Pages

Pages

Friday, February 4, 2011

LIVE BILA CHENGA: RAIS KIKWETE AMTOLEA MACHO MBOWE ...!!

Tukio hilo la aina yake kutokea tangu kuanza kwa mwaka huu, liliwakutanisha Mbowe na Rais Kikwete katika maadhimisho ya Siku ya Sheria yaliyofanyika jijini Dar es Salaam ambapo walisalimiana kwa kupeana mikono.

Mbowe na Kikwete walikutana uso kwa uso ikiwa ni siku 85 tangu Mbowe alipowaongoza wabunge wa chama chake kususia hotuba yake ya uzinduzi wa Bunge la 10, Novemba 18 mwaka 2010 kutokana na msimamo wa chama chake kutotambua matokeo ya urais.

Mwaka jana, Mbowe alitangaza chama chake kutotambua matokeo ya rais huku akitoa madai mbalimbali kuhusu taratibu zilizotumika kumwingiza kiongozi huyo madarakani.

Katika tukio la kupiga picha za pamoja ndipo Mbowe alikutana uso kwa uso na Rais Kikwete ambapo walisalimiana kwa kupeana mikono na kupiga picha pamoja huku wote wakiwa na tabasamu pana.

Alipotafutwa na gazeti la Mwananchi (wanyetishaji wa inshu hii) ili kuzungumzia tukio hilo, saa kadhaa baada ya kumalizika kwa sherehe hizo, Mbowe alisema alikwenda katika sherehe hizo kwa kuwa zilikuwa ni za mahakama na kwamba hata kungekuwa na tofauti gani kusingemzuia yeye kusalimiana na Kikwete.

"Sherehe zile si zangu wala Rais Kikwete hivyo siwezi kuwa na chuki na mahakama, ni 'Birthday' ya Mahakama yenyewe ni mhimili wa dola," alisema Mbowe.

Mbowe alisema kuwa katika maadhimisho hayo alialikwa kama mwenyekiti wa Chadema na kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni.

Mbowe alisema kuwa madai waliyotoa baada ya Uchaguzi Mkuu mwaka jana haikuwa na maana kwamba hawaitambui Serikali wala kutaka Rais Kikwete ang’oke madarakani.

Alisema kuwa mambo mawili kati ya matatu yaliyokuwemo katika dai lao yameshaanza kupatiwa ufumbuzi kwa namba moja au nyingine ambayo ni katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.



DOWANS YAINGIA NEPAL:Taarifa ya habari yasomwa gizani

Taarifa ya habari gizani
''Ifuatayo ni taarifa ya habari ikisomewa gizani, kwa kuwa umeme umekatwa.'' 

Mojawapo wa vituo vikuu vya televisheni nchini Nepal kimeanza kutangaza taarifa zake za habari za usiku katika mazingira ya nusu kiza ili kubainisha athari za ukataji mkubwa wa umeme.
Tangu mwanzoni mwa mwezi wa February, kituo cha televisheni cha Kantipur kimetumia taaa zinazotumia mafuta kutoa mwanga wakati wa taarifa yake ya habari ya dakika 30 saa moja usiku.
Mkuu wa kituo hicho alisema shabaha ni kutia shinikizo kwa serikali ikabiliane na tatizo hili.
Kwa sasa Nepal inakabiliwa na mpango wa kukata umeme kwa saa 12 kila siku.
"tunaitaka serikali izalishe umeme zaidi kwa haraka" mkuu wa Kantipur News Tirtha Koirala aliiambia BBC.
"hadi sasa watazamji wetu wamepokea vizuri hatua hii;lakini serikali bado haijasema chochote."
Licha ya kuwa na uwezo mkubwa wa kuzalisha umeme kutokana na mito, Nepal huzalisha nusu tu ya mahitaji yake ya umeme.
Miaka kumi ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya waasi wa Kimao na serikali ya Nepal vilivyomalizika mnamo mwaka 2006, imemaanisha uwekezaji mdogo sana katika sekta ya umeme ya Nepal.
Juu ya yote hayo mtandao wa kusambaza umeme nchini uliathiriwa vibaya sana baada ya kuharibiwa na mafuriko ya mto Kosi mnamo mwaka 2008.
Hii imesababisha kuwepo na mgawo wa umeme kuwa ni jambo la kawaida katika maisha ya kila siku.
Tatizo ni kubwa zaidi katika majira ya baridi ambapo ukosefu wa mvua na kina cha chini cha mito inamaanisha mabwawa yaliyopo hayawezi kuendesha shughuli zao kikamilifu.
Mamlaka ya nguvu za umeme ya Nepal yanayomilikiwa na serikali yamesema kuwa nchi inaweza kutazamia kukatwa umeme kwa kipindi cha saa 14 kila siku katika muda wa wiki chache zijazo.
"tunasumbuka sana kwa sababu ya mgawo wa umeme ," amesema Bwana Koirala .
"Takriban wanafunzi 400,000 hivi sasa wanajitayarisha kwa mtihani wa shule za sekondari na hawana mwanga wowote wa taa usiku".
"Halikadhalika wafanyibiashara wadogo wadogo ambao hawawezi kumudu jenereta au kifaa cha "inverter"nao pia hawawezi kuendesha shughuli zao."
Bwana Koirala alisema taarifa za habari za kituo chake zitaendelea kutangazwa katika mazingira ya kiza mpaka serikali itakapochukua hatua .

Tangu niingie kwenye ndoa yangu sisikii hamu ya tendo la ndoa

 DAKTARI...anajibu kama ifuatavyo...

Naomba niliongelee jambo hili kwa kina zaidi kwa upande wa wanaume kwani baadhi yaao walio katika ndoa siyo waaminifu huwa na nyumba ndogo au wapenzi kiasi cha kushindwa kutimiza wajibu wao nyumbani hali hii huwaathiri wanawake kisaikolojia.
Mwanaume mkorofi kila anaporudi nyumbani yeye na pombe zake kichwani ni kuanza kumkong’oli mke wake tena mbele ya watoto wao jamani hii ni adabu kweli? Baadhi ya wanaume ni wagomvi na wakorofi kwa wake zao hivyo husababisha mwanamke aathirike kisaikolojia kwani kila akimuona mumewe huona kero na taabu inakuja.

Sababu za kiafya nazo pia huchangia sana jambo hili wakati mwingine unakuta mwanamke anaumwa na mwanaume anaporudi tu yeye ndio kazi bila kujali kwamba mkewe ana matatizo gani ndido maana nasema kwamba wakati tunapotenda tendo hili basi tuweke akili zetu katika hili na sio kufikiria maudhi.

No comments:

Post a Comment