripina Buyogela (NCCR-Mageuzi) aliyepata kura 200 akimshinda mpinzani wake ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum, Mhonga Ruhwanya (CHADEMA) aliyepata kura 85.
Wengine waliogombea na kushindwa ni wabunge wa Viti Maalum kutoka CCM ambao ni Diana Chilolo, Kidawa Salehe na Hilda Ngoye ambapo Mhttp://www.blogger.com/post-edit.g?blogID=6314851553777364113&postID=1402286946843841773bunge wa Wawi Hamad Rashid Mohamed (CUF) alipita bila kupingwa kuwa mjumbe wa tume hiyo baada ya Shibula kujitoa katika kinyang’anyiro hicho hatua za mwisho.


No comments:

Post a Comment