Pages

Pages

Friday, February 4, 2011

MGOMO WA WASOMI CHUO KIKUU WAPAMBA MOTO..!!

Askari wa kutuliza ghasia (FFU) wakifyatua mabomu ili kuwatawanya wanachuo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, waliokuwa wakiandamana leo asubuhi kuelekea Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ajili ya kufikisha malalamiko yao ya posho ya Sh 5,000/ ambayo wanadai ni ndogo haitoshi kwa matumizi na badala yake wanaishinikiza Serikali kuwapa Sh. 10,000/=. Hata hivyo maandamano hayo yaliishia maeneo ya Savei baada ya kukuta ukuta wa polisi hao umetanda Barabarani huku wakitoa matangazo ya kusitisha maandamano hayo na kutawanyika, baada ya kutoa matangazo hayo na wanafunzi hao waliendelea kuwa maeneo hayo huku wakiimba ndipo askari hao waliamuliwa kuanza kufyatua mabomu ili kuwatawanya. Katika tukio hilo hakuna aliyejeruhiwa ila ni wanafunzi wachache tu waliokamatwa.
Bomu la machozi limeshaachiwa hapa likianza kufyatuka...
Wanafunzi hao wakitawanyika kwa kukimbia kila mtu na njia yake baada ya mabomu kuanza kufyatuliwa.
Wanafunzi hao wakiandamana, kutoka chuoni...
Wakiwa na mabango yao yenye ujumbe kuhusu kile wanachodai na wasichohitaji.
Safari ilikuwa ni ndefu huku wakitembe, kukimbia na kuimba ili kuifanya safari hiyo kuwa fupi zaid lakini waaapi, iliishia karibu zaidi.
Maandamano bado yalikuwa yakiendelea kutokea chuoni hapo.
Mkusanyiko ulianza kama hivi...

HII NDIYO HALI HALISI YA VURUGU NCHINI MISRI 
Wafuasi wa Rais wa Misri, Hosni Mubarak wamekabiliana na waandamanaji wanaomtaka kiongozi huyo aondoke madarakani katikati mwa mji wa Cairo.Maelfu ya wafuasi wa Bw Mubarak walimiminika kwenye eneo la Tahrir na kuondoa vizuizi vilivyokuwa vimewekwa na waandamanaji.
Pande hizo mbili zilirushiana maneno kabla ya kuanza kurushiana mawe. Kuna Taarifa ambazo hazijathibitishwa zinasema maafisa wa polisi waliokuwa wamevalia kiraia walikuwa miongoni mwa baadhi ya wafuasi wa Bw Mubarak waliojitokeza katika eneo la Tahrir.
Athari za vurugu hizo.watu wengi wamejeruhiwa sababu ya haki,haki iko wapi...??

Waandamanaji wanataka Rais Hosni Mubarak aondoke madarakani baada ya kutawala kwa muda wa miaka 30.Hii ni dalili ya kuchoshwa na utawala wa mabavu,mmoja wa waandamaji akiwa anaonyesha picha ya raisi huyo.
Mjini Cairo kwenyewe helikopta za kijeshi zimeendelea kuzunguka angani karibu na bustani ambapo maelfu ya watu walikusanyika licha ya amri ya kutotoka nje usiku iliyotangazwa na serikali.

No comments:

Post a Comment